Neno la Leo 255

Neno la Leo

Hii ndiyo siku aliyoifanya Bwana (Zaburi 118:24). Anza siku mpya ya Yesu kwa kusiliza na kutafakari nasi “Neno la Leo” kila siku kwa lugha ya Kiswahili.

Besuch unbedingt die Website des Podcasts und unterstütze die Macher: rss.com

Autor

Neno la Leo 255

Kategorie

Religion

Podcast-Website

rss.com

Neueste Folge

22. Okt 2026

Wo hören?

Podcasts in der App Replaio Radio Bald verfügbar

Podcasts kommen bald in die App. Installiere sie jetzt und erlebe als Erster einen ganz neuen Blick auf Podcasts

Bei Google Play herunterladen Kostenlos installieren Android fast 10 Mio. Downloads · Bewertung 4,8 iOS bald

Folgen

Hata Katika Migogoro, Upendo Unaweza Kubaki! 22.10.2026

🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 2 Samweli 18:5 tunaendelea na simulizi ya Daudi na mwanawe Absalomu wakati vita kati ya majeshi yao vinapoanza. Kabla jeshi la Daudi halijaondoka kwenda vitani, Daudi anawaagiza makamanda wake jambo la kushangaza: “Kwa ajili yangu, mtendeeni kwa upole kijana Absalomu.” Hebu fikiria! Absalomu ndiye aliyemwasi baba yake, akamfanya akimbie Yerusalemu na sasa anap...

Usiwe Tu Unangoja Msaada, Kuwa Msaada kwa Wengine! 21.10.2026

🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 2 Samweli 17:27–29 tunamkuta Daudi akiwa Mahanaimu baada ya kukimbia Yerusalemu kutokana na uasi wa mwanawe Absalomu. Daudi na watu wake wamechoka, wana njaa na wana kiu. Hawajui vita hii itaishaje. Lakini katika kipindi hicho kigumu, watu watatu, Shobi, Makiri na Barzilai , wanakuja na msaada. Wanaleta chakula, vyombo, vitanda na mahitaji mengine kwa sababu w...

Mungu Hajakaa Kimya Kama Unavyofikiri! 20.10.2026

🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 2 Samweli 17:14 tunaendelea na simulizi ya Daudi na mwanawe Absalomu. Absalomu anatafuta ushauri wa namna ya kumshinda baba yake. Ahithofeli anatoa mpango wa kumshambulia Daudi haraka lakini Hushai, ambaye alikuwa mwaminifu kwa Daudi, anatoa ushauri tofauti. Hatimaye Absalomu anaukubali ushauri wa Hushai. Biblia inatuonyesha kwamba Bwana alikuwa amekusudia kuu...

Unaweza Kumjibu, Lakini Je, Ni Lazima? 19.10.2026

🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 2 Samweli 16:5–12 tunaendelea na simulizi ya Mfalme Daudi akiwa katika safari ya kukimbia Yerusalemu baada ya uasi wa mwanawe Absalomu. Daudi tayari anapitia kipindi kigumu. Ameondoka kwenye kiti chake cha enzi na mwanawe mwenyewe amemwasi. Lakini kana kwamba hayo hayatoshi, anakutana na Shimei ambaye anaanza kumtukana, kumlaumu na kumrushia mawe. Mmoja wa wat...

Imani ya Kweli Haitegemei Jibu Unalotaka! 18.10.2026

🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 2 Samweli 15:25–26 tunaendelea na simulizi ya Mfalme Daudi akiwa katika safari ya kukimbia Yerusalemu baada ya uasi wa mwanawe Absalomu. Katika safari hiyo, makuhani wanakuja wakiwa wamebeba Sanduku la Agano. Lakini Daudi anawaambia walirudishe Yerusalemu. Kisha anasema maneno yenye uzito mkubwa: “Kama nikipata kibali machoni pa Bwana, atanirudisha tena.” Laki...

