RFI Kiswahili
Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho
Ni Makala yanayoangazia kwa jicho la tatu mazingira halisi ya dunia yalivyo bila kusahau kile ambacho kinachangia kuyaharibu. Utapata kufahamu namna ambavyo mazingira na rasilimali zinavyoharibiwa huku pia teknolojia ikijumuishwa. Hakika mazingira mazuri ya leo ni dunia yako kesho.
Vizitează neapărat site-ul podcastului și susține-i creatorul: www.rfi.fr
Autor
RFI Kiswahili
Categorie
Site-ul podcastului
Cel mai nou episod
26 oct. 2026
Unde asculți?
Podcasturi în aplicație Replaio Radio În curândPodcasturile ajung în curând în aplicație. Instaleaz-o acum și fii primul care descoperă o abordare complet nouă a podcasturilor
Episoade
Awamu ya pili: Kongamano la masoko ya kaboni barani Afrika, Kigali 26.10.2026 10:07
Pamoja na Bwana Zephaniah Kivungi, mkurugenzi wa tabianchi katika shirika la CIFF, tunaendelea na awamu ya pili ambapo nilikuahidi kuangazia ni kwa namna gani tunaweza kuhakikisha kuwa biashara ya kaboni zinawakilisha upunguzaji halisi wa gesi chafuzi.
Afrika: Nini nafasi ya masoko ya kaboni katika mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabianchi 23.10.2026 10:02
Masoko ya kaboni, yapo kwa ajili ya kuwawajibisha watu na mashirika ambayo shughuli zao zinachangia katika uchafuzi wa hewa, ambapo wanahitajika kugharamia juhudi zinazofanywa na watu mbalimbali au jamii katika kupunguza hewa ya kaboni kwenye anga, kwa mfano upandani wa miti. Nimemwalika, Zephaniah Kivungi, mkurugenzi wa tabianchi katika shirika la CIFF, ambaye atatusaidia kuelewa zaidi suala hili...
Kenya: Sahihi elfu sitini za kuitaka serikali kusitisha ukataji wa miti kwenye misituya umma 12.10.2026 9:51
Madai ya mengine kuitaka serikali kusitisha mipango yoyote ya kutenga maeneo ya misitu kwa ajili ya matumizi mengine, kama vile ujenzi wa Barabara, kudumisha marufuku ya ukataji miti ili kulinda misitu iliosalia nchini Kenya, Chukua hatua za haraka na thabiti dhidi ya shughuli za ukataji miti kinyume cha sheria na uporaji wa ardhi ndani ya maeneo ya misitu
Wanaharakati wa mazingira walalamikia athari za kiwanda cha kusafisha mafuta cha Dangote Lamu 05.10.2026 10:04
Licha ya faida za kiuchumi, mashirika ya mazingira na wanaharakati wa mazingira wanasema kiwanda hicho ni tishio kwa mifumo ikolojia ya eneo la Pwani pamoja na riziki ya jamii katika eneo hilo. Pamoja na Omar Elmawi, wakili wa mazingira na nishati kutoka Mombasa, tunajadili mradi huu wa Dangote ambao ujenzi wake unatarajiwa kukamilika katika kipindi cha miezi 40 ijayo.
Je unafahamu umuhimu wa kuzuia upotevu na uharibifu wa chakula? 28.09.2026 10:05
Mwaka huu ni maadhimisho ya saba ya siku ya kimataifa ya kutoa hamasisho kuhusu utupaji na upotevu wa chakula, ambao unachangia kati ya asilimia 8–10 ya utoaji wa gesi joto Lengo la maendeleo endelevu nambari 12.3 linalenga kuona dunia ikipunguza upot’evu na uharibufuwa chakula kwa nusu ifikapo mwaka 2030.
