Nukta Habari
Nukta the Podcast
Nukta Habari inakusogeza na mambo mtambuka yanayokuhusu ikiwemo burudani, mtindo maisha, safari, teknolojia na biashara.
Обов'язково відвідайте сайт подкасту та підтримайте його автора: nukta.co.tz
Де слухати?
Подкасти в застосунку Replaio Radio Уже незабаромПодкасти незабаром з'являться в застосунку. Встановіть уже зараз і першими побачте зовсім новий погляд на подкасти
Епізоди
UPUNGUFU WA WALIMU SHULE YA MSINGI UNAVYOATHIRI ELIMU TANZANIA 30.09.2023 9:34
Wakati watahiniwa zaidi ya milioni moja wa elimu ya msingi Tanzania Bara wakiwa wanasubiri hatma yao, baada ya kumaliza mitihani yao jana Septemba 14, 2023, utoshelevu wa walimu katika ngazi hiyo muhimu ya elimu kwa shule za Serikali umeendelea kuwa kitendawili Kitabu cha hali ya uchumi cha mwaka 2022, kinabainisha kuwa mpaka Disemba mwaka 2022 kulikuwa na jumla ya wanafunzi milioni 10.8 katika sh...
Elimu ya Veta inavyowainua walemavu wa akili Tanzania 15.09.2023 8:00
Awali, ilikuwa ni vigumu kushuhudia watu wanaozaliwa na ulemavu wakipata huduma muhimu wanazozihitaji kama elimu, afya, pamoja na kushirikiana na wanajamii wengine kuibua suluhu za matatizo yanayozikabili jamii zao. Hivi sasa zama hizo zimepita. Kutokana na hatua zilizochukuliwa na Serikali pamoja na wadau, ikiwemo kuielimisha jamii kutowabagua na kushirikiana na kundi hilo, kama binadamu wengine...
MFAHAMU MBUNIFU WA MAJIKO YANAYOTUMIA MAWE TANZANIA 08.09.2023 7:41
Nishati ya kupikia ni miongoni mwa mahitaji muhimu ya binadamu duniani kote, hiyo ndio huwezesha mapishi ya aina mbalimbali za vyakula tunavyokula ili kuimarisha afya na kuwezesha utendaji wa shughuli za kila siku. Watu wengi wanatambua gesi, mkaa, umeme, mafuta pamoja na kuni kama ndio vyanzo vya nishati ya kupikia kwa kuwa ndio ambavyo vinatumika kwa kiasi kikubwa kwa sasa huku jitihada nyingi z...
JINSI MATAPELI WANAVYOTUMIA TAASISI YA MO FOUNDATION KUIBIA WATU 01.09.2023 7:29
Kama wewe ni mtumiaji wa mtandao wa Facebook huenda umewahi kukutana na chapisho linalohusu fursa ya mikopo kutoka kwenye taasisi ya mfanyabiashara bilionea nchini Tanzania Mohamed Dewji Foundation Sehemu ya chapisho hilo lianasomeka ‘𝐉𝐈𝐏𝐀𝐓𝐈𝐄 𝐌𝐊𝐎𝐏𝐎 𝐊𝐔𝐓𝐎𝐊𝐀 𝐌𝐎𝐇𝐀𝐌𝐄𝐃 𝐃𝐄𝐖𝐉𝐈 𝐅𝐎𝐔𝐍𝐃𝐀𝐓𝐈𝐎𝐍 kwa maelekezo ya kupata vigezo na masharti njoo hwatspp kwa no👉🏿 0748923136’. Chapisho hilo pamoja na kuhamasisha...
KWA NINI BANGI INALIMWA ZAIDI TANZANIA LICHA YA OPARESHENI KALI ZA DAWA ZA KULEVYA? 25.08.2023 9:12
Mapema Agosti mwaka huu Serikali ya Tanzania ilitangaza kukamata magunia 131 ya bangi, kilo 120 za mbegu za bangi na kuteketeza jumla ya hekari 489 za mashamba ya bangi mkoani Morogoro, katika moja ya operesheni kubwa za kutokomeza dawa za kulevya iliyowahi kufanyika nchini. Katika operesheni hiyo Kamishna wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Aretas Lyimo anasema wakulim...
Teknolojia ya vifuu vya nazi itakavyo waokoa wachimbaji na madhara ya zebaki 18.08.2023 7:07
Huenda wachimbaji wadogo wa madini Tanzania wakaepukana na athari za afya pamoja na uchafuzi wa mazingira ikiwa wataasili matumizi ya bidhaa mpya ya kusafishia madini (Activated carbon) inayozalishwa nchini. Bidhaa hiyo inayotengenezwa kwa kutumia vifuu vya nazi itachochea uzalishaji wa madini na kuongeza mchango wa sekta hiyo kwenye pato la taifa kwa kuwa itapatikana kwa urahisi jambo litakaloon...