Si Kila Anayekufuata Wakati wa Furaha Atasimama Nawe Wakati wa Shida! 17.10.2026

🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 2 Samweli 15:19–21 tunaendelea na simulizi ya Daudi akiwa katika safari ya kukimbia Yerusalemu baada ya mwanawe Absalomu kuanza kuuchukua ufalme. Katika hali hii ya kutokuwa na uhakika, Daudi anakutana na Itai, mtu kutoka Gathi. Daudi anamwambia arudi badala ya kujiingiza katika matatizo yake. Lakini jibu la Itai linashangaza: “Popote atakapokuwa bwana wangu m...

Mafanikio Hayamaanishi Mwisho wa Changamoto! 16.10.2026

🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 2 Samweli 15:13–14 tunamkuta Mfalme Daudi katika hali ambayo huenda hakuwahi kufikiria angeipitia tena. Miaka mingi iliyopita alikuwa akikimbia kutoka kwa Sauli. Lakini sasa Daudi ni mfalme. Ana mamlaka, jeshi na ufalme. Hata hivyo, anapokea habari kwamba mioyo ya watu wa Israeli imeelekea kwa Absalomu, mwanawe mwenyewe. Na ghafla, mtu aliyemshinda Goliathi, a...

Tatizo Unalolipuuza Leo Linaweza Kukugharimu Kesho! 15.10.2026

🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 2 Samweli 15:10–12 tunaendelea na simulizi ya Absalomu, mwana wa Mfalme Daudi. Jana tulimwona akijenga ushawishi na kuiba mioyo ya watu wa Israeli. Leo mambo yamefika mbali zaidi. Absalomu anatuma wajumbe kwa siri katika makabila ya Israeli na kupanga kutangazwa kuwa mfalme huko Hebroni. Biblia inasema: “Fitina ikawa na nguvu, maana watu waliokuwa pamoja na Ab...

Usiishi Kwa Kutafuta Approval ya Watu! 14.10.2026

🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 2 Samweli 15:1–6 tunaendelea na simulizi ya Absalomu, mwana wa Mfalme Daudi. Baada ya kurudishwa Yerusalemu na hatimaye kukutana na baba yake, tunamwona Absalomu akianza kujenga ushawishi wake miongoni mwa watu wa Israeli. Anasimama kwenye lango la mji, anawasikiliza watu wanaokuja kutafuta haki na kuwaonyesha kwamba yeye angeweza kuwa kiongozi bora zaidi. Ana...

Si Kila “Tuko Sawa” Inamaanisha Tuko Sawa! 13.10.2026

🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 2 Samweli 14:32–33 tunamwona Absalomu hatimaye akikutana na baba yake, Mfalme Daudi, baada ya miaka mingi ya utengano. Absalomu anainama mbele ya baba yake na Daudi anambusu. Kwa macho ya nje, unaweza kusema, “Hatimaye wamepatana!” Lakini tunapoendelea kusoma simulizi hii, tunagundua kwamba matatizo ya ndani hayakuwa yamekwisha. Baadaye Absalomu anajaribu hata...

Sio Kila Ukimya Ni Amani! 12.10.2026

🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 2 Samweli 14:28 tunaendelea na simulizi ya Daudi na mwanawe Absalomu. Biblia inatuambia kwamba Absalomu aliishi Yerusalemu kwa miaka miwili bila kuuona uso wa baba yake. Miaka miwili. Mji mmoja. Baba na mwana. Lakini hakuna mazungumzo. Na hapa tunajifunza kwamba si kila ukimya ni amani. Wakati mwingine hatugombani na watu si kwa sababu tumepatana bali kwa saba...

Si Kila Anayerudi Amerudishiwa Nafasi Moyoni! 11.10.2026

🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 2 Samweli 14:21–24 tunaendelea na simulizi ya Daudi na mwanawe Absalomu. Baada ya miaka ya utengano na mipango ya Yoabu, hatimaye Daudi anakubali Absalomu arudi Yerusalemu. Kwa juu juu, hizi zinaonekana kuwa habari njema. Mwana anarudi nyumbani. Lakini kuna jambo la kushangaza. Daudi anasema: “Na ageukie nyumbani kwake wala asiuone uso wangu.” Kwa hiyo Absalom...

