Kocha Dr Makirita Amani
Dakika 10 Za Kocha
Pata mafunzo mafupi kila siku kutoka kwa Kocha Dr. Makirita Amani, MD, CFE. Mafunzo yamejikita kwenye maeneo makuu matatu; 1. Mafanikio - Kujenga Tabia na Nidhamu ya Mafanikio. 2. Fedha - Kujenga Utajiri na Uhuru wa Kifedha 3. Biashara - Kukuza Mauzo na kujenga Biashara isiyokutegemea. Karibu ujifunze na kuchukua hatua ili uweze kuyabadili maisha yako. Become a supporter of this podcast: https://www.spreaker.com/podcast/dakika-10-za-kocha--1923276/support .
Author
Kocha Dr Makirita Amani
Category
Podcast website
Latest episode
Jul 11, 2026
Where to listen?
Podcasts in the app Replaio Radio Coming soonPodcasts are coming to the app soon. Install now and be the first to see a whole new take on podcasts
Episodes
#DZK039; Poteza Matokeo, Lakini Usipoteze Tabia. 11.07.2026 10:48
Poteza Matokeo, Lakini Usipoteze Tabia. Soma hapa; https://learn.tanzaniteskills.... Rafiki, Safari ya mafanikio ni ligi inayochezwa kwa kipindi chote cha maisha yako. Kwenye ligi yoyote, mafanikio siyo kushinda michezo yote. Kuna michezo ambayo utapoteza. Lakini kama utabaki na tabia na mchakato wako, bado utafanikiwa. Kinachowazuia wengi kufanikiwa ni pale wanaporuhusu matokeo mabaya kubadili ta...
#DZK038; Geuza Udhaifu Wako Kuwa Uimara Wa Mafanikio. 10.07.2026 10:43
Geuza Udhaifu Wako Kuwa Uimara Wa Mafanikio. Soma hapa; https://learn.tanzaniteskills.... Rafiki, Sisi binadamu hatujakamilika. Huwa tuna madhaifu mengi ambayo huwa ni kikwazo kwa mafanikio tunayoyataka. Elimu, mafunzo na ushauri mwingi tunaopata huwa unatutaka tuboreshe madhaifu yetu. Matokeo ya hilo ni tunajikuta tukiwa na madhaifu imara zaidi, na hivyo kujikwamisha zaidi. Kwenye #BaruaYaKocha n...
#DZK037; Jiamulie Mambo Ili Ufanikiwe. 09.07.2026 10:26
Jiamulie Mambo Ili Ufanikiwe. Soma hapa; https://learn.tanzaniteskills.... Rafiki, Unajikwamisha kupata mafanikio makubwa, Kwa sababu ya kusubiri watu wakuamulie au wakuruhusu ufanye unachotaka. Haijawahi kutokea kwa yeyote aliyepata mafanikio makubwa, Kusubiri aruhusiwe na mtu yeyote yule. Mafanikio makubwa yanataka *uwe mtu wa kujiamulia mambo.* Kwenye #BaruaYaKocha nimekuonyesha jinsi ya kujiam...
#DZK036; Akili Tatu Za Kujenga Mafanikio Makubwa. 08.07.2026 10:47
Akili Moja Haikutoshi Kufanikiwa. Soma hapa; https://learn.tanzaniteskills.... Rafiki, Unakazana sana kufanikiwa lakini unakwama. Kwa sababu unatumia akili yako moja tu, ambayo inafikiri. Lakini una akili tatu, moja ni hiyo uliyozoea kutumia. Na nyingine mbili zipo, ambazo zina nguvu kubwa sana. Kwenye #BaruaYaKocha nimekueleza kuhusu akili tatu ulizonazo na jinsi ya kuzitumia zote kufanikiwa. Som...
#DZK035; Ushauri Wa Miaka 218 Unaokufaa Zaidi Leo. 07.07.2026 10:37
Hakuna Kipya Chini Ya Jua. Rafiki, Umekuwa unakazana kutafuta siri za mafanikio kama vile ni kitu kipya. Ambacho unasahau ni kwamba, hakuna kitu kipya kwenye hii dunia. Yote tunayoyaona yamekuwepo miaka kwa miaka. Napoleon, aliyekuwa mtawala wa Ufaransa aliandika barua kwa ndugu yake, aliyekuwa mtawala wa ufalme mwingine. Barua hiyo aliiandika mwaka 1808 na ilieleza vitu vitatu vya mtu kufanya ili...