Septemba 22, siku ya kimataifa ya kutotumia magari mijini 23.09.2026 10:03
Wananchi katika miji mbalimbali ya dunia wanahimizwa kuacha magari yao binafsi nyumbani na kukumbatia mbinu zingine za usafiri zilizo endelevu kama kutumia baiskeli au kutembea kwa miguu. Makala haya yanaangazia namna baiskeli za umeme zinaweza kuwa moja ya suluhu ya uchafuzi wa hewa kwenye miji unaotokana na sekta ya usafiri.
Kenya: Wanaharakati watoa mapendekezo mapya dhidi ya plastiki zinazochafua mazingira 14.09.2026 9:57
Kenya inakabiliwa na changamoto ya plastiki zinazotumiwa mara moja tu kama vile mifuko inayotumiwa sokoni kupakia mboga ambazo huchangia katika uchafuzi wa mazingira licha ya kupigwa marufuku. Ni Kutokana na hili ambapo wanaharakati wa mazingira wamekuja na mapendekezo mapya ya kukabiliana na tatizo hili, mbali na suluhu la uchakataji. Moja ya matokeo ya mapendekezo haya ni kuiweka Kenya katika na...
Kenya: Nyenzo(Tool) mpya inavyoanika matumizi ya ufadhili wa tabianchi Kenya 26.08.2026 10:00
Matumizi ya ufadhili wa hali ya hewa imekuwa swala kuu kwa wadau wa mazingira, kutokana na mianya ya ufuatiliaji. Nchini Kenya, shirika la Transparency International , sasa linajaribu kuziba mwanya uliopo ambapowakenya watakuwa wakifuatilia miradi na matumizi ya fedha hizi nchini humo kupitia jukwaa jipya la mtandaoni la Climate Finance Watch Tool.
Kenya: Ubunifu wa unaogeuza magugu maji kuwa mifuko ya kupakia bidhaa na matumizi mengine 24.08.2026 9:59
Kwa wavuvi katika ziwa Niavasha, kama vile Simon Macharia na Joseph Kimani, Magugu maji yamekuwa kero kwa muda mrefu, na wakati mwingine kuwasababishia hasara. Lakini sasa kutokana na ubunifu wa Joseph Nguthiri , kijana bingwa wa dunia wa Mazingira wa UNEP mwaka wa 2025, na mwanzilishi wa kampuni ya Hyapak wavuvi wanaweza kujipatia kipato zaidi.
Kenya: Familia hatarini kutokana na kupanda kwa kiwango cha maji ziwa Naivasha 10.08.2026 9:55
Familia katika kijiji cha Kihoto mjini Naivasha, zimeendelea kutaabika kutokana na athari za kupanda kwa kiwango cha maji kwenye ziwa Naivasha, na kusababisha maji kuingia kwenye kijiji ambayo pia yamesababisha kuenea kwa magugumaji. Nikurejesha nchini kenya, katika eneo la bonde la ufa, ziwa Bogoria, ziwa Baringo na Ziwa Niavasha, ni mfano wa maziwa ambayo yameendelea kushuhudia kupanda kwa kina...
El Niño: Wataalam waonya kuhusu mvua kubwa, mafuriko na joto la kali 03.08.2026 9:57
Hali ya hewa ya El Niño inaendelea kuimarika kwa kasi na inatarajiwa kutawala katika kipindi cha kuanzia mwezi Agosti hadi Oktoba mwaka wa 2026, hali itakayoongeza uwezekano wa viwango vya joto kuzidi wastani katika maeneo mengi ya dunia na kusababisha mabadiliko makubwa katika mifumo ya mvua. Mashirika ya hali ya hewa likiwemo lile la dunia WMO na KMD nchini Kenya, yameongeza utaratibu, huduma za...
