Neno la Leo 255
Neno la Leo
Hii ndiyo siku aliyoifanya Bwana (Zaburi 118:24). Anza siku mpya ya Yesu kwa kusiliza na kutafakari nasi “Neno la Leo” kila siku kwa lugha ya Kiswahili.
Be sure to visit the podcast's website and support the creator: rss.com
Where to listen?
Podcasts in the app Replaio Radio Coming soonPodcasts are coming to the app soon. Install now and be the first to see a whole new take on podcasts
Episodes
Si Kila Siku Ni Muujiza, Lakini Kila Siku Inahitaji Uaminifu 18.08.2026 9:44
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 1 Samweli 7:15–17 tunamwona Samweli baada ya ushindi mkubwa wa Israeli dhidi ya Wafilisti. Ameweka jiwe la Ebenezeri na kukumbuka msaada wa Mungu lakini hakubaki akiishi katika ushindi wa jana. Biblia inasema aliendelea kuhukumu Israeli siku zote za maisha yake na kila mwaka alizunguka maeneo mbalimbali akitekeleza wajibu wake. Hapa tunajifunza upande muhimu w...
Hata Sasa Bwana Ametusaidia! 17.08.2026 8:03
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 1 Samweli 7:12 tunafika katika wakati wa ushindi baada ya Israeli kumrudia Mungu. Samweli anasimamisha jiwe na kuliita Ebeneza , akisema, “Hata hapa Bwana ametusaidia.” Jiwe hilo lilikuwa ukumbusho kwamba hawakufika pale kwa nguvu zao wenyewe bali kwa msaada wa Mungu. Nasi tunapoitazama safari ya maisha yetu kuna milima tuliyodhani hatutaivuka, milango tuliyod...
Huwezi Kumtumikia Mungu kwa Moyo Uliogawanyika! 16.08.2026 20:28
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 1 Samweli 7:3 tunamwona Samweli akiwaita Waisraeli warudi kwa Mungu baada ya miaka ya kupotea. Lakini kurudi kwao hakukuwa suala la kusema tu kwamba wametubu. Samweli aliwataka waondoe miungu mingine na wamwelekee Bwana kwa mioyo yao yote . Neno la leo linatufundisha kwamba toba ya kweli si majuto pekee, lazima ionekane katika mabadiliko ya maisha. Huenda sisi...
Usimzoee Mungu Mpaka Ukasahau Utakatifu Wake! 15.08.2026 8:05
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 1 Samweli 6:20 tunakutana na swali zito: “Ni nani awezaye kusimama mbele za Bwana, huyu Mungu mtakatifu?” Baada ya kuona jinsi Mungu alivyoonyesha nguvu zake dhidi ya Wafilisti, sasa Waisraeli wanakumbushwa kwamba Mungu si mwenye nguvu tu, Yeye ni mtakatifu . Neno la leo linatukumbusha kwamba tunaweza kumzoea Mungu kiasi cha kupoteza kicho na heshima tunayopas...
Israeli Walishindwa, Lakini Mungu Hakushindwa! 14.08.2026 23:26
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 1 Samweli 5:3–4 tunaendelea na simulizi ya Sanduku la Agano baada ya kutekwa na Wafilisti. Wanalichukua na kuliweka katika hekalu la Dagoni kana kwamba ushindi wao dhidi ya Israeli ulimaanisha kuwa mungu wao alikuwa amemshinda Mungu wa Israeli. Lakini asubuhi Dagoni anakutwa ameanguka chini mbele ya Sanduku. Wanamwinua na siku inayofuata anaanguka tena, safari...
Unaweza Kuwa na Dini Lakini Ukakosa Uwepo wa Mungu! 13.08.2026 15:28
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 1 Samweli 4:21–22 tunakutana na moja ya nyakati nzito katika historia ya Israeli. Taifa limeshindwa vitani, Sanduku la Agano limetekwa na mtoto anapewa jina Ikabodi , likiashiria kwamba utukufu umeondoka Israeli. Lakini tatizo halikuwa kupoteza Sanduku pekee. Israeli walikuwa wameanza kutegemea ishara ya uwepo wa Mungu badala ya Mungu mwenyewe. Walitaka ushind...
