RFI Kiswahili

Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho

Science SW ↓ 24 episodes

Ni Makala yanayoangazia kwa jicho la tatu mazingira halisi ya dunia yalivyo bila kusahau kile ambacho kinachangia kuyaharibu. Utapata kufahamu namna ambavyo mazingira na rasilimali zinavyoharibiwa huku pia teknolojia ikijumuishwa. Hakika mazingira mazuri ya leo ni dunia yako kesho.

Author

RFI Kiswahili

Category

Science

Podcast website

www.rfi.fr

Latest episode

Jul 6, 2026

Where to listen?

Podcasts in the app Replaio Radio Coming soon

Podcasts are coming to the app soon. Install now and be the first to see a whole new take on podcasts

Get it on Google Play Install for free Android 5M+ downloads · 4.8 rating iOS soon

Episodes

Utengenezaji wa mkaa kutoka kwa mmea wa mianzi 06.07.2026

Misitu ni sehemu muhimu katika mapambano ya dunia dhidi ya mabadiliko ya tabianchi, hata hivyo misitu mingi ipo hatarini kutokan ana shughuli za binadamu. Fahamu kuhu mkaa unaotengenezwa kutokana na mmea wa mianzi(Bamboo)

Mkutano wa Innovate4cities: Kuharakisha hatua za kukabili mabadiliko ya tabianchi kwenye miji duniani. 29.06.2026

Mkutano huo ulioandaliwa na Global Covenant of Mayors for Climate and Energy (GCoM kwa ushirikiano na UN-Habitat, ulijadili mada tofauti kama vile sayansi ya tabianchi, sera na namna ya kuangazia mianya iliopo katika elimu, data, ufadhili na utakelezaji zinazolemaza mikakati ya kukabili tabainchi kwenye miji. Katika makala yetu hivi leo, nimezungumza na Bi Maryam Wangeshi , ni msanifu wa majengo l...

Mjadala waibuka kuhusu jinamizi la taka za nguo kwa mazingira 15.06.2026

Kila wiki, mamilioni ya nguo za mitumba hufika katika masoko kama vile Gikomba jijini Nairobi, Kenya, au Kantamanto mjini Accra, Ghana. Takriban asilimia 40 ya bidhaa hizi zinazoagizwa kutoka nje haziwezi kuvaliwa kabisa, na hivyo kuhamishia mzigo wa udhibiti wa taka za nguo kwa jamii. Nguo nyingi zilitotengenezwa kwa kutumia poliesta na nailoni, huziba njia za maji za mijini, huchafua fuo za baha...

Usimamizi endelevu wa taka kwenye mazingira hauwezi kufanikiwa bila mchango wa wakusanyaji taka 15.06.2026

Tunawaangazia wadau muhimu katika sekta ya usimamizi wa takan hapa tunazungumzia wakusanyaji taka, ambao mara nyingi mchango wao hupuuzwa nasa katika meza ya maamuzi kuhusu suala hili la cuhafuzi wa taka.

Kuna haja ya serikali za Afrika kukumbatia mfumo endelevu ya kukabili taka ngumu kwenye mazingira. 01.06.2026

Tatizo la uchafuzi wa mazingira kutokana na taka  ngumu, bado ni changamoto katika miji mingi barani Afrika. Hata hivyo, hivi karibuni, kumekuwa na jitihada kwenye baadhi ya mataifa ambapo sasa nchi zimeanza kuwa na sheria na kanuni za kuhakkisha usimamizi endelevu wa taka, kwa kuwahusisha wazalishaji na waagizaji wa bidhaa.

Kongamano la siku mbili jijini Nairobi latoa wito wa kubadili simulizi kuhusu maeneo ya nyanda za malisho(Rangelands) 25.05.2026

Kwa muda mrefu maeneo ya nyanda za malisho yamekuwa yakitazamwa kama yaliotengwa na yasio na umuhimu, licha ya kuwa na mifumoikolojia muhimu na chanzo cha riziki kwa takriban watu bilioni mbili duniani, Pamoja na kuhifadhi theluthi moja ya hewa ya kaboni duniani. Lakini sasa wadau wa mazingira, watunga sera, watafiti, wataalam na wawakilishi kutoka jamii za wafugaji baranai Afrika sasa wanatoa wit...

Juhudi za kijamii zilivyookoa msitu wa Karura uliokua umegeuka kuwa eneo la uhalifu 21.05.2026

Nairobi ni mwenyeji wa msitu mkubwa wa mvua ulio salama ndani ya mipaka yake: Hifadhi ya Karura yenye ukubwa wa hekari 1,000 ni mapafu muhimu ya mji mkuu wa Kenya, katika kuchuja uchafuzi wa mazingira kwa mamilioni. Ilikuwa ishara ya ukosefu wa usalama, sasa ni mfano mkuu wa kimataifa wa uhifadhi unaoongozwa na jamii haswa shirika la marafiki wa Karura maarufu Friends of Karura. Hata hivyo, msitu...