#DZK034; Epuka Fedha Kuwa Kikwazo Kwako Kufanikiwa. 06.07.2026 10:46
Tamaa Ya Pesa Inakuzuia Kupata Pesa Zaidi. Rafiki, Kama unasoma hapa, Najua unataka kupata pesa zaidi. Lakini kupata pesa inapokuwa ndiyo kipaumbele pekee kwako, Unakuwa unajizuia kupata pesa nyingi zaidi. Na hiyo siyo kwa sababu ya udhaifu wako, Bali ni kwa asili ya binadamu, Ipo kanuni inayosema; *Kipimo kinapogeuka lengo, kinaacha kuwa kipimo kizuri.* Hivyo ndivyo pesa inavyokuwa kikwazo kwako....
#DZK033; Epuka Huu Utani Unaokukwamisha Kufanikiwa. 04.07.2026 10:39
Kataa Kabisa Huu Utani Kwenye Maisha Yako. Rafiki, Kuna vitu huwa tunavichukulia kama utani, Lakini vinakuwa na madhara makubwa kwenye maisha yetu. Moja ya vitu hivyo ni fikra na kauli hasi. Unapojiambia vitu hasi, hata kama ni kwa utani, vinakuathiri. Kwenye #BaruaYaKocha nimekuonyesha jinsi chochote hasi kinavyoweza kukukwamisha. Nimekuonyesha jinsi unavyopaswa kuwa mkali kuondoa kila kilicho ha...
#DZK032; Kuwa Mvumilivu Kwenye Kutokuwa Na Uhakika Ufanikiwe. 03.07.2026 10:25
Kuwa na Uvumilivu Kwenye Kutokuwa na Uhakika. Rafiki, Sisi binadamu huwa tunapenda sana uhakika. Hiyo ndiyo kazi namba moja ya ubongo wetu. Ndiyo maana tunaweza kubaki kwenye mambo yasiyotupa matokeo makubwa, kwa sababu tu yana uhakika. Ili tupate mafanikio makubwa, lazima tuweze kuvumilia hali ya kutokuwa na uhakika. Kwenye #BaruaYaKocha nimekupa mwongozo wa kujenga tabia hiyo. Soma barua hiyo ha...
#DZK031; Jipe Laana Ya Ushindi Ufanikiwe Kwa Uhakika 02.07.2026 10:32
Jipe Laana Ya Ushindi Ili Ufanikiwe. Rafiki, Kuna mambo unayorudia rudia kufanya na yanakukwamisha kupata mafanikio makubwa unayoyataka. Huenda unaamini mambo hayo ndiyo hatima yako. Au umelaaniwa usipate mafanikio unayoyataka. Nina habari njema sana kwako rafiki yangu, Kwamba, unaweza kujipa laana ya ushindi. Ndiyo, unaweza kujipa laana ambayo hata iweje, ni lazima utapata ushindi. Kwa laana hiyo...
#DZK030; Jinsi Ya Kupenda Chochote Ili Ufanikiwe. 01.07.2026 10:36
Kitendawili Cha Mapenzi Na Mafanikio. Rafiki, Kuna kitendawili cha muda mrefu kuhusu mapenzi na mafanikio. Watu wengi wameshindwa kutengua kitendawili hicho na hilo linawakwamisha. Mapenzi na Mafanikio ni vitu ambavyo haviwezi kutenganishwa. Ni lazima mtu apende sana kile anachofanya ndiyo aweze kupata mafanikio. Wengi wanahangaika na vitu wanavyopenda, wakati haviwezi kuwapa mafanikio. Ambacho ha...
#DZK029; Njia Rahisi Ya Kubadili Tabia Ili Ufanikiwe. 30.06.2026 10:17
Njia Rahisi Ya Kubadili Tabia Zako. Rafiki, Moja ya vitu vilivyosimama kati yako na mafanikio yako ni tabia ulizonazo. Huwa tunajenga tabia, halafu baadaye tabia zinatujenga sisi. Ili upate matokeo ya tofauti na unayopata sasa, lazima uwe na tabia tofauti na ulizonazo sasa. Lakini kubadili tabia siyo kitu rahisi. Umejaribu mara nyingi kujenga tabia mpya lakini unakwama. Hiyo ni kwa sababu unatumia...
#DZK028; Mantiki, Ushahidi Na Matumizi - Vigezo Sahihi Vya Mafanikio. 29.06.2026 10:21
Tumia Mantiki, Ushahidi Na Matumizi Kuepuka Usumbufu Rafiki, Naweza kukupa sababu kubwa inayokukwamisha kufanikiwa. Sababu hiyo ni usumbufu. Kuhangaika na mambo mengi ambayo hayana tija kabisa. Unaweza kudhani mambo unayohangaika nayo sasa yana mchango kwako. Lakini siyo. Lipo chujio kali la kujua kipi kina mantiki na kipi hakina. Chujio hilo linaangalia vitu vitatu; 1. Mantiki - Ina maana gani ha...
