uk

RFI Kiswahili

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

News SW ↓ Епізодів: 35

Makala yanayochambua masuala na matukio mbalimbali yaliyotokea kwenye jamii kwa wiki nzima kwa kina, yanatoa fursa kwa msikilizaji kueleza hisia na mtazamo wake juu ya masuala yanayoendelea kutokea iwe ni katika uga wa uchumi na siasa duniani kote.

Обов'язково відвідайте сайт подкасту та підтримайте його автора: www.rfi.fr

Автор

RFI Kiswahili

Категорія

News

Сайт подкасту

www.rfi.fr

Останній епізод

3 жов 2026

Де слухати?

Подкасти в застосунку Replaio Radio Уже незабаром

Подкасти незабаром з'являться в застосунку. Встановіть уже зараз і першими побачте зовсім новий погляд на подкасти

Завантажити з Google Play Встановіть безкоштовно Android майже 10 млн завантажень · рейтинг 4,8 iOS незабаром

Епізоди

Uzinduzi wa kiwanda cha mafuta cha Dangote, na kifo cha Chivayo huko Zimbabwe 03.10.2026

Miongoni mwa yaliyojiri wiki hii ni pamoja na uzinduzi wa ujenzi wa kiwanda cha kusafisha mafuta cha Dangote, huko Lamu, pwani ya Kenya, mapigano yaendelea huko Ethiopia, kifo cha bilionea wa Zimbabwe, kutawazwa kwa mfalme wa Tooro, rais wa Nigeria Tinubu, aahidi kupunguza gharama ya maisha na ajira zaidi, rubani amchoma kisu mwenzake ndani ya ndege iliyokuwa ikielekea Israel, na mengineyo

Kiir avunja serikali kuelekea Uchaguzi mkuu wa Sudan Kusini, mapigano mapya yaanza nchini Ethiopia. 27.09.2026

Taarifa kuu utakayoskia kwenye makala haya ni pamoja na Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir avunja serikali kuelekea Uchaguzi mkuu wa mwezi Disemba. Kwingineko nchini Ethiopia, mapigano mapya yameanza tena kati ya vikosi vya Tigray na jeshi la nchi hiyo. Utaskia pia punde zaidi katika mkutano wa UNGA nchini Marekani.

Raia wa Burundi waondoka Kenya, mioto yaangamiza shule, kumbi za Harusi DRC 12.09.2026

Raia wa Burundi walivyokumbwa na masaibu jijini Nairobi, Kenya wengine wakaamua kuondoka, ajali ya mioto iliyotokea nchini DRC, kuanzia Kinshasa wakati wa sherehe ya harusi, kuja Bukavu Kivu kusini ambapo wanafunzi wengi walikufa katika moto ulioshika shule moja, huku ajali ya moto ikiripotiwa mjini Goma, Kivu kaskazini; mazishi ya mfalme wa Tooro huko Uganda kufanyika jumamosi hii, hali nchini Ta...

Wanaharakati Kenya wadai kuachwa huru kwa Lisu na Besigye, Tshisekedi azuru Israeli 05.09.2026

Makala hii imeangazia maandamano ya wanaharakati wa Kenya wakidai kuachwa huru kwa wapinzani Tundu Lisu huko Tanzania, na Kiiza Besigye huko Uganda, wanaokabiliwa na mashitaka ya uhaini, ziara ya rais Felix Tshisekedi huko Israeli, umoja wa mataifa kutaka serikali ya Zambia kuacha kukandamiza wapinzani baada ya uchaguzi, na mvutano kati ya Morocco na Uhispania, mashambulio makali kati ya Marekani...

Kujiuzulu kwa makamu wa rais Tanzania, Tshisekedi azindua mazungumzo ya kitaifa bila M23 29.08.2026

Makala hii imeangazia kujiuzulu kwa makamu wa rais wa Tanzania Emmanuel Nchimbi, huku bunge limemwidhinisha Deogracias Ndejembi kuwa makamu mpya wa rais, na huko DRC rais Felix Tshisekedi amezindua mazungumzo ya kitaifa ambayo yatadumu kwenye majimbo 26 kabla ya kukamilishwa mjini Kinshasa, akiwatenga waasi wa M23, siasa za Kenya, Sudan na wanajihadi wa Nigeria wanavyojikusanyia fedha, pia mzozo w...

