Michael Kamukulu
LENZI Podcast with Michael Kamukulu
Jifunze kupitia mijadala na maelezo yanayohusu mada mbalimbali ili upate ufahamu juu mienendo ya sasa katika nyanja na tasnia tofauti. Pata uchambuzi wa takwimu rasmi katika kuleta uhalisia wa mada tunazozijadili. Uwe ni mmiliki wa biashara unayetaka kuboresha biashara yako ama kufungua mradi mpya, au mtu binafsi unayetaka kuongeza ufanisi wako, podcast yetu ina kitu kwa ajili yako. SIKILIZA ILI UWEZE KUJIFUNZA
Vizitează neapărat site-ul podcastului și susține-i creatorul: podcasters.spotify.com
Autor
Michael Kamukulu
Categorie
Site-ul podcastului
Cel mai nou episod
4 nov. 2023
Unde asculți?
Podcasturi în aplicație Replaio Radio În curândPodcasturile ajung în curând în aplicație. Instaleaz-o acum și fii primul care descoperă o abordare complet nouă a podcasturilor
Episoade
S1E22 Unatumia Siku 28 kwenye Social Media kwa Mwaka: Ijue Gharama Halisi | LENZI | Michael Kamukulu 04.11.2023 4:06
Ijue gharama halishi ya muda ambao unautumia kwenye social media (mitandao ya kijamii). Kwa wastani mtumiaji wa kawaida wa internet anatumia saa 2.5 mpaka 3 kwenye mitandao ya kijamii kwa siku. Mtanzania wa kawaida anatumia wastani wa saa 2.5 kwa siku ambayo ni sawa na siku 28 za kazi kwenye social media kwa mwaka. Huu ni muda mwingi ambao usipotumika vizuri unasababisha hasara kifedha na kiafya p...
S1E21 Digital Detox: Jinsi nilivyojiondoa kwenye addiction ya SIMU na Mitandao | Michael Kamukulu LENZI 28.10.2023 10:32
DIGITAL DETOX Watumiaji wengi hawazifahamu athari zinazotokana na matumizi makubwa ya mitandao ya kijamii, simu, TV pamoja na aina nyingine ya vifaa vinavyotumia screen. Athari hizi zina madhara makubwa sana ikiwemno kusababisha changamoto za afya ya akili. Athari nyingine ni kama matumizi mabaya ya muda, kupunguza ufanisi kwenye uzalishaji, kuvunjika kwa mahusiano pamoja na madhara mengine mengi....
S1E20 Matumizi ya SIMU: Fahamu athari za matumizi yaliyopitiliza ya simu | LENZI | Michael Kamukulu 21.10.2023 7:48
Watumiaji wengi hawazifahamu athari zinazotokana na matumizi makubwa ya mitandao ya kijamii, simu, TV pamoja na aina nyingine ya vifaa vinavyotumia screen. Athari hizi zina madhara makubwa sana ikiwemno kusababisha changamoto za afya ya akili. Athari nyingine ni kama matumizi mabaya ya muda, kupunguza ufanisi kwenye uzalishaji, kuvunjika kwa mahusiano pamoja na madhara mengine mengi. Mawasiliano n...
S1E19 Mjasiriamali: YAJUE MAENEO MANNE (4) YA UWEKEZAJI USIOKUWA WA KIBIASHARA | LENZI | Michael Kamukulu 14.10.2023 5:59
Mafanikio hayatokei kwa bahati, wanaofanikiwa wote wanajuia na kuifuata misingi inayowapelekea mafanikio kwa kuwekeza kwenye maeneo yanayoongeza thamani yao kwenye maisha. Siri ya mjasiriamala au mfanyakazi mwenye mafanikio iko kwenye uwezo wake wa kuongeza thamani yake katika biashara au kazi anayoifanya. Thamani huongezeka kwa kuzingatia misingi mkuu ya fedha, maisha na mafanikio. Unaweza kutumi...
