Pastor Msafiri
Biblia Inasema Usiogope
Mafundisho mbalimbali ya Biblia yaliyobeba ujumbe kwamba USIOGOPE. Namna pekee ya kukua katika imani na kukua katika uhusiano wetu na Mungu ni kuweka woga mbali nasi. Tubaki majasiri tukipiga mbio kuumaliza mwendo tuliowekewa na kuufikia mwisho mwema, tukibarikiwa na kufanyika baraka kwa wengine.
Be sure to visit the podcast's website and support the creator: podcasters.spotify.com
Author
Pastor Msafiri
Category
Podcast website
Latest episode
Dec 2, 2024
Where to listen?
Podcasts in the app Replaio Radio Coming soonPodcasts are coming to the app soon. Install now and be the first to see a whole new take on podcasts
Episodes
Usiogope Kuuliza 02.12.2024 25:19
Lakini hawakulifahamu neno lile, likafichwa kwao wasilitambue; wakaogopa kumwuliza maana yake neno lile. Luka 9:45
Kumtafuta Bwana Kunaondoa Hofu 25.11.2024 18:50
"Nalimtafuta BWANA akanijibu, Akaniponya na hofu zangu zote." Zaburi 34:4
Usiogope Kumwona Bwana 18.11.2024 28:55
Kuna mambo hutavuka usipomwona Bwana; Kuna kiwango cha imani hutafikia usipomwona Bwana. Sikiliza somo hili ujue kwa nini ni mapenzi Yake umwone na kuondoa hofu ya kumwona. Usiogope kumwona Bwana.
Usiogope Zaka 11.11.2024 34:53
Linapokuja suala la matoleo, sadaka na zaka au changizo mbalimbali, wengi huwa hawatoi au wanatoa kidogo kwa sababu ya woga. Unaogopa hela itaisha wakati bado kuna matumizi. Unahofia too much month at the end of the money. Usiogope kutoa. Usiogope zaka.
Usiogope Baraka Ndogo 04.11.2024 13:45
Wengi wetu tuna baraka ndogo lakini tunaogopa kuukubali ukweli huu na hivyo kuzuiwa kuongezeka katika baraka. Nyumba nzima ya Yakobo ilikuwa imebarikiwa lakini baraka ndogo ukilinganisha na Yusufu; taifa zima la Israeli walikuwa wamebarikiwa lakini kwa baraka ndogo ukilinganisha na Musa. Ukishaelewa kwamba una baraka ndogo basi umekaa mahali pa kuanza kuongezeka katika baraka. Usiogope kuwa mwenye...
Usiogope Kubariki 28.10.2024 15:09
Unapokuwa katikati ya watu wasioamini; au uko chini ya bosi asiyeamini, kumbuka kwamba watu hao wanapaswa kuona baraka za Mungu maishani mwao kwa kupitia wewe. Unapaswa kuwa baraka kwao. Usiogope kuwabariki.
Usiogope Jambo Jipya 23.04.2024 18:01
Wakati jambo jipya linatukia au kutendeka, usiogope. Kama wewe ni wa Bwana basi fahamu kwamba yote ni kwa wema. Kama hauko na Bwana basi mrejee Yeye uwe upande wake ndiko kwenye amani.
Usiogope Kukataliwa 11.04.2024 25:17
Usiogope Kukataliwa, kuwa Hodari.
Nanyi Iweni Hodari 01.04.2024 27:04
Biblia inatuonyesha namna ambavyo Bwana Mungu anataka watu wake wawe hodari katika kufanya yale aliyowaamuru wayafanye; hakuna haja ya kuogopa kwa sababu Roho Yake ipo kati ya watu Wake. Kama wewe ni mwaminini basi huna haja ya kuogopa kwa sababu yale aliyosema nao wakati ule bado yanakuhusu wewe hata leo hii kwa sababu kama mwamini bado Roho Mtakatifu yuko ndani yako. Ukiwa hodari kufanya kazi ya...
Kauli ya Mtu Jasiri 06.03.2023 32:29
Mtu asiyeogopa ni jasiri, na mtu jasiri ana kauli tofauti na mtu mwoga. Waoga hukimbia wasipofuatiwa na mtu yeyote bali mwenye haki ni jasiri kama simba. Mwenye haki, haki ipatikanayo kwa imani katika Kristo Yesu, ni mtu jasiri katika Bwana na anapaswa kujua kwamba Bwana anategemea kauli yake iwe tofauti na mwoga asiye haki. Kama wewe ni mwenye haki katika Bwana kwa imani ni vema ukajifunza namna...