Si Kila Tatizo Jawabu Lake Ni Ukimya! 10.10.2026

🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 2 Samweli 14:1–3 tunaendelea na simulizi ya familia ya Daudi ambayo imepitia maumivu, ukatili, kisasi na sasa utengano. Baada ya Absalomu kumuua Amnoni, anakimbia na kuishi mbali na familia yake. Miaka inapita. Daudi anamkumbuka mwanawe. Lakini bado hakuna mazungumzo ya kweli yanayoonekana kati yao. Ndipo Yoabu anatambua hali ya moyo wa mfalme na kupanga njia...

Kisasi Hakiponyi Jeraha! 09.10.2026

🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 2 Samweli 13:28–29 tunaendelea na simulizi ya familia ya Daudi, ambako maumivu ambayo hayajashughulikiwa sasa yanazaa maumivu mengine. Jana tulimwona Absalomu akiwa amebeba hasira na chuki dhidi ya Amnoni baada ya kile alichomfanyia dada yake Tamari. Leo tunagundua jambo muhimu: Miaka miwili imepita, lakini hasira ya Absalomu haijaisha. Kwa nje alikuwa kimya....

Hatari ya Ukimya! 08.10.2026

🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 2 Samweli 13:21–22 tunaendelea na simulizi ngumu ya familia ya Daudi. Jana tulimwona Tamari akiwa amevunjika baada ya kile Amnoni alichomfanyia. Leo tunaona kile kinachotokea baada ya familia kujua. Mfalme Daudi anaposikia habari hiyo anahuzunika sana . Anakereka na kukasirika kwa kile kilichotokea. Lakini kuna jambo ambalo simulizi linatuacha tukijiuliza: Baa...

Usipuuze Maumivu ya Aliyejeruhiwa! 07.10.2026

🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 2 Samweli 13:19–20 tunabaki katika simulizi ngumu ya Tamari. Jana tuliona ukatili ambao Amnoni alimfanyia. Leo Biblia haitukimbizi haraka kwenda kwenye tukio jingine. Inatuonyesha Tamari baada ya tukio. Anararua vazi lake. Anaweka majivu kichwani. Anaweka mkono kichwani na anaondoka akilia. Biblia haitufichi maumivu yake. Na labda nasi hatupaswi kuyakimbia. Wa...

Upendo wa Kweli Huheshimu Mipaka! 06.10.2026

🎙️ Leo katika Neno la Leo tunatafakari 2 Samweli 13:10–14 , sehemu nzito na yenye maumivu katika simulizi la familia ya Daudi. Amnoni anapokuwa peke yake na Tamari anajaribu kumlazimisha kutimiza tamaa yake. Tamari anakataa wazi. Anasema, “Usifanye jambo hili.” Lakini Amnoni hasikilizi. Anatumia nguvu zake na kumdhuru. Hapa Biblia inatuweka mbele ya ukweli ambao hatupaswi kuuficha kwa lugha nyepes...

Usilishe Tamaa Isiyofaa Moyoni 05.10.2026

🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 2 Samweli 13:1–2 tunaingia katika sehemu ngumu na yenye huzuni katika familia ya Daudi. Tunamkuta Amnoni akianza kuwa na tamaa isiyofaa kwa Tamari, dada yake wa kambo. Lakini kuna jambo muhimu ambalo maandiko yanatuonyesha kabla hata hatujafika kwenye kile kitakachotokea baadaye. Amnoni anaendelea kuibeba na kuilisha tamaa hiyo moyoni mpaka inamtesa. Na hapa t...

Mungu Bado Anaweza Kuandika Sura Mpya! 04.10.2026

🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 2 Samweli 12:24–25 tunafika katika sehemu tofauti kabisa ya simulizi la Daudi. Tumemwona akikosea vibaya. Tumemwona akikubali dhambi yake. Tumemwona akisamehewa lakini akikabiliana na consequences. Tumemwona akiomba. Tumemwona akilia. Na jana tulimwona akiinuka tena. Leo Biblia inatuonyesha kwamba hadithi haikuishia pale. Daudi anamfariji Bathsheba. Baadaye wa...