S1E18 MTUMIAJI WA SIMU: Fahamu njia tano (5) za kuongeza usalama wako mtandaoni | LENZI | Michael Kamukulu 07.10.2023 6:45
Katika zama hizi za kidijitali tulizonazo, kulinda usalama wa taarifa zako kwenye mitandao ni muhimu kuliko ilivyokuwa hapo awali. Jiunge nasi katika video hii tunapoongelea njia tano (5) muhimu za kuimarisha usalama wako mtandaoni. Jifunze jinsi ya kulinda namba yako ya simu, kuweka kinga imara kwenye akaunti zako za baruapepe, kuhifadhi alama za vidole vyako, kujilinda dhidi ya tishio la "d...
S1E17 Jinsi ya Kufanya Manunuzi Salama Mtandaoni: Mambo Matano (5) ya Muhimu | LENZI | Michael Kamukulu 30.09.2023 5:02
Watu walio wengi hawajui jinsi ya kununua bidhaa kwa njia salama kwenye mtandao kama vile Alibaba, Amazon, Kikuu, Ali Express na mitandao mingine ya aina hii. Kabla ya kuagiza bidhaa kwenye mtandao au simu, ni muhimu kuhakikisha kwamba pesa yako iko salama na unanunua kwa wauzaji wanaoaminika. Unaweza kutumia njia kama vile M Pesa, Tigo Pesa, Airtel Money au nyingine kama vile Sim Banking. Na unaw...
S1E16 Harufu Ya Chakula Haitibu Njaa: Furaha inayotegemea kuwaridhisha watu wengine bila faida binafsi, ni UTUMWA 23.09.2023 3:14
Njaa hutibiwa na chakula, wala harufu nzuri na hata sio lazima chakula kiwe kitamu sana. Haijalishi kama kinaliwa jioni, mchana, asubuhi wala usiku. Harufu ni hisia inayokuvutia kuelekea kwenye chakula, lakini usipokula hicho chakula, njaa haitaondoka. Hii inatokea sana kwenye maisha yetu ya kila siku katika kutafuta mafanikio ya career, mahusiano, nk. Tunahitaji maarifa sahihi ili kufanya maamuzi...
S1E15 Ishara 5 kwamba unapoteza kuliko unavyopata (unapoteza MUDA, THAMANI, FEDHA kwenye kazi na biashara) 16.09.2023 8:51
Kama hasara ama gharama ya kupata jambo lolote inakuwa kubwa kuliko faida zinazotokana na jambo hilo, basi hatuna budi kuachana na jambo husika na kutafuta mbadala unataofaa na kutupa manufaa tunayoyahitaji. Kama gharama za matumizi zinazidi kiwango cha mshahara ama faida ya biashara, ni wakati wa kubadilisha kazi au biashara hiyo. Mara nyingine inakuwa vigumu kufahamu kwamba tayari uko kwenye hal...
S1E14 Fahamu sababu za kuichoka kazi yako (Mambo Matatu [3] ya kuzingatia) | LENZI | Michael Kamukulu 09.09.2023 10:09
Wengi wetu tunaamini kwamba biashara ya bodaboda inawanufaisha zaidi waendesha pikipiki na bajaji lakini ukweli unaweza ukawa tofauti. Waendeshaji wengi wa vyombo hivi vya moto sio wamiliki wa biashara, wao ni watoa huduma. Mtazamo wao kwenye biashara hii unawafanya wasiwe wamiliki wa kazi yao wenyewe. Wanaweka mkazo zaidi kwenye kurejesho hesabu ya mabosi wao kuliko kuisimimaia biashara kwa ajili...
S1E13 Ni Nani Anashikilia Uchumi, Soko na Umiliki wa Biashara ya Bodaboda?? | LENZI | Michael Kamukulu 02.09.2023 9:40
Wengi wetu tunaamini kwamba biashara ya bodaboda inawanufaisha zaidi waendesha pikipiki na bajaji lakini ukweli unaweza ukawa tofauti. Waendeshaji wengi wa vyombo hivi vya moto sio wamiliki wa biashara, wao ni watoa huduma. Mtazamo wao kwenye biashara hii unawafanya wasiwe wamiliki wa kazi yao wenyewe. Wanaweka mkazo zaidi kwenye kurejesho hesabu ya mabosi wao kuliko kuisimimaia biashara kwa ajili...