Hizi ndio hifadhi tano kubwa za Taifa, Tanzania 11.08.2023 7:10
Tanzania ni miongoni mwa mataifa ambayo yamebarikiwa vivutio vingi vya utalii ambavyo sio tu vinapendezesha nchi bali ni chanzo kizuri cha mapato hususani fedha za kigeni ambazo hutumika kwa shughuli za maendeleo. Tovuti ya runinga ya Tanzania Safari Channel ambayo hutangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini, inabainisha kuwa Asilimia 40 ya ardhi ya Tanzania imetengwa kwa ajili ya uhifadhi. Hii...
MVUVI MPAMBANAJI NDANI YA ZIWA VICTORIA 21.03.2023 6:17
Ziwa Victoria ni moja ya maziwa makuu ya Afrika Mashariki. Ni ziwa ambalo lipo kwenye mstari wa ikweta na limezungukwa na nchi tatu zilizopo Afrika Mashariki yaani Tanzania, Kenya na Uganda. Ziwa hili ni chanzo cha Mto Nile wenye urefu wa kilomita 6,650 na urefu huo unaufanya kuwa mto mrefu zaidi duniani, Ziwa Victoria ndiyo ziwa kubwa zaidi barani Afrika na lina ukubwa wa kilomita za mraba 68,800...
ELIMU YA SAIKOLOJIA INAVYOWABEBA WATU WENYE UALBINO TANZANIA 21.03.2023 9:15
Watu wenye ulemavu wa ngozi nchini Tanzania wamekuwa wakikabiliwa na changamoto mbalimbali unyanyapaa ikiwa miongoni, licha ya afua zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali kuelimisha watu wanaowazunguka, baadhi ya walemavu hushindwa kujumuika na wanajamii wengine kutokana na hofu au mitizamo ya kifikra waliyonayo wao wenyewe hata kama jamii ina mtizamo chanya juu yao. Abdushakur Mrisho ametuandalia...
Ifahamu zahanati iliyoanzishwa kwa mkopo wa halmashauri 01.10.2022 8:20
Ni Zahanati ya Afya ya Jamii iliyopo Kata ya Kipunguni jijini Dar es Salaam ambayo ni ya kwanza katika kata hiyo. Vijana nane wametumia mkopo Sh100 milioni wa Halmashauri ya Ilala kuianzisha ili kupunguza changamoto za afya jijini humo. Esau Ng'umbi anasimulia zaidi.
Mradi wa umemejua unavyowafaidisha wanavijiji Tanzania 03.06.2022 7:30
Ni mradi wa jiko linalotumia mionzi ya umemejua kupikia vyakula mbalimbali. jiko hilo la aina yake limebuniwa na Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam ili kupunguza matumizi ya kuni na mkaa.
Wazazi wanavyopambana kuwapatia chakula wanafunzi shuleni Pangani 22.04.2022 6:34
Salaaam msikilizaji wa NUKTA THE PODCAST karibu katika muendelezo wa makala zetu na leo tunasafiri hadi Wilayani pangani mkoani Tanga kumulika namna wazazi wanavyopambana kuwapatia chakula wanafunzi katika shule za sekondari, i mimi ni Suleman Omar Mwiru.
Zaidi ya Watanzania 500,000 kukumbukwa na uhaba wa chakula 25.03.2022 3:29
Wakati baadhi ya Watanzania wakila na kusaza kiasi cha kutupa chakula, ripoti mpya ya usalama wa chakula na lishe Tanzania inakadiria kuwa kuanzia Mei 2022 watu 592,000 watakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula kutokana na kushuka kwa uzalishaji wa mazao ya chakula katika baadhi ya maeneo nchini. Ripoti hiyo ya Tathmini ya Usalama wa Chakula na Lishe iliyotolewa Februari 2022 na Wizara ya Kilimo na...
“Show” ya kibabe iliyowakutanisha mastaa wa Afrika 25.03.2022 5:48
‘Young, Famous & African’ au kwa kifupi unaweza kuita YFA, ni ‘reality show’ yaani imebeba uhalisia wa maisha ya wahusika. Natumaini katika pita pita zako kwenye mitandao ya kijamii, umeshakutana na jina hilo. Wahusika wake ni vijana nyota, maarufu na wenye ‘mishiko’ yao haswaa kutoka nchi mbalimbali Afrika. Ndani humo utakutana na ‘Dj’ maarufu kusini mwa Afrika, hapa namzungumzia Dj Naked, mu...
Jukumu la kutunza mazingira ni la kila mtu 25.03.2022 1:40
Utunzaji wa mazingira yanayotuzunguka ni njia mojawapo ya kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi ikiwemo mafuriko na ongezeko la joto.
Ukame ulivyowarudisha wafugaji kwenye umaskini Tanzania 24.03.2022 6:00
Mwaka 2021 unavyoanza alikuwa ana matumaini lukuki kuwa ng’ombe wake aliokuwa nao wangechangia kwa kiwango kikubwa kumuongezea kipato na kumtoa katika umaskini. Miezi 11 baadaye ndoto ya Ndirana Ndirana Jijungu, mkazi wa Kijiji cha Mwamihanza wilayani Maswa mkoani Simiyu ilizimwa ghafla kwa kupoteza ng’ombe wanne kati ya sita baada ya kukosa malisho kutokana na ukame. Hata hivyo, ukame wa mwishoni...
