Neno la Leo 255
Neno la Leo
Hii ndiyo siku aliyoifanya Bwana (Zaburi 118:24). Anza siku mpya ya Yesu kwa kusiliza na kutafakari nasi “Neno la Leo” kila siku kwa lugha ya Kiswahili.
Be sure to visit the podcast's website and support the creator: rss.com
Where to listen?
Podcasts in the app Replaio Radio Coming soonPodcasts are coming to the app soon. Install now and be the first to see a whole new take on podcasts
Episodes
Unaweza Kulia na Bado Ukawa na Imani! 28.09.2026 13:10
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 1 Samweli 30:3–6 tunakutana na moja ya siku nzito zaidi katika maisha ya Daudi. Daudi na watu wake wanarudi Ziklagi wakitarajia kurudi nyumbani. Lakini wanapofika, wanakuta mji umechomwa moto na familia zao zimechukuliwa mateka. Biblia inasema: “Daudi na watu waliokuwa pamoja naye wakapaza sauti zao wakalia hata walipokuwa hawana nguvu tena za kulia.” Hawa ni...
Usifanye Maamuzi Makubwa Ukiwa Umechoka na Kuogopa! 27.09.2026 21:43
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 1 Samweli 27:1 tunakutana na Daudi katika hali ambayo huenda wengi wetu tunaifahamu. Jana alikuwa amesimama imara katika imani. Alikuwa na nafasi nyingine ya kumuua Sauli lakini akakataa. Alikuwa tayari kumwachia Mungu matokeo. Lakini leo tunamsikia Daudi akisema moyoni mwake: “Siku moja nitaangamia kwa mkono wa Sauli.” Ngoja kidogo. Huyu si Daudi aliyemshinda...
Usijilipizie Kisasi Hata Ukipewa Nafasi 26.09.2026 8:35
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 1 Samweli 26:9–11 tunamwona Daudi akikabiliwa tena na mtihani ambao tayari aliwahi kuupita. Mara ya kwanza Sauli aliingia katika pango ambamo Daudi alikuwa amejificha. Daudi alikuwa na nafasi ya kumuua lakini akakataa. Sasa inatokea tena. Daudi na Abishai wanaingia kambini usiku na kumkuta Sauli amelala. Mkuki wake uko karibu na kichwa chake. Abishai anaangali...
Si Kila Anayekuzuia Ni Adui Yako! 25.09.2026 16:33
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 1 Samweli 25:32–33 tunakutana na jambo la kushangaza kuhusu Daudi. Jana tulimwona akikataa kulipiza kisasi kwa Sauli. Lakini leo Daudi mwenyewe anakaribia kufanya kile alichokataa kufanya jana. Nabali amemdharau na Daudi amekasirika. Anaondoka akiwa tayari kulipiza kisasi. Ndipo Abigaili anapoingia katika simulizi. Anamfuata Daudi na kuzungumza naye kwa hekima...
Usiruhusu Aliyekuumiza Abadilishe Wewe Ni Nani! 24.09.2026 19:15
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Kupitia 1 Samweli 24:12 tunaendelea na Daudi baada ya kukataa kumuua Sauli pangoni. Daudi anatoka nje na kumwonyesha Sauli kipande cha vazi lake. Ujumbe ni wazi: “Nilikuwa na nafasi ya kukuua, lakini sikufanya hivyo.” Kisha anasema, “Bwana na ahukumu kati yangu na wewe… lakini mkono wangu hautakuwa juu yako.” Daudi hakujifanya kwamba Sauli hajamkosea. Sauli alikuwa amemfa...
Si Kila Mlango Uliofunguka Ni Mlango wa Mungu! 23.09.2026 21:48
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Kupitia 1 Samweli 24:4–6 tunamwona Daudi akikabiliwa na nafasi ambayo kwa macho ya kibinadamu inaonekana kama jibu la maombi yake. Sauli amekuwa akimtafuta ili kumuua. Lakini sasa, bila kujua, Sauli anaingia katika pango lilelile ambamo Daudi na watu wake wamejificha. Watu wa Daudi wanaona jambo moja tu: “Hii ndiyo nafasi yako!” Adui yako yuko mbele yako. Hakuna anayekuzu...