Kauli ya Mtu Jasiri TRAILER 04.03.2023 2:00
Mtu asiyeogopa ni jasiri, na mtu jasiri ana kauli tofauti na mtu mwoga. Waoga hukimbia wasipofuatiwa na mtu yeyote bali mwenye haki ni jasiri kama simba. Mwenye haki, haki ipatikanayo kwa imani katika Kristo Yesu, ni mtu jasiri katika Bwana na anapaswa kujua kwamba Bwana anategemea kauli yake iwe tofauti na mwoga asiye haki. Kama wewe ni mwenye haki katika Bwana kwa imani ni vema ukajifunza namna...
Mambo Yanayoathiri Imani 04.03.2023 47:04
Kutoogopa ni suala la imani kwa sababu inakupasa kusimama na maandiko kwa imani kwamba yuko Mungu anayakuzungukia pande zote na tena anayeangalia kwamba ufikie mwisho mwema. Na pia kwa sababu woga ni udhihirisho wa kutoamini au kuwa na imani haba hivyo haikwepeki kwamba mambo yanayoathiri imani yako yanagusa moja kwa moja kuogopa au kutoogopa kwako. Katika episode hii tunaangalia mambo manne yanay...
Usiogope Tetesi za Vita 26.01.2023 17:46
Sasa hivi kuna vita vinapiganwa kati ya Urusi na Ukraine, taifa dhidi ya taifa, na bado chokochoko za vita kusambaa ni kubwa. Huku Afrika vita vya wenyewe kwa wenyewe zimezoeleka. Lakini bado tunafahamu kwamba majaribio ya silaha kali na ripoti za gunduzi mbalimbali za namna za kupigana vita na kuua mamilioni ya watu kwa muda mfupi zinavyotisha wengi. Kuhusu siku hizi za mwisho, Yesu alisema "msio...
Watoto Alionipa Bwana 19.01.2023 15:29
Katika nyakati hizi tulizopo sio kitu kigeni masikioni kusikia mtoto kabakwa au kanajisiwa, kauawa na dada wa kazi au kaibwa. Yaani kesi ni chungu nzima. Mambo ni magumu kiasi kwamba wazazi wanaishi kwa hofu juu ya watoto wao. Kama wewe ni mzazi na unamwamini Mungu Aliye hai katika Kristo Yesu basi huna haja ya kuogopa kwa sababu ya Jina hili la fahari na lenye kutisha. Watoto hao aliokupa Bwana w...
Hao Wamchao Bwana 09.01.2023 17:09
Moja ya jambo litakalokufanya usiogope ni kumcha Bwana. Lakini si tu kutoogopa, Kumcha Bwana kunaleta mambo mengi ya baraka maishani mwako. Lakini hata kumcha Bwana maana yake nini? Haya ndiyo tunayojifunza katika episode hii.
Mambo 7 ya Kutoogopa 02.01.2023 20:31
Biblia Inasema Usiogope; usiogope nini? Yako mengi ambayo watu wanayaogopa lakini Biblia inasema usiyaogope. Katika episode hii tunaangalia mambo 7 ya kutoogopa ili kupiga hatua katika imani.
Huna Hatia 07.03.2022 15:14
Katika maisha ya imani Shetani hupigana vita ili kututoa katika ujasiri tulionao katika Kristo Yesu. Na adui hufanikiwa katika hili pale anapoweza kutujaza dhamiri ya hatia ndani yetu kwamba sisi ni wakosa na hatuna haki mbele za Mungu. Wakristo wengi wanaishi katika dhamiri ya hatia au wataingia kwenye huo mtego hivi karibuni kwa sababu wameshapelekwa kwenye kona ya kuamini kwamba haki yao inatok...