Fahamu kuhusu chanzo cha wimbi la joto kali linaloshuhudiwa Ulaya. 28.07.2026 9:58
Wimbi la joto kali limekumba bara la Ulaya kwa muda sasa, hali iliyosababisha viwango vya juu vya joto katika nchi kadhaa na kusababisha maelfu ya vifo. Zaidi ya watu 300,000 wamehamishwa na angalau mtu mmoja alifariki dunia kutokana na moto wa nyika nchini Ufaransa na Uhispania, huku vikosi vya zimamoto vikipambana na mioto hiyo. Leo katika uchambuzi wetu tunaungana na Daktari Joyce Kimutai, mwan...
Juhudi za akina mama kuhifadhi fukwe za bahari pwani ya Kenya 21.07.2026 10:04
Wakati mataifa mbalimbali duniani yakiongeza juhudi za kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi na uchafuzi wa bahari, nchini Kenya akina mama wamejitokeza mstari wa mbele kulinda mazingira. Katika Kaunti ya Mombasa, wameanzisha kampeni ya kupanda miti ya asili na kurejesha uoto uliopotea kwenye maeneo ya pwani. .Hii leo katika makala mazingira leo dunia yako kesho ,tunaangazia juhudi za a...
Utengenezaji wa mkaa kutoka kwa mmea wa mianzi 06.07.2026 9:49
Misitu ni sehemu muhimu katika mapambano ya dunia dhidi ya mabadiliko ya tabianchi, hata hivyo misitu mingi ipo hatarini kutokan ana shughuli za binadamu. Fahamu kuhu mkaa unaotengenezwa kutokana na mmea wa mianzi(Bamboo)
Mkutano wa Innovate4cities: Kuharakisha hatua za kukabili mabadiliko ya tabianchi kwenye miji duniani. 29.06.2026 10:01
Mkutano huo ulioandaliwa na Global Covenant of Mayors for Climate and Energy (GCoM kwa ushirikiano na UN-Habitat, ulijadili mada tofauti kama vile sayansi ya tabianchi, sera na namna ya kuangazia mianya iliopo katika elimu, data, ufadhili na utakelezaji zinazolemaza mikakati ya kukabili tabainchi kwenye miji. Katika makala yetu hivi leo, nimezungumza na Bi Maryam Wangeshi , ni msanifu wa majengo l...
Mjadala waibuka kuhusu jinamizi la taka za nguo kwa mazingira 15.06.2026 9:58
Kila wiki, mamilioni ya nguo za mitumba hufika katika masoko kama vile Gikomba jijini Nairobi, Kenya, au Kantamanto mjini Accra, Ghana. Takriban asilimia 40 ya bidhaa hizi zinazoagizwa kutoka nje haziwezi kuvaliwa kabisa, na hivyo kuhamishia mzigo wa udhibiti wa taka za nguo kwa jamii. Nguo nyingi zilitotengenezwa kwa kutumia poliesta na nailoni, huziba njia za maji za mijini, huchafua fuo za baha...
Usimamizi endelevu wa taka kwenye mazingira hauwezi kufanikiwa bila mchango wa wakusanyaji taka 15.06.2026 10:04
Tunawaangazia wadau muhimu katika sekta ya usimamizi wa takan hapa tunazungumzia wakusanyaji taka, ambao mara nyingi mchango wao hupuuzwa nasa katika meza ya maamuzi kuhusu suala hili la cuhafuzi wa taka.
Kuna haja ya serikali za Afrika kukumbatia mfumo endelevu ya kukabili taka ngumu kwenye mazingira. 01.06.2026 10:06
Tatizo la uchafuzi wa mazingira kutokana na taka ngumu, bado ni changamoto katika miji mingi barani Afrika. Hata hivyo, hivi karibuni, kumekuwa na jitihada kwenye baadhi ya mataifa ambapo sasa nchi zimeanza kuwa na sheria na kanuni za kuhakkisha usimamizi endelevu wa taka, kwa kuwahusisha wazalishaji na waagizaji wa bidhaa.