Mbinu zitakazosaidia kudhibiti taka za baharini 23.03.2022 5:53
Kudhibiti uchafuzi wa bahari Serikali na wadau wanasema taasisi za utafiti na viwanda zinahitaji kufanya kazi kwa ushirikiano ikiwemo kuimarisha mifumo ya ulejerezaji taka. Pia kupiga marufuku kabisa matumizi ya chupa za plastiki na kutoa elimu kwa wananchi juu ya uhifadhi wa mazingira ya bahari kama anavyoripoti Suleman Mwiru.
Gharama kubwa zinavyorudisha nyuma jitihada za kuokoa mazingira Wilaya ya Kibaha 22.03.2022 5:48
Baada ya kubaini faida na urahisi wa kutumia nishati ya gesi kupikia, mwalimu wa moja ya shule za sekondari wilayani Kibaha aliamua kuchukua hatua. Alianza jitihada za kutumia gesi kuongeza ufanisi katika mapishi shuleni kwao na kupunguza kiasi cha kuni zinazotumika kupikia ili kuokoa mazingira. Hata hivyo, changamoto iliyobaki ni gharama kubwa za kupata nishati hiyo. Herimina Mkude anatujuza zaid...
Changamoto zinapokuletea fursa 18.03.2022 7:55
Ni filamu ya "Fine Wine", inayomuhusu mwanadada Kaima anayepitia changamoto katika mahusiano. Licha ya uzuri na ‘usmati’ alionao binti huyu, mahusiano yake na kijana Tunji ni pasua kichwa kuliko hata majukumu yake ya kazi. Maisha ya Kaima yanabadilika siku ambayo wanakubaliana kukutana na Tunji katika mgahawa fulani, lakini kaka huyo anamwambia mpenziwe kuwa amsubiri kwani kuna jambo la ghafla lim...
Taka za kielektroniki zinavyotafuna mazingira ya Tanzania 14.03.2022 4:21
Hakuna mifumo mizuri ya kutupa taka za kielektroniki nchini Tanzania kama ilivyo kwenye nchi zilizoendelea hivyo suluhu kubwa iliyopo ni kuzitupa kama taka nyingine.
The Last Royal Treasure: Filamu ya kuchangamsha wikiendi yako 11.03.2022 6:47
Filamu ya ‘The Last Royal Treasure’, inahusu kundi moja la maharamia au kwa Kiingereza wanafahamika kama pirates. Meli yao imebeba watu ambao wana historia tofauti za kimaisha. Wengine walikuwa majenerali wa vita, watoto wa manahodha, huku wengine wakiwa ni wezi walioshindikana.
Changamoto zinazorudisha nyuma urejelezaji taka Tanzania 10.03.2022 7:02
Ukosefu wa elimu ya udhibiti wa taka hasa plastiki, sera na sheria zinazosimamia mazingira zimetajwa na wadau wa mazingira kuwa zinaweza zikachelewesha safari ya kupunguza uharibifu wa mazingira hasa unaosababishwa na taka za plastiki.
Chupa za plastiki za vinywaji vya kuongeza nguvu zinavyochocheo uharibifu wa mazingira 05.03.2022 7:00
Kuzagaa kwa chupa za plastiki za rangi zinazotumika kuhifadhia vinywaji vya kuongeza nguvu katika mitaa mbalimbali nchini Tanzania hasa jijini Dar es Salaam kumeibua changamoto mpya ya kudhibiti uchafuzi wa mazingira. Licha ya chupa za maji kuokotwa kwa ajili ya kufanyiwa urejelezaji, chupa za rangi zimekuwa zikiachwa zikizagaa mitaani kwa sababu wenye viwanda hawazihitaji katika shughuli zao.&nbs...
Magugu maji yanavyowatesa watumiaji wa Ziwa Victoria 28.02.2022 6:34
Kuendelea kuwepo kwa magugu maji katika Ziwa Victoria kumeibua kadhia mbalimbali kwa watumiaji wa ziwa hilo wakiwemo wavuvi na wamiliki wa boti na meli kwa sababu hutanda katika eneo kubwa na kuzuia shughuli zao. Wanafanya nini kukabiliana nayo? Msikilize mtangazaji Herimina Mkude ambaye anatoa ufafanuzi zaidi.
Simulizi ya Mtaa unaomezwa na maji ya Ziwa Victoria 25.02.2022 6:57
Ni Mtaa wa Ziwa mkoani Mwanza ambao umeharibiwa huku nyumba za wakazi wake zikizama kwenye maji baada ya kina cha maji cha Ziwa Victoria. Kuongeza kwa kina cha maji cha ziwa hilo ni matokeo ya uchafuzi wa mazingira, mafuriko na mvua kubwa iliyonyesha mwaka 2020. Wadau wa mazingira washauri watu kuondoka katika mtaa huo huku wakihimiza watu kuacha kujenga au kufanya shughuli za kilimo na uzal...
Схожі подкасти
Replaio не є видавцем подкастів; назви шоу, обкладинки та аудіо належать їхнім авторам і поширюються через публічні RSS-канали