Goodluck Joseph
Wanangu podcast
This podcast is hosted by Goodluck Joseph, a curious guy who likes to share all the things he finds interesting in the form of a podcast episode. In other words, this podcast is an extension of his personality and more. Expect to hear topics that range from music, movies, and books to random ideas, all presented in a creative manner.
Where to listen?
Podcasts in the app Replaio Radio Coming soonPodcasts are coming to the app soon. Install now and be the first to see a whole new take on podcasts
Episodes
Episode 74 | Kuzima kwa MTV 05.01.2026 8:24
Kufuatia Paramount kuzifunga chaneli za MTV zilizokuwa zikipiga muziki pekee sehemu mbali mbali duniani, episode hii inakuletea makala fupi iliyolenga kukujuza kuhusu kuchipua, kukua, kubadilika na hatimaye kuporomoka kwa brand hii iliyoweka alama mioyoni mwa watu wengi.
Episode 73 | Consistency 29.12.2025 13:22
Katika episode hii ya mwisho kwa mwaka 2025, host anapata nafasi ya kuzungumza na rafiki yake kuhusu alichojifunza ndani ya mwaka huo, kazi za sanaa alizozifurahia zaidi, matumizi ya AI na mengineyo.
Episode 72 | Little rooms 22.12.2025 12:19
Kupitia hotuba ya Andre 3000 kwenye Rock n' roll hall of fame 2025, tunakumbushwa kwamba mafanikio mengi makubwa duniani huanzia kwenye vyumba vidogo sana (Little rooms).
Episode 71 | Netflix yazidi kutanua mbawa 15.12.2025 10:53
Netflix yainunua Warner Bros. kwa bilioni za kimarekani 82.7. Hii inamaanisha nini kwenye kiwanda cha filamu duniani?
Episode 70| Makala ya Diddy 08.12.2025 14:13
Episode hii inaangazia makala (Documentary) mpya iliyotolewa na 50 Cent kumuhusu hasimu wake Diddy.
Episode 69 | Hiphop vs Singeli 01.12.2025 10:33
"Hiphop na Singeli ni aina mbili za muziki tofauti kabisa!" Sikiliza episode hii uone jinsi gani kauli hii inavyopoteza mashiko.
Episode 68 | Timbaland, why? 10.11.2025 11:10
Pale mtayarishaji bora na gwiji wa muziki anapoamua kukumbatia teknolojia mpya katika muziki na kusahau haki na fursa ambazo teknolojia hiyo inazivunja na kunyima wasanii, nafasi yake inabakia wapi?
Episode 67 | Sauti Sol 27.10.2025 11:22
Safari ya Sauti Sol katika muziki, kuanzia kuundwa kwa bendi, kazi walizofanya na hatimaye kuvunjika.
Episode 66 | Camp Mulla: Jiwe walilokataa waashi. 20.10.2025 17:53
Fuatilia hadithi ya namna Camp Mulla ilivyokuja kuwa moja ya makundi ya muziki ambayo hayatasahaulika kwa miaka mingi ijayo.
Episode 65 | Je, Ayesha Curry hana shukrani? 13.10.2025 8:43
Katika ulimwengu huu uliyojaa maoni ya kila namna kupitia mitandao ya kijamii, pale mke wa moja ya nyota wa mpira wa kikapu duniani anapoitwa asiye mwenye shukrani, kuna lipi la kujifunza?
Episode 64 | Viashiria vinapogeuka mtego 06.10.2025 13:10
Je, viashiria vinapogeuka kuwa malengo, bado vinaonyesha hali halisi? Jua kwanini mara nyingi namba hazielezi ukweli wote. Sikiliza namna ya kutambua mtego wa viashiria katika maisha ya kila siku.
Episode 63 | Charlie Kirk 22.09.2025 12:32
Katika episode hii host anazungumzia mauaji ya mwanaharakati Charlie Kirk aliyepigwa risasi mnamo tarehe 10 septemba, 2025 huko Utah nchini marekani. Yapi hasa yalikuwa ni maisha aliyoishi enzi za uhai wake, na ni itikadi zipi alizozisimamia zilizosababisha kutokea kwa mauaji hayo? Tega sikio.