Usitafute Baraka Pekee, Tafuta Uwepo wa Mungu! 12.08.2026 19:07
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 1 Samweli 3:19 tunaona Samweli akiendelea kukua na kuingia katika kusudi lake kama nabii. Lakini Biblia inatuonyesha siri iliyokuwa nyuma ya safari yake: “Bwana alikuwa pamoja na Samweli.” Mafanikio yake hayakuanzia katika kipawa, uwezo au nafasi yake bali katika uwepo wa Mungu uliokuwa pamoja naye. Hili linatufundisha kwamba tunaweza kuwa na mipango mizuri, e...
Acha Kuzungumza Tu, Jifunze Kumsikiliza Mungu! 11.08.2026 9:43
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 1 Samweli 3:9–10 tunafika katika moja ya nyakati muhimu sana katika maisha ya Samweli: Mungu anamwita kwa jina. Samweli alikuwa tayari akimtumikia Mungu lakini bado hakujifunza kuitambua sauti yake. Baada ya kuelekezwa na Eli, anajibu, “Sema, kwa maana mtumishi wako anasikiliza.” Kupitia simulizi hii tunajifunza kwamba uhusiano wetu na Mungu hauwezi kuwa sisi...
Kumuheshimu Mungu ni Njia ya Kwenda Mbele! 10.08.2026 20:28
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 1 Samweli 2:30 tunaingia katika simulizi ya familia ya Eli na kukutana na kanuni nzito kutoka kwa Mungu: “Wale wanaoniheshimu nitawaheshimu.” Wana wa Eli walikuwa na nafasi ya kuheshimiwa kama makuhani lakini walitumia nafasi hiyo vibaya na kuidharau kazi ya Mungu. Kupitia maisha yao tunajifunza kwamba mbele za Mungu cheo, nafasi au kuonekana wa kiroho hakutos...
Mungu Anakuandaa Kupitia Ukuaji wa Taratibu. 09.08.2026 10:11
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo simulizi linahamia kwa Samweli kupitia 1 Samweli 2:26 . Kabla hajawa nabii mkubwa tunayemjua baadaye, Biblia inatuonyesha Samweli akiwa katika mchakato wa kukua, kujifunza na kupata kibali mbele za Mungu na wanadamu. Kupitia maisha yake tunajifunza kwamba Mungu hafanyi kila kitu kwa siku moja. Mara nyingi hutumia hatua ndogo za kila siku kujenga tabia, imani na uwezo...
Mungu Bado Anaandika Sura za Hadithi ya Maisha Yako 08.08.2026 8:42
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo tunaendelea na wimbo wa Hana kupitia 1 Samweli 2:6–8 . Hana anaposema kwamba Bwana hushusha na kuinua, hufukarisha na kutajirisha, hazungumzi kuhusu Mungu ambaye amesikia habari zake tu. Anazungumza kuhusu Mungu ambaye amemwona akibadilisha maisha yake mwenyewe. Mwanamke aliyekuwa akilia kila mwaka huko Shilo sasa amekuwa ushuhuda kwamba hali ya leo si lazima iwe mwis...
Mungu Hupima Moyo Wako na Sio Mafanikio Yako! 07.08.2026 9:42
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo tunaendelea na wimbo wa Hana kupitia 1 Samweli 2:3 . Baada ya Mungu kubadilisha maisha yake, Hana angeweza kutumia ushindi wake kuwajibu wale waliokuwa wamemdharau. Badala yake, anatukumbusha kwamba tusiseme kwa majivuno kwa sababu Mungu anajua yote na ndiye anayepima matendo ya mwanadamu . Kupitia maisha yake tunajifunza kutowadharau wengine kwa sababu ya hali wanayo...
