RFI Kiswahili
Jukwaa la Michezo
Makala haya yanaangazia maendeleo ya michezo mbalimbali Ulimwenguni na pia huwa haiwaweki kando wanamichezo waliobobea na vilevile kufanya uchanganuzi wa kina wa michezo wakati wa mashindano mbalimbali.
Vizitează neapărat site-ul podcastului și susține-i creatorul: www.rfi.fr
Unde asculți?
Podcasturi în aplicație Replaio Radio În curândPodcasturile ajung în curând în aplicație. Instaleaz-o acum și fii primul care descoperă o abordare complet nouă a podcasturilor
Episoade
Mkutano Mkuu wa CAF, Raundi ya nne Kufuzu AFCON 2027, Uchaguzi wa FIFA 21.11.2026 23:53
Tuliyokuandalia leo ni pamoja na yaliyojiri kwenye mkutano mkuu wa CAF wa 48, uchambuzi na matokeo ya raundi ya nne kufuzu michuano ya Afcon 2027, nembo ya michuano hiyo ikitolewa huku makao makuu yakipelekwa Tanzania, mechi za kufuzu AFCON U23, marufuku ya Peres Jepchirchir, FIFA yatangaza kupokea wagombea watatu kuwania urais mwaka ujao, raundi ya kwanza Kombe la Dunia chini ya miaka 17, ratiba...
Olimpiki ya vijana ikitamatika, Raundi ya tatu kufuzu AFCON 2027 imeanza 15.11.2026 23:51
Leo tutaangazia mashindano ya Olimpiki ya vijana kutamatika jijini Dakar, Senegal, uchambuzi wa raundi ya tatu ya mechi za kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika 2027, fainali ya klabu bingwa Afrika kwa kina dada, AFCON U23, ukuaji wa gofu ya kina dada Tanzania. Azma ya Arsene Wenger kuwania urais wa FIFA, Michael Carrick afutwa kazi Man Utd Pochettino atajwa kocha mpya.
Je, Afrika iko tayari kuandaa michezo mikuu ya Olimpiki ya majira ya joto? 08.11.2026 24:05
Leo kwenye kipindi tunapiga darubini na tathmini ya uwezo wa Afrika kuandaa michezo mikuu ya Olimpiki baada ya kuandaa michezo ya Olimpiki ya vijana kwa mara ya kwanza, tuzo za CAF mwaka huu, klabu ya APR yaondolewa kwenye Ligi ya BAL, fainali ya handboli Afrika kwa kina dada, kocha mpya wa Yanga, Nigeria yashinda Kombe la Dunia la wasichana chini ya miaka 17, derby ya Lubumbashi kati ya Lupopo na...
DAKAR 2026: Kenya yashinda dhahabu, Burundi yashinda shaba katika wiki ya kwanza 07.11.2026 23:49
Tuliyokuandalia leo - wiki ya kwanza kwenye michezo ya Olimpiki ya vijana Dakar, Senegal; Kenya yashinda dhahabu Huku Burundi ikishinda shaba. Michuano ya klabu bingwa kwa kina dada Afrika. Tiketi za mechi ya Bayern dhidi ya Ajax. Nigeria yatinga fainali ya Kombe La Dunia la wasichana chini ya miaka 17. Naibu rais wa FKF Mcdonald Mariga aondolewa katika wadhfa wake. Mshambuliaji wa Tenerife Jesus...
Kenya yatinga nusu fainali kwenye Baseball5 michezo ya Olimpiki ya Vijana 01.11.2026 24:01
Leo tumeangazia Michezo Ya Olimpiki Ya Vijana Yaingia Siku Ya Pili Jijini Dakar, Senegal, Kwenye mjadala: Uwanja Wa Talanta Kufunguliwa Na Mechi Kati Ya Bayern Munich Dhidi Ya Ajax na Nafasi Ya Mwafrika Kushinda Tuzo La Ballon D’or Iko Wapi? Samson Adamu Ndiye Katibu Mkuu Mpya Wa Caf, Kuanza kwa Klabu Bingwa Kwa Kina Dada, DRC yang'ara Mashindano Ya Ndondi Mjini Kinshasa, Droo Ya Handboli Ya Afrik...
