RFI Kiswahili
Gurudumu la Uchumi
Fahamu masuala kadha wa kadha kuhusu uchumi kama vile, namna ya kupambana na umaskini, mfumuko wa bei, kushamiri kwa matumizi ya dola na athari za kuyumba kwa uchumi wa dunia kwa nchi za Afrika. Mada hizi zinafanyiwa utafiti wa kina na zinazungumzwa kwa lugha rahisi inayoeleweka ili kukufanya uelewe na usichoke kusikiliza .
Where to listen?
Podcasts in the app Replaio Radio Coming soonPodcasts are coming to the app soon. Install now and be the first to see a whole new take on podcasts
Episodes
Kodi na Maendeleo: Je, tunapata thamani ya kodi tunazolipa? 08.07.2026 9:56
Katika makala ya Gurudumu la Uchumi hivi leo, tunajadili nafasi ya kodi katika maendeleo ya uchumi, umuhimu wa kulipa kodi, na jinsi serikali na wananchi wanavyoweza kushirikiana kujenga uchumi imara na wenye manufaa kwa wote.
Je, kukopa kunasaidia ukuaji wa uchumi au kunaleta hatari za siku zijazo? 24.06.2026 10:04
Msikilizaji nchi nyingi za Afrika Mashariki zimeendelea kukopa ili kufadhili maendeleo, na huku wadau wengine wakisema mikopo ni muhimu kwa ukuaji wa uchumi, Wengine wanaonya kuwa madeni yanapoongezeka kupita kiasi, serikali hulazimika kutumia fedha nyingi kulipa madeni hayo badala ya kuboresha huduma muhimu kama vile afya, elimu na ajira. Katika Makala ya Gurumu la Uchumi hivi leo, tunauliza: Je,...
Kutoka taslimu hadi kidijitali: Namna simu zinavyobadili mfumo wa malipo Afrika 10.06.2026 10:03
Ufanyaji biashara na utumaji wa fedha kwa njia ya simu za kiganjani barani Afrika unakua kwa kasi, pochi za simu zimerekodi takriban asilimia 19 ya uingiaji wa pesa kwenye eneo la Kusini mwa Jangwa la Sahara, huku wastani wa gharama ya utumaji pesa ukishuka hadi karibu asilimia 3.54 hii ni kwa mujibu wa benki ya dunia. Kwanye Makala ya Gurudumu la uchumi wiki hii, tunaangazia matumizi ya telknoloj...
Sekta ya maua Kenya yatikiswa na gharama na kuyumba kwa masoko ya kimataifa 04.06.2026 9:55
Msikilizaji Sekta ya maua nchini Kenya, ambayo kwa muda mrefu imekuwa miongoni mwa nguzo muhimu za uchumi na chanzo kikuu cha mapato ya fedha za kigeni, ikiingizia nchi zaidi ya dola bilioni moja za Marekani kila mwaka, sasa inakabiliwa na changamoto zinazotia wasiwasi kuhusu mustakabali wake.
Umuhimu wa bara la Afrika kufanya biashara za ndani 03.06.2026 10:01
Katika makala ya wiki hii, tunajadili ni kwanini nchi za Afrika zinapaswa kuongeza kasi ya ufanyaji wa biashara za wenyewe kwa wenyewe kukuza utangamano wa kikanda.
Mkutano wa 'Africa Forward' una maana gani kwa mustakabali wa Afrika 06.05.2026 9:57
Tarehe 11 na 12 ya wiki ijayo, Jiji la Nairobi, Kenya litakuwa mwenyeji wa mkutano wa kwanza wa kihistoria wa ‘Africa Forward’ kati ya Ufaransa na Afrika, mkutano ambao unafanyika kwenye nchi inazungumza Kingereza, ambapo viongozi wa Afrika, wafanyabiashara na wabunifu vijana kutoka Afrika na Ufaransa watakongamana kwa siku mbili. Kwenye Makala ya Gurudumu la Uchumi hivi leo tunaangazia uhusiano m...