Ziara ya rais wa DRC nchini Tanzania, ushindi wa Hakainde Hichilema huko Zambia 22.08.2026

Makala hii imeangazia ziara ya rais wa DRC Félix Tshisekedi nchini Tanzania, mahakama ya Tanzania yasema kiongozi wa chama cha Chadema Tundu Lissu ana kesi ya kujibu ya uhaini, rais Hakainde Hichilema ndiye mshindi wa uchaguzi mkuu wa Zambia wiki iliyopita, utasikia siasa za Nchini Kenya, Sudan na kampeni za uchaguzi mkuu zilianza siku ya jumatano nchini Nigeria, pia tutaenda huko Senegal, na kwen...

Uchaguzi wa nchini Zambia, siasa za DRC, Kenya naTanzania kushika kasi 15.08.2026

Uchaguzi wa urais na wabunge ulivyofanyika nchini Zambia wiki hii, na sasa wananchi wanasubiri matokeo rasmi, baada ya vurugu za siku ya Ijumaa, rais wa Kenya William Ruto aliongoza mazungumzo kuhusu ruwaza ya Kenya 2060, muungano wa upinzani nchini DRC watishia kuitisha maandamano kupinga marekebisho ya katiba; tutaangazia siasa za Tanzania, Sudan, Washington kuiwekea vikwazo Iran kuhusu udhibiti...

Mahakama ya haki yaratibu vikao vya kusikiliza kesi iliyowasilishwa na DRC dhidi ya Rwanda 08.08.2026

Mahakama ya Kimataifa ya Haki wiki hii iliratibu vikao vya kuskiliza kesi iliyowaislishwa na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo dhidi ya Rwanda, ambapo Kinshasa inaituhumu Kigali kwa kukiuka mikataba minne ya kimataifa ikiwemo mkataba wa mauaji ya kimbari, mkataba wa kupinga mateso na mkataba wa kutokomeza aina zote za ubaguzi dhidi ya wanawake.

Kuzirai kwa kiongozi wa upinzani Uganda, mahakama ya katiba nchini DRC yaamua 01.08.2026

Kinara wa upinzani nchini Uganda azirai akiwa mahakamani, mahakama ya katiba nchini DRC ilisema kwamba sheria iliyopendekezwa kuhusu kuandaa kura ya maoni katika nchi hiyo ni ya kikatiba, seneta wa Nairobi Edwin Sifuna autikisa mwamba wa siasa nchini Kenya kuelekea uchaguzi wa 2027, siasa za Tanzania, Sudan, na Morocco ambako wahamiaji waliamua kuogelea kuvuka kwenda ulaya, uhispania, Washington i...

Watu zaidi ya 20 kuuawa mashariki mwa DRC, mchakato wa katiba mpya Tanzania 25.07.2026

Shambulio la ADF laua zaidi ya 20 mashariki mwa DRC, ziara ya waziri mkuu Judith Suminwa huko Ituri, gavana wa zamani wa migori akutwa na hatia ya mauaji, huku rais Ruto akionya kuhusu matumizi ya wahuni kwenye mikutano ya kisiasa, siasa za Tanzania, Sudan na rais wa zamani wa Senegal Macky Sall, kuwasilisha maono yake mbele ya baraza la Umoja wa Mataifa, katibu mkuu wa UN Antonio Guteress atoa wi...

Matokeo ya uchaguzi mdogo Ol Kalou Kenya; rais wa DRC aitisha mazungumzo jumuishi 18.07.2026

Miongoni mwa yaliyojiri wiki hii ni wapiga kura na wanahabari walivyoshambuliwa wakati wa  uchaguzi mdogo Ol Kalau na kuzua hofu kuhusu uchaguzi wa 2027 nchini Kenya: wanafunzi wasiopungua 20 kupoteza maisha katika ajali ya barabarani kule Uganda, shambulio la waasi wa ADF huko Mangina mashariki mwa DRC, usalama kuzorota huko Sudan, ziara ya waziri mkuu wa Ufaransa Sebastien Lecornu kule Morocco,...

Makubaliano kati ya Marekani na Iran kuvunjika, maandamano ya mawakili wa Kenya 11.07.2026

Yaliyojiri wiki hii ni kuvunjika kwa makubaliano kati ya Marekani na Iran, mazishi ya kiongozi wa kiroho wa Iran A.Khamenei, rais wa Tanzania Samia Suluhu kuwaonya wanaharakati dhidi ya kuchochea vurugu-wanasiasa wa upinzani, wanahabari pamoja na wanaharakati, Uganda waishi kwa hofu kutokana na vitisho vya mkuu wa majeshi, wapinzani wa jukwaa la C64 DRC walikutana na rais wa Burundi Evariste Ndayi...