S1E12 Kwa nini hatuwezi kulipa madeni?? (2/3 ya watanzania hawawezi kumudu gharama za maisha) 19.08.2023 13:31
Ripoti ya @finscope ya 2023 imeongelea mambo mengi ikiwa ni pamoja na sababu zinazowafanya Watanzania kukopa fedha. Katika kuichambua zaidi hii ripoti na kuunganisha taarifa nyingine (nje ya ripoti) tumegundua kuwa watu wengi wanaamini kwamba kumekuwepo na u]kukosekana kwa uaminifu baina yta watu hususani kwenye masuala ya kifedha ambapo watu walio wengi wanakopa na wanakuwa hawalipi madeni yao....
S1E11 Zijue Kazi 10 Mpya Kwenye Soko la Ajira (Duniani!) 12.08.2023 14:16
Kama ni mwanafunzi, episode hii itakusaidia kuchagua kozi sahihi za kusomea vyuoni katika kipindi hiki ambacho ajira hazitabiliki. Kozi zenye ajira leo zinaweza zisiwe na nafasi za ajira tena sokoni ndani ya mmiaka michache. Mfanyakazi yeyote asiyejiendeleza (binafsi) kwa kuongeza maarifa yake katika anachokifanya, uwezekano wake wa kufanikiwa kwenye Maisha ni mdogo. Kutokana na mabadiliko ya maen...
S1E10 SIRI 5 za KUKUA, na KUFANIKIWA kwenye KAZI (AJIRA) na maisha 05.08.2023 14:53
Elimu rasmi ni muhimu sana katika kufungua milango ya kazi (ajira); lakini vyeti peke yake havitoshi kukupa mafanikio unayotamanni kuyapata kwenye Maisha kwa kupitia kazi/ajira yako. Kuna mbinu na kanuni nyingi ambazo hazifundishwi kwenye mifumo ya elimu rasmi lakini zinapatikana mtaani baada ya kuanza kufanya kazi. Mfanyakazi yeyote asiyejiendeleza (binafsi) kwa kuongeza maarifa yake katika anach...
S1E9 Biashara na Wajasiriamali 7 wenye washindani usioutegemea (bila kujali pesa) - Unusual Rivals 29.07.2023 18:00
Unveiling the Hidden Rivals: How Unexpected Foes Shape the Market! 🚀 Discover the secret competition behind the scenes as seemingly unrelated products and services battle for your attention and loyalty. From phone-camera filters vs cosmetics makers to writing AI vs editors, we expose the surprising clashes that influence customer choices. 🤔 Join us for an eye-opening journey into the world of in...
S1E8 [Part 2] Simu Sio Chanzo za Migogoro kwenye Mahusiano ft. Teacher Gonza 22.07.2023 24:37
Katika ulimwengu huu ambao matumizi ya simu na mitandao ya kijamii yamekuwa makubwa, simu zinadhaniwa kuwa mojawapo ya vyanzo vikuu vinavyosababisha migogoro na kuvunjika kwa mahusiano na ndoa. Msikilize Michael Kamukulu pamoja na Teacher Gonza wakielezea ni kwa namna gani simu SIO chanzo cha migogoro ya mahusionao kama wengi wanavyodhani.
S1E7 [Part 1] Simu Sio Chanzo cha Migogoro kwenye Mahusiano ft Teacher Gonza 15.07.2023 25:57
Katika ulimwengu huu ambao matumizi ya simu na mitandao ya kijamii yamekuwa makubwa, simu zinadhaniwa kuwa mojawapo ya vyanzo vikuu vinavyosababisha migogoro na kuvunjika kwa mahusiano na ndoa. Msikilize Michael Kamukulu pamoja na Teacher Gonza wakielezea ni kwa namna gani simu SIO chanzo cha migogoro ya mahusionao kama wengi wanavyodhani.