Kila unachofaa kufahamu kuhusu michuano ya Olimpiki ya vijana ya 2026 01.11.2026 24:04
Leo tunazungumzia kuanza kwa mashindano ya Olimpiki ya Vijana jijini Dakar, Senegal, CAF kurejesha AFCON kila ya baada ya miaka miwili, droo ya michuano ya klabu bingwa Afrika, ufunguzi wa uwanja wa Talanta nchini Kenya wazua gumzo kubwa, Kenya yabanduliwa michuano ya Kombe la Dunia chini ya miaka 17, DRC yaibuka bingwa wa mashindano ya Afrika ya ndondi huku Harry Kane akishinda tuzo la Ballon d'O...
Mechi za kufuzu Afcon U20, U17, Olimpiki, Klabu Bingwa Afrika na F1 17.10.2026 23:59
Mechi za kufuzu Afcon U20, U17 na Olimpiki ya 2028 zinaendelea, Raundi ya pili ya kufuzu mechi za klabu bingwa, Tanzania yabanduliwa kwenye mashindano ya Afcon mchezo wa futsal, CAF na FIFA zaongeza ruzuku kwa wanachama wake, Mchezo wa langalanga kurejea Afrika kuanzia mwaka 2030, Raga ya dunia daraja la pili kurejea Kenya, Kombe la dunia la wasichana chini ya miaka 17 lang’oa nanga nchini Morocco...
Debi la Kariakoo Simba na Yanga, nani atashinda leo, Mkutano wa CAF wa Kimkakati 10.10.2026 23:57
Tuliyokuandalia leo ni pamoja na michuano ya kufuzu Afcon U23, U20 na U17, Olimpiki ya LA 2028, yaliyojadiliwa katika mkutano wa kimkakati wa CAF, debi la kariakoo leo usiku kati ya Yanga na Simba, Ligi kuu ya soka Kenya yarejea huku mwamuzi akivamiwa, Safari Rally yarejea katika kalenda ya WRC 2027, Rwanda ipo karibu kufikia makubaliano ya kuandaa mkondo wa F1 mwaka 2030, Messi astaafu soka la ki...
CAF: Raundi ya pili kufuzu Afcon 2027, Ronaldo aondoka katika kambi ya Ureno 03.10.2026 23:57
Tuliyokuandalia leo ni pamoja na uchambuzi wa matukio na matokeo ya raundi ya pili kufuzu michuano ya Kombe la Mtaifa ya Afrika 2027, mechi za kufuzu Afcon U23 na U20, kocha wa Ghana afutwa kazi, Jnr Starlets ya Kenya wajiandaa kushiriki Kombe la Dunia la wasichana U17, ukumbi wa kwanza wa ndondi ya kina dada nchini Sudan Kusini, mkusanyiko wa spoti Afrika Mashariki, Ronaldo ajiondoa kwenye kambi...
Raundi ya kwanza kufuzu AFCON 2027 imekamilika, Fainali za Netboli na Voliboli 26.09.2026 24:02
Tuliyokuandalia leo ni pamoja na matokeo na matukio ya raundi ya kwanza mechi za kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika 2027, fainali za mashindano ya netboli na voliboli Afrika na Cecafa U20, kambi ya Harambee Stars yakumbwa na misukosuko, je kocha McCarthy ana imani na shirikisho la soka Kenya?, Ligi ya Kenya kurejea, Lupita Nyong'o awekeza klabuni Nairobi City Thunder, je Mbappe anaweza kushinda Bal...
Riadha za 2029 zatua Nairobi, ziara ya Motsepe Afrika Mashariki 19.09.2026 23:53
Tuliyokuandalia leo ni pamoja na Nairobi kushinda haki za kuandaa riadha za dunia mwaka 2029, michuano ya voliboli Kombe la Mataif ya Afrika ya wanaume, golikipa wa Senegal Edouard Mendy anuia kustaafu soka la kimataifa, ziara ya Motsepe Kenya na Tanzania kukagua viwanja vya Afcon 2027, ni kwa nini ligi ya Kenya haijaanza, michuano ya Cecafa U20, kocha mpya wa Ufaransa Zinadine Zidane ampa unahodh...
Awamu ya marudiano kufuzu klabu bingwa Afrika, Tuzo za Ballon d'Or 2026 12.09.2026 23:57
Raundi ya kwanza ya kufuzu klabu bingwa Afrika yatamatika, Inaki Williams astaafu soka la kimataifa, yaliyojadiliwa kwenye kongamano la tatu la Sportsbiz Afrika, moto wa Olympiki kuelekea Olimpiki ya Dakar wawashwa, FIFA yapuuza madai ya Morocco kuandaa Kombe la Dunia la 2030, waafrika waliotajwa kwenye orodha ya tuzo za Ballon d'Or, Ufaransa yajiondoa kumuunga mkono Infantino kuchaguliwa urais te...