Akili unde na mustakabali wa uchumi wa Afrika: Fursa mpya kwa vijana wabunifu 22.04.2026 10:01
Katika kipindi ambacho Afrika inaendelea kukabiliana na changamoto za kiuchumi na kijamii, teknolojia ya Akili Unde (AI) inaibuka kama nyenzo muhimu ya kuleta mabadiliko. Kutoka kilimo hadi afya, na kutoka elimu hadi utawala bora, ubunifu wa kidijitali unaanza kubadilisha namna matatizo ya muda mrefu yanavyotatuliwa. Katika makala hii, tunazungumza na Kevin Obote kijana mbunifu wa teknolojia ambay...
Kwa nini vikwazo vya usafirishaji ni kizuizi kikubwa cha biashara Afrika Mashariki 01.04.2026 9:59
Kupitia ripoti iliyozinduliwa juma hili na shirikisho la wazalishaji nchini Kenya, inaonyesha kuwa kusafirisha bidhaa katika njia muhimu za biashara za Afrika bado ni ghali na haitabiriki, ambapo wakati mwingine hugharimu hadi dola 7,000 za Marekani kwa kontena moja kati ya Nairobi na Lusaka. Kwenye Makala ya Gurudumu la Uchumi juma hili, tumezungumza na Tobias Alando, mkurugenzi mtendaji wa shiri...
Uwazi kwenye ubinafsishaji wa mashirika ya uma ni muhimu kwa maendeleo 11.03.2026 10:03
Msikilizaji Katika miaka ya hivi karibuni, nchi nyingi za Afrika Mashariki zimekuwa zikifanya mageuzi makubwa ya kiuchumi. Mojawapo ya mageuzi hayo ni ubinafsishaji wa mashirika ya umma. Leo tunajiuliza, Je, ubinafsishaji ni kweli unasaidia uchumi kukua, au serikali inapaswa kubaki na umiliki wa mashirika muhimu?
Vita ya Iran: Afrika imejipangaje kukabiliana na athari za kiuchumi 04.03.2026 10:03
Msikilizaji mara zote mgogoro wa mashariki ya kati, umekuwa na athari hasi za kiuchumi na biashara duniani, Swali kubwa tunajiuliza hivi leo ni Je, Afrika iko salama kiasi gani? Vita hivi vitaathiri vipi uchumi wa dunia — na gharama za maisha kwa mwananchi wa kawaida barani Afrika?
Ushirikishwaji wa wanawake katika sekta za kiuchumi chanzo cha ukuaji wa uchumi 25.02.2026 10:01
Benki ya Dunia inasema hata katika nchi zenye sheria za kisasa kuhusu usawa kazini, nchi hizo zimeshindwa kuzitekeleza, hadi sasa hakuna nchi iliyofikia kiwango cha juu cha usawa kazini, n ani asilimia kidogo tu ya wanawake wanaishi kwenye nchi zenye angalau sheria bora, huku mataifa 70 ikiwemo Misri, Madagascra na Somalia zikipiga hatua katika kuboresha mazingira ya usawa kati yam waka 2023 na 20...
Ushirikiano wa kikanda hatarini: Nakisi ya bajeti yaibua maswali mapya 18.02.2026 9:47
Juma hili tunajadili kuhusu mustakabali wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, hasa wakati huu kukiwa na taarifa kuwa inakabiliwa na mgogoro wa kifedha. Taarifa zinaonesha kuwa Jumuiya hiyo inakabiliwa na upungufu wa bajeti unaofikia karibu dola za marekani milioni 89, pengo ambalo huenda likatatiza shughuli za Jumuiya hiyo, jambo ambalo limemfanya rais wa Kenya William Ruto ambaye ni mwenyekiti wa jumui...
Dubai: Viongozi wa dunia waangazia mageuzi ya sera, ubunifu na mifumo mipya ya utawala 05.02.2026 9:59
Mkutano wa siku tatu wa Serikali za Dunia mwaka 2026 huko Dubai umesisitiza kuhusu udhibiti wa Akili Mnemba, AI, mageuzi ya kidijitali, uchumi endelevu na thabiti duniani. Viongozi mbalimbali wametoa wito wa kuwepo ushirikiano thabiti wa kimataifa na mifumo mipya ya utawala inayoweza kutazamia changamoto za siku zijazo lakini pia kushughulikia masuala ya pamoja kama vile mabadiliko ya hali ya he...
