RFI Kiswahili
Gurudumu la Uchumi
Fahamu masuala kadha wa kadha kuhusu uchumi kama vile, namna ya kupambana na umaskini, mfumuko wa bei, kushamiri kwa matumizi ya dola na athari za kuyumba kwa uchumi wa dunia kwa nchi za Afrika. Mada hizi zinafanyiwa utafiti wa kina na zinazungumzwa kwa lugha rahisi inayoeleweka ili kukufanya uelewe na usichoke kusikiliza .
Be sure to visit the podcast's website and support the creator: www.rfi.fr
Where to listen?
Podcasts in the app Replaio Radio Coming soonPodcasts are coming to the app soon. Install now and be the first to see a whole new take on podcasts
Episodes
Kutoka Ufugaji wa Mifugo hadi Samaki: Mabadiliko ya Kiuchumi Kajiado 07.01.2026 9:58
Msikilizaji jamii ya Wamaasai kwa muda mrefu imekuwa ikitegemea ufugaji wa mifugo kama chanzo kikuu cha riziki na chakula, hata hivyo, mabadiliko ya tabianchi yaliyoambatana na ukame wa mara kwa mara yamilazimisha jamii hii kutafuta mbinu mbadala za kujipatia kipato, mojawapo ni ufugaji wa samaki.
Sherehe za mwisho wa mwaka zisikuache bila pesa, fahamu mbinu za kudhibiti matumizi yako. 24.12.2025 10:00
Tunapofika mwisho wa mwaka, jamii huingia katika kipindi cha sikukuu kama krismasi na mwaka mpya, ni wakati wa furaha, sherehe na kukutana na familia, lakini pia ni kipindi ambacho matumizi ya fedha huongezeka, watu wengi hujikuta wakitumia zaidi ya uwezo wao na mipango kusimama, tunajadili namna gani unaweza kuwa na nidhamu ya matumizi ya mwisho wa mwaka iwe kwa muajiriwa, mjasiriamali au mfanyab...
Ripoti ya Oxfam-Kenya: Uchumi unakua, lakini Wakenya wengi ni masikini, kwa nini? 03.12.2025 9:58
Msikilizaji juma lililopita shirika la kimataifa la kupambana na umasikini, OXFAM nchini Kenya, ilichapisha ripoti inayoonesha kuongezeka kwa pengo la usawa. Kwa mujibu wa shirika hilo, pengo la walionacho na wasio nacho linaendelea kuongezeka ambapo matajiri 125 wa Kenya kwa sasa wana utajiri wa zaidi ya watu milioni 42 raia wa Kenya. Tunajiuliza, kwa nini ukuaji wa uchumi hauwahusu watu wengi?
Mapinduzi ya Elimu Bondo: Jinsi Teknolojia Inavyowawezesha Wasichana Kuandika Kesho Yao 26.11.2025 10:04
Katika maeneo mengi nchini, hasa magharibi mwa Kenya, wasichana wengi wanaojikuta wakisuasua katika mitihani ya sekondari huishia kwenye ndoa za mapema na mimba za utotoni—mazingira yanayozima ndoto zao kabla hata hazijachanua. Lakini safari hii, upepo wa mabadiliko umeanza kuvuma. Serikali za majimbo, kwa ushirikiano na Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD), zimeanzisha mpango wa mafunzo ya kita...
Mandale: Kinywaji Cha Asili Kinachowainua Wanawake wa Goma 19.11.2025 10:01
Msikilizaji katika uhalisia mgumu wa maisha ya wakazi wa Goma, hususan baada ya mji huo kuangukia mikononi mwa waasi wa AFC/M23, imeibuka hadithi ya kipekee ya uvumilivu na ubunifu wa wanawake. Kati ya changamoto za ukosefu wa ajira na kuyumba kwa uchumi wa familia, wanawake kwenye mji huo wamegeukia ujuzi wa jadi wa kutengenezaji wa kinywaji cha asili kinachoitwa Mandale.
Similar podcasts
Replaio is not a podcast publisher; show names, artwork and audio belong to their authors and are distributed through public RSS feeds.