Misri yashinda ubingwa wa Afrika voliboli, Tanzania na Uganda mabingwa Cecafa 05.09.2026 23:51
Tuliyokuandalia ni pamoja na Misri kushinda ubingwa wa Afrika wa voliboli wa kina dada, Quieroz arejea Ghana huku Pitso Motsimane akiteuliwa kocha wa Afrika Kusini, Ligi ya Mabingwa Afrika yang'oa nanga, Tanzania na Uganda zashinda taji za Cecafa michuano ya shule za upili CAF, droo ya Afcon U20 yatolewa, riadha za Diamond League, kocha wa PSG Luis Enrique atia saini mkataba mpya, Djokovic abandul...
Michuano ya voliboli ya Afrika ya kina dada yaingia raundi ya mtoano 29.08.2026 23:57
Tuliyokuandalia leo ni pamoja na Nigeria kuapisha shirikisho la mpito kusimamia soka, Ethiopia yawasilisha ombi la kuandaa Afcon 2028, DRC yabanduliwa michuano ya Afrika ya Voliboli, mechi za kufuzu Kombe la Dunia la Basketboli yaingia raundi ya pili; wakenya Faith na Wanyonyi wang'ara riadha za Zurich Diamond League, Rayon Sport yajiandaa mechi za Kombe la Shirikisho, Kenya yaibuka bingwa mashind...
Vieira ndiye kocha mpya wa Senegal, uwanja wa Talanta wafikia asilimia 95 22.08.2026 23:54
Leo tunaangazia ushindi wa Cameroon taji la Wafcon, Patrick Vieira ndiye kocha mpya wa Senegal, Wanyonyi ang'ara riadha za Diamond League, bondia wa mwafrika kusini auawa nchini Afrika Kusini, uwanja wa Talanta umefikia asilimia 95 kukamilika, michuano ya kufuzu klabu bingwa kwa kina dada ukanda wa Cecafa yaanza, ratiba ya Kombe la Dunia la wanawake 2027 yatolewa, Shakhtar kutumia uwanja wa Stamfo...
Malawi na Cameroon zatinga fainali michuano ya WAFCON 2026 nchini Morocco 15.08.2026 24:00
Tuliyoangazia leo ni pamoja na uchambuzi wa matokeo na matukio ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa kina dada inayofikia tamati wikendi hii, mechi za kufuzu kombe la dunia la basketboli chini ya miaka 18, Kenya yawasilisha nia ya kuandaa mashindano ya dunia ya riadha 2029. Je, Yanga itatetea ubingwa wa ligi kuu Tanzania baada ya kushinda ngao ya jamii?, PSG yashinda taji la UEFA Super Cup, tetesi za...
WAFCON yaingia mtoano, Rayon mabingwa wa CECAFA, CAF yamuunga mkono Infantino 08.08.2026 20:48
Tumeangazia uchambuzi wa matokeo na matukio kwenye Kombe la Mataifa ya Afrika kina dada inayoingia kwenye mtoano, droo ya michuano ya klabu bingwa, CAF yamuunga mkono rais Infantino, Rayon yashinda ubingwa CECAFA baada ya miaka 28, Simba Day ni leo, mshindi wa medali ya fedha mbio za kutembea mita 10,000 kwenye michezo ya Jumuiya ya Madola 2026 Stephen Ndangiri apigwa marufuku kwa tuhuma za kutumi...
Darubini ya mashindano ya Wafcon, Jumuiya ya Madola na Cecafa Kagame Cup 01.08.2026 23:55
Leo kwenye kipindi tunaangazia WAFCON inayoendelea nchini Morocco - Kenya yaaga mashindano huku Tanzania ikisalia na matumaini lakini Nigeria na Afrika Kusini zimeanza kwa kusuasua, wanariadha wanaendelea kunyakua medali katika mashindano ya Jumuiya ya Madola nchini Scotland, wakati mashindano ya Cecafa Kagame Cup yakiingia nusu fainali.
CAF: Wafcon, mashindano ya jumuiya ya madola na Kombe la Cecafa yaanza 25.07.2026 23:55
Tuliyokuandalia leo ni pamoja na kuanza kwa mashindano ya kina dada ya Afcon, Kombe la Cecafa, mashindano ya Jumuiya ya Madola, tetesi za uhamisho Ulaya na Afrika Mashariki, mahakama ya kutatua migogoro duniani kuskiza kesi ya kubaini bingwa wa Afcon 2025 mwezi Oktoba tarehe nane.