Nchini Colombia, mkutano wa kwanza wa kimataifa kuhusu mafuta ya visukuku 12.05.2026

Msikilizaji, juma moja lililopita, mawaziri kutoka karibu mataifa 50 duniani walikutana nchini Colombia kwa mkutano wa mazingira uliolenga kujadili mbinu za mataifa kuachana kikamilifu na nishati zinachafua mazingira ikiwemo gesi na mafuta. Mjadala kuhusu mataifa kuachana na matumizi ya nishati chafu zinazochangia ongezeko la joto duniani, umekuwepo katika mikutano tofauti ya kimataifa ya mazingir...

Jamii katika maeneo kame nchini kenya zawezeshwa ili kustahimili athari za mabadiliko ya tabianchi. 27.04.2026

Nchini Kenya, mzozo wa rasilimali katika jamii zinazopatikana katika maeneo kame ni changamoto ya muda mrefu, na kumekuwa na jitihada ya mashirika tofauti kuziwezesha jamii hizo kustahimili changamoto zitokanazo na athari za mabadiliko ya tabianchi.  Kupitia mradi wa IMARA, jamii ya wafugaji sasa wamegeukia ukulima wa aina tofauti ambao baadhi yao unawadsaidia hata kupata chakula ya mifugo wao.

Sera za Mipango miji barani Afrika zinazingatia ustahimilivu wa majanga mijini? 20.04.2026

Mkutano wa pili wa Umoja wa Afrika unaofahamika kama 'Jukwaa la Mijini Afrika (AUF) ulianzishwa kwa nia ya kuwezesha mazungumzo na uratibu wa ukuaji endelevu wa miji na makazi ya watu barani Afrika. Pamoja na Maryam Wangeshi , msanifu wa majengo, tunaangazia matokeo ya mkutano huo na ikiwa mataifa ya Afrika yana mipangilio ilio bora katika kuwezesha miji yetu kustahimili majanga ya kimazingira.

Ukulima wa mianzi katika kutunza mazingira ya mito nchini Kenya. 10.04.2026

Mimea ya mianzi yaani Bamboo ni mojawapo ya mimea kote ulimwenguni inayoweza kupandwa katika mazingira tofauti kama vile sehemu tambarare au chemichemi.   Ukulima  wa mianzi unaboresha mazingira kwa kuzuia mmomonyoko wa udongo, kurejesha rotuba kwa udongo haswaa sehemu zilizo karibu na mito na hata kama kitega uchumi.

Manufaa ya ardhi oevu ya Ondiri kwa jamii ya kikuyu 01.04.2026

Katika awamu ya kwanza tuliangazia uluhimu wa maeneo ya ardhi poevu katika mazingira, ikiwa ni pamoja na kutumika kama makazi ya aina tofauti ya spishi ya viumbe hai lakini pia ni mazalia ya samaki. Sasa ardhioevu ya Ondiri ni nyumbani kwa zaidi ya spishi 90 za ndege, Kwa mfano, tulifanikiwa kumuona ndege aina ya Korongo ambao mara nyingi wao hutoroka katika ardhioevu ambayo mazingira yake yamecha...

Uhifadhi wa kinamasi cha Ondiri mjini Kikuyu, nchini Kenya 24.03.2026

Vijana katika shirika la uhifadhi la Marafiki wa ardhi oevu ya Ondiri, ambayo ni nyumbani kwa viumbe hai na bayoanuai yenye umuhimu katika mazingira. Katika mazingira, maeneo haya yanya faida kama vile,  kufanya kazi kama sponji ya kunyonya hewa ukaa kutoka kwenye anga zaidi ya misitu ya mvua. Hutumika kama makazi ya aina tofauti ya spishi ya viumbe hai lakini pia ni mazalia ya samaki. Ardhi oevu...

Matumizi ya mitego ya wadudu inayotumia sola yaboresha parachichi na mazingira 24.02.2026

Wakulima wa Meru kaskazini mashariki mwa Kenya wanakumbatia matumizi ya mitego ya wadudu inayotumia nishati ya jua ili kukabiliana na false codling moth (FCM), mdudu anayeharibu mazao ya parachichi. Eneo la kaskazi mashariki huzalisha kiwango kikubwa cha parachichi zinazouzwa ulaya na Asia Kupitia teknolojia hii, wakulima  sasa wameanza kupata nafasi katika masoko ya nje....vile vile wamepunguza u...

Jukumu la redio katika kuelimisha kuhusu mazingira na tabianchi 17.02.2026

Dunia inapokabiliwa na mgogoro wa mabadiliko ya tabianchi  na changamoto zingine za kimazingira, je redio imekuwa na mchango gani katika kuhakikisha jamii zinapata taarifa na habari wanazohitaji kufanya maamuzi muhimu kuhusu mazingira yao.