DRC yasherehekea miaka 66 ya uhuru, amnesty yalaani vita Sudan, mazishi ya Khamenei huko Iran 04.07.2026

Makala imeangazia maadhimisho ya miaka 66 ya uhuru wa jamahuri ya kidemokrasia ya Congo, kuanzishwa kwa majaribio ya dawa zizonaweza kuwa tiba ya Ebola aina ya Bundibugyo huko DRC, kufungwa kwa kituo cha televisheni cha NTV na Gazeti la Daily Moniter nchini Uganda, shirika la Amnesty International, layatuhumu mataifa ya nje  kwa kuendelea kuchochea mzozo wa Sudan. Polisi nchini Afrika Kusini wazui...

Maandamano ya Gen Z Kenya, ziara ya rais Ndayishimiye DRC,vifo Venezuela vyafikia920 27.06.2026

Maandamno ya vijana wa Gen Z kuwakumbuka wenzao waliouawa katika maandamano ya mwaka wa 2024 nchini Kenya, kesi ya aliyekuwa meya wa jiji la Kampala Uganda Erias Lukwago, ziara ya rais wa Burundi pia mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, jijini Kinshasa DRC, Evariste Ndayishimiye, yaliyojiri huko Sudan, Nigeria, Tunisia lakini pia mitetemeko miwili ya ardhi huko Venezuela iliyouwa watu zaidi ya 900, na p...

DRC na kombe la dunia, pia ebola,Gen z kuandamana juni 25 Kenya,hali ya sasa Iran 20.06.2026

Ni wiki ambayo imegubikwa na michuano ya kombe la dunia 2026 huko Marekani, wiki hii eneo hili la Afrika mashariki na kati lilichangamka baada ya timu ya DRC Leopards kutoka sare na Ureno, virusi vya ebola na juhudi za kikanda kuudhibiti, kukamatwa kwa wakili Erias Lukwago kule Kampala Uganda, lakini pia mashambulio ya kigaidi kwenye uwanja wa ndege wa mjini Niamey huko Niger, na mkutano wa G7 jij...

Michuano ya kombe la dunia, hali ya Ebola kwenye ukanda 13.06.2026

Ni wiki ambayo imegubikwa na maandamano kadhaa nchini huko Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, huko Nanyuki nchini Kenya, na watu kutoka nchi kadhaa za Afrika kuihama Afrika Kusini kutokana na ongezeko la chuki dhidi ya wageni, lakini kubwa kabisa wiki hii lililotikisa ulimwengu ni michuano ya kombe la dunia ya mwaka wa 2026 iliyong’oa nanga huko Marekani, Mexico na Canada, bila kuisahau ziara ya Ki...

Ufaransa yazindua mnara wa kumbukumbu ya genocide Rwanda, mgomo wa kitaifa DRC 06.06.2026

Ufaransa yazindua mnara wa ukumbusho wa mauaji ya kimbari huko Rwanda kwenye jiji la Paris, wapinzani wa DRC juni 03 waliitisha mgomo wa kitaifa, watu zaidi ya kumi waliuawa katika shambulio lililotekelezwa na waasi wa ADF huko Mbau wilaya ya Beni mashariki mwa DRC tunaangazia hotuba ya rais wa Uganda kwa taifa, ziara ya rais wa Tanzania huko Urusi, Afrika kusini kudai kuwa hakuna ubaguzi wala chu...

Wanafunzi 16 wafa katika moto wa shule ya bweni Kenya, mkuu wa WHO azuru DRC 30.05.2026

Wanafunzi kadhaa kupoteza maisha na wengine kujeruhiwa katika shule ya Sekondari ya wasichana Nakuru nchini Kenya, ziara ya mkurugenzi mkuu wa shirika la afya duniani WHO, Uganda kutangaza kuufunga mpaka wake na DRC, hali nchini Sudan, huku Nigeria, kuelekea uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika mwezi Januari mwaka ujao, na pia ripoti zinasema Marekani na Iran zakubaliana kuongeza usitishwaji wa vita...

DRC yashirikiana na WHO, AU kupambana na Ebola, sitisho la mgomo wa madereva Kenya 23.05.2026

Habari kuu za dunia wiki hii ni pamoja na kuzuka kwa mlipuko wa ugonjwa hatari wa ebola, DRC na juhudi za kimataifa zinazolenga kupambana na virusi hivyo, mkutano wa Kigali kuhusu nyuklia, mgomo wa madereva wa usafiri wa umma ulivyoathiri wananchi, Kenya, hali nchini Sudan ; lakini pia wahamiaji wasio na vibali wanavyohangaishwa kule Afrika kusini, ziara ya rais wa Urusi kule China ; lakini pia Ma...