Kuwa Mtu Anayeimarisha Imani ya Wengine 22.09.2026 18:15
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 1 Samweli 23:16 tunakutana tena na Yonathani. Daudi bado anakimbia. Sauli bado anataka kumuua na mazingira yake bado hayajabadilika. Lakini Yonathani anamtafuta Daudi. Na Biblia haisemi tu kwamba alikuja kumtembelea au kumfariji. Inasema jambo zuri sana: “Akamwimarisha mkono wake katika Mungu.” Yonathani hakuondoa Sauli. Hakutatua tatizo la Daudi. Hakumwahidi...
Usifikiri Mungu Amekuacha Kwa Sababu Tatizo Bado Lipo 21.09.2026 11:17
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 1 Samweli 23:14 tunamkuta Daudi bado anakimbia. Sauli hajakata tamaa. Maandiko yanasema alikuwa akimtafuta Daudi kila siku . Lakini katikati ya simulizi hiyo kuna maneno machache yenye ujumbe mkubwa sana: “Lakini Mungu hakumtia mikononi mwake.” Angalia jambo hilo. Mungu hakumwondoa Sauli mara moja. Hakumaliza tatizo lote siku hiyo. Daudi bado alikuwa jangwani....
Muulize Mungu Kabla ya Kuchukua Hatua! 20.09.2026 17:44
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 1 Samweli 23:2 tunamwona Daudi akikabiliwa na uamuzi mwingine muhimu. Anaambiwa kwamba Wafilisti wanashambulia Keila na kuiba mazao yao. Daudi alikuwa na sababu nyingi za kujiamini. Huyu ndiye aliyemshinda Goliathi. Ana uzoefu wa vita. Sasa ana watu wanaomfuata. Angeweza kusikia taarifa hiyo na kusema, “Hili nalijua. Twendeni kupigana.” Lakini jambo la kwanza...
Usihitimishe Hadithi Yako Ukiwa Pangoni! 19.09.2026 12:52
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 1 Samweli 22:1–2 tunamkuta Daudi mahali ambapo huenda hakuwahi kufikiria angefika: katika pango la Adulamu. Fikiria safari yake. Alipakwa mafuta kuwa mfalme. Akamshinda Goliathi. Wanawake wakaimba jina lake. Akaingia katika nyumba ya mfalme na kila kitu kikaonekana kinaelekea juu. Lakini sasa yuko pangoni. Kwa macho ya kawaida, unaweza kuangalia maisha ya Daud...
Hata Watu wa Imani Huogopa! 18.09.2026 34:42
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 1 Samweli 21:12–13 tunakutana na upande tofauti kabisa wa Daudi. Huyu ndiye Daudi aliyesimama mbele ya Goliathi wakati jeshi lote la Israeli limejaa hofu. Huyu ndiye aliyesema, “Ninakujia kwa jina la Bwana.” Huyu ndiye aliyetangaza, “Vita ni vya Bwana.” Lakini leo Biblia inatuambia kwamba Daudi akaogopa sana. Akiwa anakimbia kutoka kwa Sauli, anafika Gathi na...
Rafiki Yako Akifanikiwa Kuliko Wewe, Bado Utamshangilia? 17.09.2026 35:27
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 1 Samweli 20:17 tunaendelea kuangalia urafiki wa ajabu kati ya Daudi na Yonathani. Maandiko yanatuambia kwamba Yonathani alimpenda Daudi kama alivyoipenda nafsi yake mwenyewe na akamtaka athibitishe tena kiapo chao. Lakini kuna kitu kinachoufanya urafiki huu kuwa wa kipekee zaidi. Yonathani alikuwa mwana wa mfalme. Kwa kawaida angeweza kutarajia kwamba siku mo...