Ushindani wa mataifa makubwa na mustakabali wa uchumi wa Dunia 21.01.2026 10:01
Msikilizaji mataifa makubwa kama Marekani, China, Urusi na Ulaya yanaendelea kushindana kiuchumi, kuanzia kwenye biashara, teknolojia, nishati na rasilimali. Lakini je, ushindani wao unaathiri vipi uchumi wa dunia? Leo kwenye Makala ya Gurudumu la Uchumi tunajadili, “Athari za Kiuchumi kwa Dunia Zitokanazo na Ushindani wa Maslahi ya Kiuchumi kati ya Mataifa Makubwa.”
Kenya Kuwa Singapore ya Afrika: Ndoto au Uhalisia? 14.01.2026 9:55
Msikilizaji Rais wa Kenya, William Ruto, ameendelea kusisitiza azma ya kuifanya nchi yake kuwa Singapore ya Afrika, suala ambalo limeibua mjadala mkali nchini humo baadhi wakisema ni suala ambalo halitawezekana chini ya utawala wake na wengine wakiona ni jambo linalowezekana. Kwenye makala yetu leo tunajiuliza, je, Kenya inaelekea huko? Ndoto hii inawezekana au ni siasa?
Kutoka Ufugaji wa Mifugo hadi Samaki: Mabadiliko ya Kiuchumi Kajiado 07.01.2026 9:58
Msikilizaji jamii ya Wamaasai kwa muda mrefu imekuwa ikitegemea ufugaji wa mifugo kama chanzo kikuu cha riziki na chakula, hata hivyo, mabadiliko ya tabianchi yaliyoambatana na ukame wa mara kwa mara yamilazimisha jamii hii kutafuta mbinu mbadala za kujipatia kipato, mojawapo ni ufugaji wa samaki.
Sherehe za mwisho wa mwaka zisikuache bila pesa, fahamu mbinu za kudhibiti matumizi yako. 24.12.2025 10:00
Tunapofika mwisho wa mwaka, jamii huingia katika kipindi cha sikukuu kama krismasi na mwaka mpya, ni wakati wa furaha, sherehe na kukutana na familia, lakini pia ni kipindi ambacho matumizi ya fedha huongezeka, watu wengi hujikuta wakitumia zaidi ya uwezo wao na mipango kusimama, tunajadili namna gani unaweza kuwa na nidhamu ya matumizi ya mwisho wa mwaka iwe kwa muajiriwa, mjasiriamali au mfanyab...
Ripoti ya Oxfam-Kenya: Uchumi unakua, lakini Wakenya wengi ni masikini, kwa nini? 03.12.2025 9:58
Msikilizaji juma lililopita shirika la kimataifa la kupambana na umasikini, OXFAM nchini Kenya, ilichapisha ripoti inayoonesha kuongezeka kwa pengo la usawa. Kwa mujibu wa shirika hilo, pengo la walionacho na wasio nacho linaendelea kuongezeka ambapo matajiri 125 wa Kenya kwa sasa wana utajiri wa zaidi ya watu milioni 42 raia wa Kenya. Tunajiuliza, kwa nini ukuaji wa uchumi hauwahusu watu wengi?
Mapinduzi ya Elimu Bondo: Jinsi Teknolojia Inavyowawezesha Wasichana Kuandika Kesho Yao 26.11.2025 10:04
Katika maeneo mengi nchini, hasa magharibi mwa Kenya, wasichana wengi wanaojikuta wakisuasua katika mitihani ya sekondari huishia kwenye ndoa za mapema na mimba za utotoni—mazingira yanayozima ndoto zao kabla hata hazijachanua. Lakini safari hii, upepo wa mabadiliko umeanza kuvuma. Serikali za majimbo, kwa ushirikiano na Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD), zimeanzisha mpango wa mafunzo ya kita...
Mandale: Kinywaji Cha Asili Kinachowainua Wanawake wa Goma 19.11.2025 10:01
Msikilizaji katika uhalisia mgumu wa maisha ya wakazi wa Goma, hususan baada ya mji huo kuangukia mikononi mwa waasi wa AFC/M23, imeibuka hadithi ya kipekee ya uvumilivu na ubunifu wa wanawake. Kati ya changamoto za ukosefu wa ajira na kuyumba kwa uchumi wa familia, wanawake kwenye mji huo wamegeukia ujuzi wa jadi wa kutengenezaji wa kinywaji cha asili kinachoitwa Mandale.
Similar podcasts
Replaio is not a podcast publisher; show names, artwork and audio belong to their authors and are distributed through public RSS feeds.