Baada ya Siku Ngumu, Unaweza Kuinuka Tena 03.10.2026

🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 2 Samweli 12:20 tunakutana na Daudi baada ya kupokea jibu ambalo hakulitaka. Jana tulimwona akiwa chini, akifunga na kumwomba Mungu kwa ajili ya mtoto wake. Leo habari inafika: Mtoto amekufa. Watumishi wa Daudi wanaogopa hata kumwambia. Wanafikiri kama alikuwa katika hali ile mtoto akiwa hai, atakuwaje akigundua kwamba amekufa? Lakini Daudi anaposikia habari h...

Omba Hata Kama Hujui Mungu Atajibu Vipi! 02.10.2026

🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 2 Samweli 12:16–17 tunamwona Daudi katika sehemu tofauti kabisa na jana. Jana alisimama mbele ya Nathani na kukubali: “Nimemkosea Bwana.” Leo yuko chini mbele za Mungu akiomba. Mtoto wake anaumwa sana. Daudi anafunga, anaingia ndani na kulala chini usiku kucha akimtafuta Mungu. Na hapa kuna jambo la kuvutia. Daudi tayari amesikia kile Nathani alichosema. Hajui...

Ukikosea, Usijifiche. Rudi kwa Mungu! 01.10.2026

🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 2 Samweli 12:13–14 tunakutana na moja ya moments nzito zaidi katika maisha ya Daudi. Nabii Nathani amesimama mbele yake na kumwambia wazi: “Wewe ndiye mtu huyo.” Daudi sasa hana mahali pa kujificha. Angeweza kujitetea. Angeweza kutoa sababu. Angeweza kutumia mamlaka yake kama mfalme kumyamazisha Nathani. Lakini Daudi anasema: “Nimemkosea Bwana.” Hakuna excuse....

Maliza Vizuri! 30.09.2026

🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 1 Samweli 30:23–26 na 31:1–4 tunafunga mwezi wetu na wakati huohuo tunafika mwisho wa safari yetu kupitia kitabu cha 1 Samweli . Na Biblia inatuacha na picha mbili tofauti sana: Daudi na Sauli. Daudi anatoka katika kipindi kigumu sana kule Ziklagi. Ameona mji wake ukiteketea. Amelia mpaka hana nguvu. Watu wake wametaka kumpiga mawe. Lakini Daudi akajitia nguvu...

Mungu Anaweza Kukurejeshea Ulichofikiri Kimepotea! 29.09.2026

🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 1 Samweli 30:8, 18–19 tunaendelea na Daudi baada ya moja ya siku ngumu zaidi katika maisha yake. Jana tulimwacha Ziklagi ikiwa imechomwa moto. Familia zimechukuliwa mateka. Watu wake wamevunjika moyo kiasi cha kutaka kumpiga mawe. Daudi akalia mpaka hakuwa na nguvu tena za kulia. Lakini Biblia ikasema: “Daudi akajitia nguvu katika Bwana Mungu wake.” Leo tunaon...

Unaweza Kulia na Bado Ukawa na Imani! 28.09.2026

🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 1 Samweli 30:3–6 tunakutana na moja ya siku nzito zaidi katika maisha ya Daudi. Daudi na watu wake wanarudi Ziklagi wakitarajia kurudi nyumbani. Lakini wanapofika, wanakuta mji umechomwa moto na familia zao zimechukuliwa mateka. Biblia inasema: “Daudi na watu waliokuwa pamoja naye wakapaza sauti zao wakalia hata walipokuwa hawana nguvu tena za kulia.” Hawa ni...

Höre den Podcast Neno la Leo in Replaio

Radio und Podcasts in einer App - kostenlos und ohne Anmeldung. Installiere sie noch heute und verpasse den Start nicht

Bei Google Play herunterladen

Replaio ist kein Herausgeber von Podcasts; die Namen der Sendungen, Cover und Audioinhalte gehören ihren Autoren und werden über öffentliche RSS-Feeds verbreitet