Rafiki wa Kweli Anakutetea Hata Usipokuwepo! 16.09.2026 36:07
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 1 Samweli 19:4–5 tunamwona Yonathani akifanya jambo linalotuonyesha maana nyingine ya urafiki wa kweli. Sauli sasa anataka Daudi auawe. Daudi hayupo kwenye mazungumzo haya lakini Yonathani yupo. Na badala ya kukaa kimya, anamkumbusha baba yake ukweli: Daudi hajamkosea. Anamkumbusha jinsi Daudi alivyohatarisha maisha yake kupigana na Goliathi na jinsi Mungu ali...
Unaweza Kufanikiwa Bila Kumpoteza Mungu Njiani! 15.09.2026 21:32
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 1 Samweli 18:14 tunakutana na maneno machache lakini yenye ujumbe mkubwa sana kuhusu maisha ya Daudi: “Daudi akafanikiwa katika njia zake zote, naye Bwana alikuwa pamoja naye.” Ni rahisi kusimama kwenye sehemu ya kwanza, “Daudi akafanikiwa.” Lakini siri ya maisha yake ipo katika sehemu inayofuata: “Bwana alikuwa pamoja naye.” Mwezi huu tumemfuata Daudi kutoka...
Usiruhusu Wivu Uharibu Moyo Wako! 14.09.2026 35:01
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 1 Samweli 18:7–9 tunaona mabadiliko ya kusikitisha yakianza ndani ya moyo wa Sauli. Baada ya ushindi, wanawake wanaimba wakisema Sauli amewaua maelfu yake na Daudi makumi ya maelfu yake. Sauli anasikia comparison hiyo na kuanzia hapo anaanza kumwangalia Daudi kwa jicho tofauti. Lakini Daudi hajamkosea Sauli. Tatizo ni kwamba mafanikio ya Daudi yameanza kumfany...
Mungu Hutupa Watu wa Kutembea Nasi! 13.09.2026 53:12
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 1 Samweli 18:1–3 tunaanza kuona maisha ya Daudi baada ya ushindi dhidi ya Goliathi. Lakini jambo la kwanza tunalokutana nalo si vita nyingine. Tunakutana na Yonathani . Maandiko yanatuambia kwamba moyo wa Yonathani uliungana na moyo wa Daudi, akampenda kama nafsi yake mwenyewe na wakafanya agano la urafiki. Kwa wakati huu Daudi huenda hajui umuhimu ambao urafi...
Usidharau Kile Mungu Amekiweka Mikononi Mwako! 12.09.2026 44:11
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 1 Samweli 17:49–50 tunafika katika wakati ambao tumekuwa tukiuelekea kwa siku kadhaa. Daudi anaweka mkono katika mfuko wake, anachukua jiwe, analitia katika kombeo na kumpiga Goliathi kwenye paji la uso. Yule mtu aliyekuwa amelitia hofu jeshi zima la Israeli anaanguka. Goliathi alikuwa na upanga, mkuki, deraya na uzoefu mkubwa wa vita. Daudi alikuwa na kombeo...
Fanya Unachoweza, Mungu Atashughulikia Usichoweza! 11.09.2026 23:12
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 1 Samweli 17:47 tunaendelea pale tulipoishia jana. Daudi amemwambia Goliathi, “Ninakujia kwa jina la Bwana.” Sasa anaongeza jambo muhimu zaidi: “Vita ni vya Bwana.” Lakini angalia jambo hili. Baada ya kusema vita ni vya Bwana, Daudi hakukaa chini akisubiri Mungu afanye kila kitu. Bado alikimbia kuelekea kwa Goliathi. Bado alichukua jiwe. Bado alitumia kombeo l...
Kwa Jina la Bwana! 10.09.2026 13:49
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 1 Samweli 17:45 tunafika katika moja ya kauli zenye nguvu zaidi katika simulizi ya Daudi na Goliathi. Goliathi anasimama mbele ya Daudi akiwa na upanga, fumo, mkuki, uzoefu wa vita na mwonekano wa kutisha. Daudi ana fimbo, kombeo na mawe. Kwa macho ya kibinadamu, hakuna ushindani. Lakini Daudi anasema: “Wewe unanijia kwa upanga na fumo na mkuki, bali mimi nina...