Yoweri Museveni aapishwa muhula wa saba Uganda, kongamano la Afrika forward Nairobi 16.05.2026

Miongoni mwa habari kuu za dunia zilizopewa uzito juma hili ni pamoja na kuapishwa kwa rais wa Uganda Yoweri Museveni kwa muhula wa saba, kufanyika na kutamatika kwa mkutano wa Afrika na Ufaransa jijini Nairobi nchini Kenya, kauli ya rais wa Rwanda Paul Kagame akikosoa vikwazo vya Marekani kuhusu nchi yake, eneo la Afrika magharibi hususan Nigeria, Ghana na Mali, lakini pia Ziara ya rais wa Mareka...

Watu 518 walifariki Tanzania wakati wa vurugu za uchaguzi, mapigano bado yanaendelea DRC 25.04.2026

Taarifa kuu wiki hii ni ripoti ya tume ya uchunguzi nchini Tanzania iliyosema watu 518 walifariki wakati wa ghasia za uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba mwaka uliopita.  Tunaangazia pia taarifa kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambapo licha makubaliano ya kusitisha vita kati ya waasi wa M23/AFC na serikali ya Kinshasa, kuendelea kushuhudiwa kwa mapigano ya mara kwa mara. Kiongozi wa kanisa katoli...

Kifo tatanishi cha waziri wa habari wa Burundi, Iran na Marekani zatunishiana misuli 18.04.2026

Makala hii imeangazia kifo cha waziri wa mawasiliano na vyombo vya habari nchini Burundi Gabby Bugaga, waasi wa AFC/M23 na serikali ya DRC wanaokutana huko Uswis wakubaliana kuhusu kubadilishana na wafungwa, huku Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo ikisisitizia msimamo wake wa kuitaka Rwanda kuwaondoa wanajeshi wake katika eneo la mashariki, ziara ya kiongozi wa kanisa katoliki nchini Cameroon kabla...

Rwanda yaadhimisha miaka 32, mauaji ya kimbari, Israeli yashambulia Lebanon 11.04.2026

Maadhimisho ya siku 100 maarufu kama kwibuka kukumbuka mauaji ya mwaka 1994 nchini Rwanda, mwanadiplomasia wa Marekani James Swan kuanza kazi kama mkuu wa Monusco huko DRC, mazungumzo kati ya serikali ya nchi hiyo na waasi wa M23 kufanyika kule Geneva Uswiz chini ya upatanishi wa Qatar, hali ya kisiasa nchini Kenya na Tanzania, na sudan; kampeni za uchaguzi mkuu nchini Benin kutamatishwa kuelekea...

Waasi wa ADF waua 40 mashariki mwa DRC, Iran yapuuzi vitisho vya Trump 04.04.2026

Miongoni mwa matukio makubwa yaliyojiri wiki hii ni pamoja na timu ya taifa ya soka ya DRC Leopards kufuzu kushiriki fainali ya michuano ya kombe la dunia 2026, shambulio la waasi wa ADF laua 30 mashariki mwa DRC, watoto wanne wadungwa kisu hadi kufa katika shule moja nchini Uganda, wapigakura wahamasishwa kujiandikisha nchini Kenya na kupanda kwa bei ya mafuta, kuapishwa kwa rais wa Jamhuri ya af...

UN yasikitishwa na hali mashariki mwa DRC, miili 33 yagunduliwa nchini Kenya 28.03.2026

Miongoni mwa yaliyojiri wiki hii ni pamoja na baraza la usalama la umoja wa mataifa lataka kufunguliwa upya kwa viwanja vya ndege kwenye miji ya Goma na Bukavu mashariki mwa DRC, kiongozi wa upinzani nchini Uganda Bobi Wine alisema uhuru wake sio mjadala, miili 14 ilipatikana iliyopatikana nchini Kenya kufanyiwa upasuaji kubaini chanzo cha vifo. utambuzi wa utumwa kuwa uhalifu dhidi ya haki za ubi...

Слухайте подкаст Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii у Replaio

Радіо та подкасти в одному застосунку - безкоштовно й без реєстрації. Встановіть уже сьогодні та не пропустіть запуск

Завантажити з Google Play

Replaio не є видавцем подкастів; назви шоу, обкладинки та аудіо належать їхнім авторам і поширюються через публічні RSS-канали