#DZK027; Jitofautishe Hivi Na Akili Mnemba (AI) 27.06.2026 10:32
Je AI Itakuacha Salama? Rafiki, Teknolojia nyingi zimekuja duniani, Ambazo zimefanya maisha yetu binadamu kuwa bora. Kila teknolojia imekuwa inategemea sana mwongozo wa binadamu ili ifanye kazi. Lakini sasa hivi tuko kwenye mapinduzi ya teknolojia ambayo ni ya tofauti kabisa. Teknolojia hii haitegemei sana mwongozo wa binadamu, bali inaweza kujiongoza yenyewe. Teknolojia hii siyo tena kifaa cha ku...
#DZK026; Epuka Huu Upumbavu Wa Kujitakia Unaokukwamisha Kufanikiwa. 26.06.2026 10:30
#BZK; Epuka Huu Upumbavu Wa Kujitakia Unaokukwamisha Kufanikiwa. Rafiki, Hatua muhimu sana kwenye safari ya mafanikio makubwa ni kuepuka kuwa mpumbavu. Hiyo ni kwa sababu upumbavu ni mzigo ambao ni vigumu sana mtu kuutua. Wakati ujinga inawezekana kuutua kwa kujifunza, upumbavu huwa unamganda mtu kwa muda mrefu. Huwa kuna aina mbili za upumbavu. Ya kwanza ni ule upumbavu wa msingi ambao mtu anakuw...
#DZK025; Usibadilike Kuendana Na Dunia, Ibadili Dunia Iendane Na Wewe. 25.06.2026 10:24
Ibadili Dunia, Iendane na Wewe. Rafiki, Watu wa kawaida huwa wanabadilika kuendana na dunia. Watu wasio wa kawaida huwa wanaibadili dunia kuendana nao. Je unadhani ni kundi lipi linaloleta mafanikio makubwa? Jibu ni kundi la wanaoibadili dunia. Sasa kama unajua hivyo, mbona bado unakazana kubadilika ili uendane na dunia? Kwenye #BaruaYaKocha nimekueleza kwa kina jinsi ya kuibadili dunia iendane na...
#DZK024; Kufanikiwa, Ondoka Ukanda Wa Faraja Kwenda Ukanda Wa Ukuaji. 24.06.2026 10:34
Jenga Ushahidi Sahihi Wa Mafanikio. Rafiki, Mambo mengi tunayofanya ni kwa msukumo wa ushahidi tunaopata. Na kutokana na ushahidi huo, tuna kanda tatu tunazoweza kuwa kifikra. Moja ni ukanda wa faraja (comfort zone) ambapo tunapata ushahidi tuliozoea. Mbili ni ukanda wa ukuaji (growth zone) ambapo tunapata ushahidi chanya. Na tatu ni ukanda wa utisho (panic zone) ambapo tunapata ushahidi hasi. Kwe...
#DZK023; Njia Rahisi Ya Kuwabadilisha Watu Wakubaliane Na Wewe. 23.06.2026 10:33
Wabadilishe watu bila kuwabadilisha. Rafiki, Najua kuna watu wengi sana unaotaka kuwabadilisha ili wawe vile unavyotaka wewe. Labda ni mwenza wako, ambaye ana tabia fulani usizozipenda. Wanaweza kuwa watoto, ambao unataka wajenge tabia sahihi za mafanikio. Au wafanyakazi ambao unataka wajitume zaidi kwenye majukumu yao. Ukijaribu kuwalazimisha watu wabadilike, ndiyo unakuwa umewaambia wasibadilike...
#DZK022; Soma, Andika na Fundisha Ili Ufanikiwe. 22.06.2026 10:46
Soma, Andika, Fundisha. Rafiki, Kuna kanuni rahisi sana ya mafanikio, Ambayo ukiifuata, utaweza kujenga ubobezi na ushawishi mkubwa. Kanuni hiyo ni ya *K Tatu; Kusoma, Kuandika na Kufundisha.* Unatakiwa *KUSOMA* ili kujifunza. *KUANDIKA* ili kuelewa. Na *KUFUNDISHA* ili kubobea. Kwenye #BaruaYaKocha nimekuonyesha jinsi unavyoweza kutumia hayo matatu kufanya makubwa na kufanikiwa. Isome barua hiyo...