Episode 62 | Sanaa ya kuachilia 15.09.2025 10:04
Katika maisha, mara nyingi tunafundishwa kujifunza mambo mapya, lakini wachache hufundishwa kuachilia yale yasiyotufaa tena. Katika kipindi hiki tunazungumzia sanaa ya kuachilia , yaani uwezo wa kuacha imani, mitazamo, na mazoea yaliyopitwa na wakati ili kufungua nafasi ya ukuaji mpya.
Episode 61 | Vua gamba 08.09.2025 12:08
Kambakoche anaweza kutufundisha nini kuhusu maisha? Katika kipindi hiki tunaangazia ukweli kwamba mara nyingine shinikizo katika maisha ni ishara ya kukua.
Episode 60 | Usiendeshwe na matokeo 01.09.2025 12:30
Kumbe matokeo ya mitihani huathiri maisha sio tu ya wale waliofanya vibaya bali hata waliofaulu vizuri. Katika episode hii host anatumia hadithi ya kweli kufikisha ujumbe huo. Pia, pata kusikia kuhusu segment mpya iliyoongezeka kwenye show. Karibu!
Episode 59 | Kwanini chenji ni tatizo Tanzania? 25.08.2025 11:45
Kwa nini kupata chenji baada ya kununua kitu ni tatizo nchini Tanzania? Katika episode hii host anajadili sababu, madhara na suluhisho la kadhia hii.
Episode 58 | AGI: The dinosaurs of AI 18.08.2025 11:38
Kuna uhusiano gani kati ya dinosaurs (Mijusi mikubwa ya kale) na Akili bandia? Katika episode hii, host anazungumzia maana halisi ya AGI, historia yake, maoni ya wataalamu, na kwa nini mustakabali wake unaweza kuwa muhimu, wenye kutisha na usiotabirika.
Episode 57 | Marion Stokes 11.08.2025 13:07
Kutana na Marion Stokes mmarekani aliyekuwa akirekodi vipindi vya televisheni nyumbani kwake masaa 24 kila siku kwa miaka 35 mfululizo.
Episode 56 | Makoma 04.08.2025 14:59
Fuatilia kuinuka, kupaa, kuanguka, na kunyanyuka tena kwa moja kati ya makundi bora na muhimu ya muziki wa injili kuwahi kutokea barani Afrika.
Episode 55 | Pretty privilege 28.07.2025 13:38
Baada ya likizo isiyokuwa rasmi, host anarejea na 'Pretty privilege', episode iliyojikita katika kudadavua maana ya dhana inayodai kwamba watu wenye mvuto au uzuri hupendelewa katika nyanja mbali mbali za kimaisha. Karibu!
Episode 54 | Chinese bamboo 19.05.2025 12:00
Katika kipindi hiki, unatumika mfano wa mianzi ya kichina (Chinese bamboo) na jinsi inavyotufundisha uvumilivu, ustahimilivu, na imani katika maisha. Kama mimea hii, inavyochukua muda mrefu bila kuonyesha dalili zozote za ukuaji kabla ya kukua ghafla kwa kasi, juhudi zetu pia mara nyingi huchukua muda kuzaa matunda.
Episode 53 | Nadharia ya njama 12.05.2025 14:51
Fahamu maana halisi ya 'Nadharia ya Njama' (Conspiracy theory) na chunguza kwa undani sababu zinazowafanya watu kuvutiwa au kuamini juu ya nadharia hizo. Host wako anakupa mtazamo mpana na mifano halisi kuhusiana na jinsi gani nadharia hizi huenea na kupokelewa kwa urahisi katika jamii.
Episode 52 | Umesikia kuhusu vibe coding? 14.04.2025 12:04
Akili bandia inazidi kutuonyesha kwamba haijaja kucheza na sisi. Sikiliza jinsi unavyoweza kutengeneza software bila utaalamu wowote, kinachotakiwa ni vibe yako tu!
Episode 51 | Sakata la Luigi Mangione (Part 2) 07.04.2025 11:56
Episode hii ni mwendelezo (part 2) wa episode 48 kuhusu kisa cha Luigi Mangione (26) anayeshitakiwa kwa kosa la kumuua aliyekuwa CEO wa kampuni ya bima ya afya nchini marekani, Brian Thompson.
Episode 50 | 'The ICU is the ICU.' 31.03.2025 13:32
Kama binadamu tunajifunza kupitia mambo mengi, sikia funzo hili ambalo host amelipata wakati akirudia kuangalia series ya Succession.
Similar podcasts
Replaio is not a podcast publisher; show names, artwork and audio belong to their authors and are distributed through public RSS feeds.