Usijaribu Kuwa Mtu Mwingine! 09.09.2026 40:24
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 1 Samweli 17:38–40 tunaendelea na simulizi ya Daudi kuelekea kwa Goliathi. Baada ya Sauli kukubali Daudi aende kupigana, anamvika mavazi yake ya vita, kofia ya shaba, deraya na kumpa upanga. Ni vifaa vizuri kabisa vya vita, lakini Daudi anapojaribu kutembea navyo anatambua jambo muhimu: hajavizoea. Anavivua. Badala yake anachukua fimbo yake, mawe matano laini...
Kumbuka Mungu Alivyokusaidia Zamani! 08.09.2026 20:05
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 1 Samweli 17:34–37 tunagundua siri ya ujasiri ambao Daudi alionyesha jana. Sauli anamwangalia Daudi na kuona kijana asiye na uzoefu wa vita. Goliathi, kwa upande mwingine, amekuwa mtu wa vita tangu ujana wake. Kwa macho ya Sauli, Daudi hana kile kinachohitajika. Lakini Daudi anajua jambo ambalo Sauli halijui. Ana historia na Mungu. Anamweleza jinsi alipokuwa a...
Usingoje Kila Mtu Aamini Ndipo Wewe Uamini! 07.09.2026 16:34
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 1 Samweli 17:32 tunafunga wiki yetu ya kwanza ya Septemba tukiwa tumemfuata Daudi kutoka malishoni mpaka sasa amesimama mbele ya mfalme. Kwa siku nyingi jeshi la Israeli limekuwa likimsikiliza Goliathi akitoa vitisho. Kila anapotokea, hofu inaenea. Wanaume waliofunzwa vita wanaona ukubwa wa tatizo na mioyo yao inakata tamaa. Lakini Daudi, kijana ambaye hata ha...
Usiruhusu Maneno ya Watu Yazuie Kufikia Malengo Yako! 06.09.2026 16:52
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 1 Samweli 17:28–29 tunaendelea na simulizi ya Daudi na Goliathi. Jana tuliona Daudi akiitazama changamoto kwa macho tofauti. Lakini kabla hajafika hata mbele ya Goliathi, anakutana na vita nyingine ambayo huenda hakuitarajia: maneno ya ndugu yake mwenyewe, Eliabu. Eliabu anamsikia Daudi akiuliza kuhusu Goliathi, anakasirika na kuanza kumshutumu. Anahoji sababu...
Usimfanye Goliathi Wako Kuwa Mkubwa Kuliko Mungu 05.09.2026 39:01
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 1 Samweli 17:26 tunaingia katika moja ya simulizi zinazojulikana zaidi katika Biblia, simulizi ya Daudi na Goliathi. Lakini kabla Daudi hajachukua jiwe, kabla hajatumia kombeo na kabla Goliathi hajaanguka, kuna jambo muhimu sana linalotokea: Daudi anaiona hali ileile ambayo kila mtu anaiona lakini anaichukulia kwa mtazamo tofauti. Jeshi lote la Israeli lilimwo...
Mungu Akifungua Mlango, Atakukuta Uko Tayari? 04.09.2026 32:49
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 1 Samweli 16:18 tunaendelea na simulizi ya Daudi. Jana tulimwona akipakwa mafuta lakini bado hakwenda moja kwa moja kuwa mfalme. Leo tunasikia mtu akimwelezea kwa Sauli: Daudi anajua kupiga kinubi, ni shujaa, ana busara katika kusema na zaidi ya yote, Bwana yu pamoja naye. Jambo la kuvutia ni kwamba sifa hizi hazikuanza kujengwa siku ambayo nafasi ya kwenda ik...
Similar podcasts
Replaio is not a podcast publisher; show names, artwork and audio belong to their authors and are distributed through public RSS feeds.