S1E5. UBUNIFU [Part 2]: Jinsi DIGITALI inavyofungua milango ya FURSA za uzalishaji wa MAUDHUI na MAWASILIANO ft. Jane Shussa 08.07.2023 28:02
Katika episode hii, Michael Kamukulu anaongea na Jane Shussa kuhusu jinsi mabadiliko ya kidigitali yanavyobadilisha namna ya UZALISHAJI WA MAUDHUI na MAWASILIANO. Pamoja, wanachunguza athari za mabadiliko haya kwenye sekta mbalimbali. Wanaongeleo pia usalama mitandaoni nan je ya mitandao katika zama hizi mpya. Jiunge nao kwenye mada hii ya kuvutia inayojikita katika mabadiliko yasiyokwepeka kwa wa...
S1E5. UBUNIFU [Part 1]: Jinsi DIGITALI inavyofungua milango ya FURSA za uzalishaji wa MAUDHUI na MAWASILIANO ft. Jane Shussa 01.07.2023 28:10
Katika episode hii, Michael Kamukulu anaongea na Jane Shussa kuhusu jinsi mabadiliko ya kidigitali yanavyobadilisha namna ya UZALISHAJI WA MAUDHUI na MAWASILIANO. Pamoja, wanachunguza athari za mabadiliko haya kwenye sekta mbalimbali. Wanaongeleo pia usalama mitandaoni nan je ya mitandao katika zama hizi mpya. Jiunge nao kwenye mada hii ya kuvutia inayojikita katika mabadiliko yasiyokwepeka kwa wa...
S1E4. [Part 2] Je, tuko salama kwenye ulimwengu wa Data na Teknolojia? ft. Miriam Mwaibula 24.06.2023 20:58
SEHEMU YA PILI Zifahamu siri na maarifa ya kuwa salama katika zama mpya za Data na Teknolojia. Jifunze: Data ni nini? Matumizi salama ya mitandao! Utunzaji wa taarifa muhimu, na mengine mengi...
S1E3. [Part 1] Je, tuko salama kwenye zama mpya za Data na Teknolojia? ft.Miriam Mwaibula 17.06.2023 23:10
Zifahamu siri na maarifa ya kuwa salama katika zama mpya za Data na Teknolojia. Jifunze kuhusu: 1. Maana ya data na takwimu! 2. Matumizi salama ya mitandao! 3. Utunzaji wa taarifa muhimu, na mengine mengi...
S1E2. SIRI ya kufanya KAZI mbili: Moja ikitegemea ELIMU na nyingine ikitegemea KIPAJI ft. Grace Brown 10.06.2023 26:32
Katika soko gumu la ajira ambapo wanaopoteza kazi ni wengi kuliko wanaopata kazi mpya, Grace Brown anaelezea ni kwa jinsi gani yeye anaweza kufanya kazi mbili, moja ikitegemea KIPAJI chake wakati nyingine ikitegemea ELIMU yake. In the tough job market where there are more people losing jobs than finding new ones, Grace Brown explains how she can work two jobs, one relying on her TALENT and the oth...
S1E1: Fahamu kwa nini takribani 1/4 ya shule zote za Msingi za Binafsi Tanzania ziko Dar es Salaam 03.06.2023 25:48
Fahamu kwa nini takribani 22% ya shule za msingi za binafsi ziko Dar es Salaam wakati 25% nyingine ikiwa katika mikoa ya Mwanza, Arusha, Kilimanjaro na Pwani. 📺 Video Podcast Description: "Unlocking Tanzania's Private Education Secret: Inside Dar es Salaam's School Boom!" English Description 🏫 Discover the captivating story behind Dar es Salaam, Tanzania's private education...
LENZI Podcast Trailer 08.05.2023 1:16
Jifunze kupitia mijadala na maelezo yanayohusu mada mbalimbali ili upate ufahamu juu mienendo ya sasa katika nyanja na tasnia tofauti. Tunakupatia uchanmguzi wa takwimu rasmi katika kuleta uhalisia wa mada tunazozijadili. Uwe ni mmiliki wa biashara unayetaka kuboresha shughuli zako, mfanyabiashara unayetafuta kufungua mradi mpya, au mtu binafsi anayetaka kuongeza ufanisi wako, podcast yetu ina kit...
Podcasturi asemănătoare
Replaio nu este editorul podcasturilor; numele emisiunilor, coperțile și materialul audio aparțin autorilor lor și sunt distribuite prin fluxuri RSS publice