Hatau ya Marekani kujiondo kwenye mikataba ya mazingir na tabianchi na athari zake 15.02.2026

Aliporejea madarakani Januari 20 2025, kwa mara ya pili Trump aliiondoa Marekani katika mkataba wa tabianchi wa Paris wa 2015. Mwaka wa 2025, Washington haikuwatuma maafisa wake wa juu katika mkutano wa tabianchi wa COP30, uliofanyika Belem, Brazil. Na sasa wiki chache zilizopita, utawala wa Trump ulitangaza kuiondoa Marekani katika mashirika 66 ya kimataifa, ikiwemo ile ya UNFCCC.

Awamu ya pili Siku ya Kimataifa ya nishati safi 26 01 2026: Biogesi kama moja ya suluhisho 07.02.2026

    Upatikanaji wa nishati safi ya kupikia katika jamii kwenye vitongoji duni. Tumetembelea mtaa wa Kawangware, jijini Nairobi, kufahamu juhudi ambazo shirika la Umande Trust linafanya katika suala zima la upatikanaji wa nishati safi kwa kuzingatia usafi wa mazingira. 

Siku ya Kimataifa ya nishati safi 26 01 2026: Biogesi kama moja ya suluhisho 27.01.2026

Upatikanaji wa nishati safi ya kupikia katika jamii kwenye vitongoji duni. Tumetembelea mtaa wa Kawangware, jijini Nairobi, kufahamu juhudi ambazo shirika la Umande Trust linafanya katika suala zima la upatikanaji wa nishati safi kwa kuzingatia usafi wa mazingira. 

Mfumo wa sola tembezi wanufaisha wakulima maeneo kame nchini Kenya 22.01.2026

Katika maeneo mengi ya kusini mashariki mwa Kenya, ukame na mvua zisizotabirika zimekuwa changamoto kubwa kwa wakulima. Hata hivyo, katika kijiji cha Gachuriri, Mbeere, teknolojia rahisi ya umwagiliaji  mimea maji kwa kutumia sola tembezi inayotumia nishati ya jua inaanza kubadili kilimo na kurejesha matumaini kwa wakulima wadogo.

Jinsi jamii ya wamasaai wanavyohamia kwenye ufugaji wa samaki baada ya mabadiliko ya tabia nchi 18.01.2026

Jamii ya wamaasai ambayo Kwa miaka mingi inategemea mifugo imekuwa ikipata changamoto haswa wakati wa kiangazi.  Kiangazi uathiri mifugo kwani ukosefu wa lishe unasababisha wanyama kufa. Hata hivyo Jamii hiyo imebuni mbinu mbadala ya kisasa ya ufugaji samaki. Lakini kutokana na joto jingi linaloshuhudia katika eneo la kajiado, tatizo la kuwakuza samaki hao katika vidimbwi inaonekana wazi wazi kwan...

Awamu ya pili: Matukio muhimu ya mazingira na tabianchi mwaka wa 2025 05.01.2026

Katika awamu ya kwanza tuliangazia miaka kumi ya mkataba wa tabianchi wa Paris na ahadi mpya za kitaifa NDCs. Awamu  ya pili na mwisho tunaendelea kuangazia mkutano wa tabianchi COP30 uliofanyika jijini Belem, Brazil, pamoja na mkutano wa saba wa kimataifa wa mazingira UNEA-7 uliofanyika jijini Nairobi kati ya Disemba 8 na 12 ùwaka wa 2025.

Awamu ya kwanza:Matukio muhimu ya mazingira na tabianchi 2025 30.12.2025
Wanaharakati wataka uhifadhi wa msitu wa mvua wa Kongo kupewa kipaumbele 26.12.2025

Misitu ya mvua barani Afrika kimsingi imejikita katika Bonde kubwa la Kongo, msitu wa pili kwa ukubwa duniani wa kitropiki, unaohifadhi wanyamapori wa kipekee kama sokwe, na tembo wa msituni, pamoja na maeneo mengine muhimu kama vile Misitu ya Guinea ya Afrika Magharibi, misitu ya Afromontane Mashariki, na misitu ya pwani kutoka Kenya hadi Msumbiji yenye misitu ya kipekee ya kisiwa cha Madagaska....

Lugha ya kiswahili katika kuimarisha uelewa, uhamasishaji na hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi 19.12.2025

Wakati viongozi wa dunia, wanasayansi na watunga sera wanapokutana katika miji mikuu ya Dunia kujenga hoja kuhusu hatima ya sayari kupitia mikutano ya tabianchi ya Umoja wa Mataifa,  Wataalamu wa lugha,,  walimu pamoja na  wanafunzi waaendeleza  mijadala. Kaulimbiu ukiwa ni namna lugha adimu ya kiswahili inavyotumika katika kupambana na mabadiliko ya tabianchi.

Listen to the Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho podcast in Replaio

Radio and podcasts in one app - free, with no sign-up. Install today and do not miss the launch

Get it on Google Play

Replaio is not a podcast publisher; show names, artwork and audio belong to their authors and are distributed through public RSS feeds.