Kongamano la siku mbili jijini Nairobi latoa wito wa kubadili simulizi kuhusu maeneo ya nyanda za malisho(Rangelands) 25.05.2026 10:09
Kwa muda mrefu maeneo ya nyanda za malisho yamekuwa yakitazamwa kama yaliotengwa na yasio na umuhimu, licha ya kuwa na mifumoikolojia muhimu na chanzo cha riziki kwa takriban watu bilioni mbili duniani, Pamoja na kuhifadhi theluthi moja ya hewa ya kaboni duniani. Lakini sasa wadau wa mazingira, watunga sera, watafiti, wataalam na wawakilishi kutoka jamii za wafugaji baranai Afrika sasa wanatoa wit...
Juhudi za kijamii zilivyookoa msitu wa Karura uliokua umegeuka kuwa eneo la uhalifu 21.05.2026 19:56
Nairobi ni mwenyeji wa msitu mkubwa wa mvua ulio salama ndani ya mipaka yake: Hifadhi ya Karura yenye ukubwa wa hekari 1,000 ni mapafu muhimu ya mji mkuu wa Kenya, katika kuchuja uchafuzi wa mazingira kwa mamilioni. Ilikuwa ishara ya ukosefu wa usalama, sasa ni mfano mkuu wa kimataifa wa uhifadhi unaoongozwa na jamii haswa shirika la marafiki wa Karura maarufu Friends of Karura. Hata hivyo, msitu...
Nchini Colombia, mkutano wa kwanza wa kimataifa kuhusu mafuta ya visukuku 12.05.2026 9:09
Msikilizaji, juma moja lililopita, mawaziri kutoka karibu mataifa 50 duniani walikutana nchini Colombia kwa mkutano wa mazingira uliolenga kujadili mbinu za mataifa kuachana kikamilifu na nishati zinachafua mazingira ikiwemo gesi na mafuta. Mjadala kuhusu mataifa kuachana na matumizi ya nishati chafu zinazochangia ongezeko la joto duniani, umekuwepo katika mikutano tofauti ya kimataifa ya mazingir...
Jamii katika maeneo kame nchini kenya zawezeshwa ili kustahimili athari za mabadiliko ya tabianchi. 27.04.2026 9:32
Nchini Kenya, mzozo wa rasilimali katika jamii zinazopatikana katika maeneo kame ni changamoto ya muda mrefu, na kumekuwa na jitihada ya mashirika tofauti kuziwezesha jamii hizo kustahimili changamoto zitokanazo na athari za mabadiliko ya tabianchi. Kupitia mradi wa IMARA, jamii ya wafugaji sasa wamegeukia ukulima wa aina tofauti ambao baadhi yao unawadsaidia hata kupata chakula ya mifugo wao.
Sera za Mipango miji barani Afrika zinazingatia ustahimilivu wa majanga mijini? 20.04.2026 10:02
Mkutano wa pili wa Umoja wa Afrika unaofahamika kama 'Jukwaa la Mijini Afrika (AUF) ulianzishwa kwa nia ya kuwezesha mazungumzo na uratibu wa ukuaji endelevu wa miji na makazi ya watu barani Afrika. Pamoja na Maryam Wangeshi , msanifu wa majengo, tunaangazia matokeo ya mkutano huo na ikiwa mataifa ya Afrika yana mipangilio ilio bora katika kuwezesha miji yetu kustahimili majanga ya kimazingira.
Ukulima wa mianzi katika kutunza mazingira ya mito nchini Kenya. 10.04.2026 9:57
Mimea ya mianzi yaani Bamboo ni mojawapo ya mimea kote ulimwenguni inayoweza kupandwa katika mazingira tofauti kama vile sehemu tambarare au chemichemi. Ukulima wa mianzi unaboresha mazingira kwa kuzuia mmomonyoko wa udongo, kurejesha rotuba kwa udongo haswaa sehemu zilizo karibu na mito na hata kama kitega uchumi.
Replaio nu este editorul podcasturilor; numele emisiunilor, coperțile și materialul audio aparțin autorilor lor și sunt distribuite prin fluxuri RSS publice