#DZK021; Usijenge Msingi Wa Mafanikio Kwenye Mchanga. 20.06.2026 10:42
Acha Kujenga Msingi Wa Mafanikio Kwenye Mchanga Rafiki, Unapambana sana kufanikiwa. Lakini mafanikio yanakuwa magumu kufikia. Na hata ukiyapata, hayadumu. Hilo halisababishwi na mafanikio kushindikana. Bali linasababishwa na msingi unaojenga wa mafanikio. Wengi wanahangaika kujenga msingi wa mafanikio kwenye mchanga. Dhoruba kidogo inapotokea, inasambaratisha kila kitu. Kwenye #BaruaYaKocha nimeku...
#DZK020; Hamasa, Jasho Na Hatari Kwenye Safari Ya Mafanikio Makubwa. 19.06.2026 10:41
Hamasa, Jasho na Hatari Rafiki, Mafanikio makubwa yanaenda kwa kanuni hii; 1. Hamasa - 10% 2. Jasho (Kazi) - 90% 3. Hatari - Mara zote. Watu wengi wanakwama kufanikiwa kwa sababu wanageuza kanuni hiyo. Wanadhani hamasa pekee inawatosha kufanikiwa. Wanakwepa kuweka kazi kubwa inayohitajika. Na wanakwepa hatari. Kama unafanya chochote kati ya hivyo, jua unajikwamisha mwenyewe kufanikiwa. Kwenye #Bar...
#DZK019; Tumaini Unalohitaji Ili Kufanikiwa Kwa Uhakika 18.06.2026 10:07
Ukiwa na Tumaini Hili, Hakuna Kitakachokushinda. Rafiki, Pamoja na wengi kutaka mafanikio makubwa kwenye maisha yao, Ni wachache sana wanaoyapata. Na siyo kwa sababu mafanikio yamewekwa kwa ajili ya wachache. Bali ni kwa sababu wengi wanakosa Tumaini la kuendelea na safari, hasa mambo yanapokuwa magumu. Kwenye #BaruaYaKocha nimekushirikisha Tumaini ambalo ukilijenga, hakipo kinachoweza kukuangusha...
#DZK018; Okoa Muda Na Nguvu, Ufanikiwe. 17.06.2026 10:45
Unapoteza Rasilimali Muhimu Bila Tija. Rafiki, Muda wako na nguvu zako ni rasilimali muhimu sana kwako. Hizo ndiyo rasilimali kuu zinazohitajika kwenye kujenga mafanikio makubwa. Lakini pia ni rasilimali zenye uhaba mkubwa. Una ukomo wa muda na nguvu zako zinaisha kila unapozitumia. Cha kushangaza, licha ya ukomo wa rasilimali hizo, umekuwa unazipoteza bila tija. Umekuwa unafanya mambo yanayotumia...
#DZK017; Raha Rahisi Zinakupoteza 16.06.2026 10:49
RAHA RAHISI, MAFANIKIO MAGUMU. Rafiki, Moja ya vitu vinavyokuzuia kupata mafanikio makubwa ni raha unazopata kwa urahisi. Mambo mengi tunayofanya ni kwa ajili ya kupata raha. Na pale raha inapopatikana kirahisi, kama kupitia ulevi, mitandao na kufanya mapenzi, inazuia kufanya makubwa yanayohitajika kwenye mafanikio. Kwenye #BaruaYaKocha nimekuonyesha jinsi ya kukwepa mtego huo wa Raha Rahisi ili u...
#DZK016; Jiamini Kupitiliza Upate Mafanikio Makubwa 15.06.2026 10:37
MAFANIKIO MAKUBWA HAYATOKANI NA AKILI ZA KAWAIDA. Soma hapa; https://learn.tanzaniteskills.... Rafiki, Umekuwa unayataka mafanikio makubwa, Lakini hujayapata mpaka sasa. Siyo kwa sababu haiwezekani, Bali kwa sababu njia unazotumia siyo sahihi. Njia kuu inayokupotosha ni wewe kutumia akili zako za kawaida. Hizo ndiyo akili zimekufikisha hapo ulipo sasa. Na kamwe, haziwezi kukufikisha zaidi ya hapo...
#DZK015; Fanikiwa Bila Kutegemea 'Koneksheni' 13.06.2026 10:44
Uhakika Wa Mafanikio Kama Unaanzia Chini. Soma hapa; https://learn.tanzaniteskills.... Rafiki yangu mpendwa, Unaanzia chini kabisa, Huna koneksheni, Huna akili nyingi, Huna urithi, Na huna fursa ambazo wengine wanazipata. Je kuna nafasi yoyote kwako kufanikiwa? Jibu ni NDIYO KUBWA. Mafanikio makubwa hayategemei sana unaanzia wapi, Bali yanategemea unaelekea wapi. Kwenye #BaruaYaKocha nimekueleza m...
Similar podcasts
Replaio is not a podcast publisher; show names, artwork and audio belong to their authors and are distributed through public RSS feeds.