Ufaransa na Uingereza zaondolewa kwenye nusu fainali Kombe la Dunia 18.07.2026 23:55
Tuliyokuandalia leo ni pamoja uchambuzi wa nusu fainali, mechi ya mshindi wa tatu na taarifa kuu kuhusu Kombe la Dunia kuhusu washindi kutuzwa pete pamoja na medali na kombe huku Ballon d'Or yatangaza mchezaji anayecheza nje ya Ulaya ana uwezo wa kushinda tuzo hiyo. Timu ya taifa ya kina dada ya Kenya na Tanzania zasafiri kwa ajili ya Kombe la Mataifa ya Afrika nchini Morocco, fainali ya Congo Cup...
Mbio za nusu fainali Kombe la Dunia, Kocha mpya wa Yanga ni nani? 11.07.2026 23:58
Tuliyokuandalia leo ni pamoja na uchambuzi wa raundi ya 16 bora na robo fainali michuano ya Kombe la Dunia, Misri na Morocco zikiaga mashindano, Mbappe na Messi wang'ang'ania kiatu cha dhahabu, Yanga yapata kocha mpya Manqoba Mngqithi kutoka Afrika Kusini, Emmanuel Wanyonyi avunja rekodi ya mita 1000m mashindano ya Diamond League, mchezo mpya wa Flag Football waendelea kukua na kupata umaarufu Afr...
Kombe La Dunia 2026: Raundi ya 32 yakamilika, Morocco na Misri zafuzu 16 bora 04.07.2026 23:57
Tuliyokuandalia leo ni mkusanyiko wa matukio ya raundi ya 32, je ni wakati timu changa kuanza kutamba? Timu mbili tu za Afrika kati ya tisa zafuzu kumi na sita bora, nini kimeiponza Afrika? uchambuzi wa raundi ya 16 bora inaanza leo, kiatu cha dhahabu na mechi za kufuzu Kombe la Dunia la wasichana chini ya miaka 17. Yanga yashinda ubingwa wa Tanzania kwa mara ya 32 huku DRC ikifuzu raundi ya pili...
Kombe la Dunia 2026: Timu saba za Afrika zafuzu hatua ya muondoano 27.06.2026 23:57
Hatua ya makundi kwenye Kombe la Dunia inafikia kilele hii leo, ni timu gani zimefuzu hatua ya mtoano? Wiki ya pili ya michuano hii imeshuhudia rekodi zikiwekwa na kuvunjwa huku mataifa ya Afrika yakiendelea kufanya vizuri zaidi, lakini pia tutakupa uchambuzi wa mechi za kesho asubuhi. Aidha tumeangazia michuano ya Afrika Mashariki mchezo wa Baseball, tetesi za uhamisho na mashindano ya Paris Diam...
Wiki ya kwanza Kombe la Dunia 2026. Matokeo na Matukio yaliyojiri 20.06.2026 24:03
Leo tumeangazia kwa undani matukio na matokeo yote ya wiki ya kwanza michuano ya Kombe la Dunia 2026 - Mbappe, Messi waweka historia wakati Cape Verde na DRC zikihangaisha miamba wa soka wa ulaya, Tunisia yamfuta kazi kocha, uchambuzi wa mechi za leo. Aidha ni mwaka mmoja kuelekea Kombe la Mataifa ya Africa 2027, matokeo ya tenisi kombe la Davis Cup, Police fc ya Rwanda yamfuta kazi kocha wake, ma...
Kombe la Dunia laanza likitatizika kuwasha msisimko Marekani, Mexico na Canada 13.06.2026 24:02
Tumeangazia Kombe la Dunia 2026 kuanza kwa vikwazo kadhaa, raia wa Afrika waiunga mkono Mexico dhidi ya Afrika Kusini, uchambuzi wa mechi ya leo Brazili dhidi ya Morocco, DRC wakijiandaa kupambana na Ureno wiki ijayo, maandalizi ya mbio za Kigali Marathon zakamilika, klabu ya Gor Mahia nchini Kenya yaamrishwa kufanya uchaguzi upya,
Replaio nu este editorul podcasturilor; numele emisiunilor, coperțile și materialul audio aparțin autorilor lor și sunt distribuite prin fluxuri RSS publice