Usiishie Kupokea Baraka, Mjue Mtoa Baraka! 06.08.2026 10:08
Leo kwenye Neno la Leo Leo tunaanza wimbo wa Hana kupitia 1 Samweli 2:1–2 . Baada ya kusubiri kwa uvumilivu, kupokea muujiza na kumrudishia Mungu Samweli, Hana anafanya jambo kubwa zaidi: anamwabudu Mungu. Cha kushangaza ni kwamba wimbo wake hauzungumzi sana kuhusu mtoto aliyempata bali kuhusu ukuu, utakatifu na uaminifu wa Mungu. Kupitia simulizi hii tunajifunza kwamba lengo la mwisho la baraka s...
Subiri kwa Amani, Kisha Mpe Mungu Utukufu! 05.08.2026 18:20
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo tunahitimisha simulizi ya Hana kupitia 1 Samweli 1:27–28 . Baada ya kusubiri kwa imani na kupokea amani kabla ya jibu, Hana anashuhudia uaminifu wa Mungu na anarudi mbele zake kutimiza ahadi yake. Hakuliona jibu la maombi yake kama mafanikio yake binafsi bali kama zawadi kutoka kwa Mungu, hivyo akamrudishia Mungu kile alichokuwa amempa. Kupitia simulizi hii tunajifunz...
Wakati wa Mungu! 04.08.2026 17:26
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo tunaendelea na simulizi ya Hana kupitia 1 Samweli 1:20 . Baada ya kipindi kirefu cha kusubiri, machozi na maombi, wakati wa Mungu ulifika. Hana akapata mtoto wa kiume aliyemwita Samweli, akisema, “Kwa sababu nilimwomba kwa Bwana.” Kupitia simulizi hii tunajifunza kwamba Mungu hachelewi wala hasahau ahadi zake. Anapokuwa kimya, mara nyingi huwa anaandaa jambo kubwa zai...
Mungu Hukupa Amani Kwanza Kabla ya Majibu! 03.08.2026 14:15
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo tunaendelea na simulizi ya Hana kupitia 1 Samweli 1:17 . Baada ya kumimina moyo wake mbele za Mungu, Hana anapokea maneno ya kuhani Eli: “Nenda kwa amani.” Cha kushangaza ni kwamba hali yake ilikuwa bado haijabadilika, lakini moyo wake ulikuwa umebadilika. Kupitia simulizi hii tunajifunza kwamba Mungu mara nyingi hutupa amani kabla ya kutupa jibu la maombi yetu. Tunap...
Maombi Yanaweza Kubadili Historia. 02.08.2026 13:46
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo tunaendelea na simulizi ya Hana kupitia 1 Samweli 1:10–11 . Akiwa na uchungu mkubwa moyoni, Hana hakukata tamaa wala hakulipiza kisasi kwa waliomdhihaki. Badala yake, alimimina moyo wake mbele za Mungu kwa maombi ya dhati na akaweka nadhiri ya kumrudishia Mungu kile ambacho angekipokea. Kupitia simulizi hii tunajifunza kwamba Mungu husikia maombi yanayotoka katika moy...
Ni Mungu Pekee! 01.08.2026 10:23
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo tunaanza simulizi ya Hana kupitia 1 Samweli 1:1–8 . Hana alikuwa akipendwa sana na Elkana, lakini bado moyo wake ulikuwa umebeba maumivu ambayo hakuna mwanadamu angeweza kuyaponya. Kupitia simulizi hii tunajifunza kwamba kuna mahitaji ya ndani ambayo hayawezi kutimizwa na upendo wa watu, mafanikio au mali, bali na Mungu pekee. Je, tunampelekea Mungu kilio cha mioyo ye...
Safari ya Ruth! Kutoka Machozi Hadi Ukoo wa Mfalme! 31.07.2026 18:28
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo tunahitimisha kitabu cha Ruthu kupitia Ruthu 4:16–22 . Naomi, ambaye aliwahi kurudi Bethlehemu akiwa amevunjika moyo na kujiona hana tumaini, sasa amembeba Obedi mikononi mwake. Mungu alikuwa amegeuza maombolezo yake kuwa furaha na kuandika historia mpya ambayo haikuishia kwake pekee. Kupitia Obedi alizaliwa Yese, akazaliwa Mfalme Daudi na hatimaye Yesu Kristo, Mwokoz...
Vipi Kama Utapoteza Kila Ulichonacho? 30.07.2026 21:55
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo tunaendelea na simulizi ya Ruthu kupitia Ruthu 4:15 . Wanawake wa Bethlehemu wanamwambia Naomi kwamba Mungu amemletea mtoto ambaye atamrejeshea uhai na kumtunza katika uzee wake. Kupitia Ruthu, Mungu hakurejesha tu kile ambacho Naomi alikuwa amepoteza, bali alimpa tumaini jipya, furaha mpya na sababu mpya ya kuishi. Kupitia simulizi hii tunajifunza kwamba urejesho wa...
Inakuwaje Tunapohisi Mungu Ametusahau Kabisa? 29.07.2026 18:34
Leo tunaendelea na simulizi ya Ruthu kupitia Ruthu 4:14 . Wanawake wa Bethlehemu wanamsifu Mungu kwa sababu hakumwacha Naomi bila mkombozi. Yule aliyewahi kufikiri kwamba Mungu amemwacha sasa anaona kwa macho yake jinsi Bwana alivyokuwa akitimiza ahadi zake hatua kwa hatua. Kupitia simulizi hii tunajifunza kwamba ukimya wa Mungu si ishara ya kutusahau. Kwa wakati wake mkamilifu, hubadilisha majonz...
Mungu Hasahau Ahadi Zake! 28.07.2026 16:43
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo tunaelekea katika kilele cha simulizi ya Ruthu kupitia Ruthu 4:13 . Baada ya safari ndefu ya maumivu, kusubiri na uaminifu, Mungu anatimiza ahadi zake kwa kumjalia Ruthu ndoa, familia na mtoto wa kiume. Kupitia simulizi hii tunajifunza kwamba Mungu hachelewi wala hawahi. Anapotimiza makusudi yake, hufanya zaidi ya yale tuliyokuwa tunatarajia na hubadilisha kipindi cha...
Unaweza Kufanikiwa Bila Njia za Mkato 27.07.2026 20:53
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo tunaendelea na simulizi ya Ruthu kupitia Ruthu 3:18 . Naomi anamwambia Ruthu asubiri kwa utulivu, kwa sababu Boazi hatapumzika mpaka amalize jambo hilo kwa njia iliyo sahihi. Ingawa alikuwa na nia njema ya kumkomboa Ruthu, Boazi hakuchagua njia za mkato wala hakupuuza utaratibu uliowekwa. Kupitia simulizi hii tunajifunza kwamba mafanikio ya kudumu hayajengwi kwa harak...
Tulia, Muache Mungu Atende! 26.07.2026 10:59
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo tunaendelea na simulizi ya Ruthu kupitia Ruthu 3:9–13 . Ruthu alifanya sehemu yake kwa utii, na Boazi akathibitisha nia yake ya kumkomboa. Hata hivyo, kulikuwa bado na jambo moja lililopaswa kutatuliwa kabla ya mpango huo kutimia. Badala ya kukimbilia kutatua kila kitu kwa nguvu zao wenyewe, Ruthu na Boazi walichagua kuheshimu utaratibu na kusubiri wakati wa Mungu. Ku...
Utiifu wa Ruthu na Siri ya Pumziko 25.07.2026 15:31
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo tunaendelea na simulizi ya Ruthu kupitia Ruthu 3:1–5 . Naomi anamweleza Ruthu kwamba wakati umefika wa kutafuta pumziko , yaani maisha yenye usalama, ulinzi na mustakabali ambao Mungu alikuwa amemwandalia. Badala ya kutegemea hekima yake mwenyewe, Ruthu alichagua kutii kila alichoelekezwa na Naomi. Kupitia simulizi hii tunajifunza kwamba pumziko la kweli halitokani na...
Similar podcasts
Replaio is not a podcast publisher; show names, artwork and audio belong to their authors and are distributed through public RSS feeds.