Usione Shaka 28.02.2022 22:02
Mara nyingine tunakuwa na imani ya kuanza kitu au kupokea uponyaji lakini baada ya muda kidogo uponyaji unapeperuka au kile tulichokianza kinakwama. Tunakuwa kama Petro ambaye alianza kutembea juu ya maji halafu akaona upepo mkali akaogopa na kuanza kuzama. Tunaacha kuangalia chanzo cha imani yetu, yaani Kristo Yesu, na kuangalia mazingira. Kumbuka mwenye haki ataishi kwa imani si kwa kuona.
Anguko la Watesi Wako 21.02.2022 26:25
Katika maisha unapokuwa unafanya mapenzi ya Mungu, wale wanaoinuka dhidi yako yaani watesi wako na kwa sababu unafanya mapenzi ya Mungu basi watesi wako wanakuwa kinyume na Mungu. Kama uko katika mapenzi ya Mungu na unakutana na watesi, jipe moyo, maandiko yanasema watesi wako wataanguka.
Usiogope Uchawi part 3 03.01.2022 25:24
Tumepewa mamlaka ya kukanyaga simba na nyoka, naam, mwanasimba na joka tunapaswa kuwaseta kwa miguu. Ukifuatilia hili "joka" ambalo Mkristo umepewa mamlaka ya kulikanyaga utafahamu kwamba ni lile joka, yaani Shetani au Ibilisi kwa jina. Kwa mamlaka uliyonayo siyo tu kwa vibaraka wa shetani bali hata kwa shetani mwenyewe. Ndiyo maana maandiko yanasema mpingeni Shetani naye atawakimbia. Kama baba ya...
Usiogope Uchawi pt. 2 27.12.2021 23:46
Wachawi wote wanatumika chini ya baba yao shetani, yule nyoka wa zamani. Kwa hiyo wao ni kama baba yao yaani nyoka. Kama umeokoka, siyo tu kwamba Mungu anakulinda dhidi ya adui, bali Kristo amekupa mamlaka ya kukanyaga nyoka na ng'e na nguvu zote za adui. Huna haja ya kuogopa...
Usiogope Uchawi 20.12.2021 25:38
Watu wengi na hata Wakristo wameshikwa na hofu kubwa ya uchawi au kulogwa. Yaani inafika mahali maamuzi ya mtu yanakuwa yanategemea sana suala la kulogwa, ingawa yeye ni Mkristo. Unaogopa kuishi mahali kwa sababu kuna wachawi, unaogopa kwenda mahali kwa sababu ya wachawi, wengine mpaka wanaogopa kulala usiku kwa sababu ya wachawi. Sikiliza somo hili upate kujifunza mambo ya msingi ya imani y...
Usiogope, Zinakuja Siku za Kurejeshwa 13.12.2021 30:19
Katika mambo magumu unayopitia na kipindi kigumu ulichokikabili kwa muda sasa, pamoja na mateso yote yanayokusonga, usikate tamaa wala usiogope. Mungu ameahidi siku za kurejeshwa ambapo nuru itarudi usoni mwako na furaha itajaa moyoni. Ingawa ulihenya na kuwa ishara ya laana, au alama ya chukizo na kielelezo cha namna mtu anavyoweza kuporomoka, Bwana ameahidi kuinuliwa kwako mpaka iwe alama ya jin...
Usiogope Kifo 06.12.2021 24:45
Mtu anayemwamini Yesu Kristo, na mafundisho yake, hana haja ya kuogopa kifo. Yesu alikuja kutuweka huru, kwa hiyo sisi tunaoamini siyo watumwa tena. Waebrania 2:14,15 imesema “ Basi kwa kuwa watoto wana nyama na damu, Yeye pia alishiriki katika ubinadamu wao, ili kwa kifo chake, apate kumwangamiza huyo mwenye nguvu za mauti, yaani, Shetani, na kuwaweka huru wale waliokuwa utumwani maisha yao yote...
Utokapo Kwenda Vitani Usiogope 31.05.2021 11:54
Mara unapobidi kukabiliana na upinzani wa aina yeyote ile, mtu au vitu au mazingira, usiogope. Mara nyingine unakabiliana na adui anayeonekana ana uwezo kuliko wewe, ana nguvu kuliko wewe, ana nyenzo kuliko wewe na hata kama maadui ni wengi kuliko wewe, bado usiogope. Kwa sababu upande wako yuko Mungu mtenda maajabu asiyeshindwa. Usiogope unapotoka kukabiliana na upinzani.
Similar podcasts
Replaio is not a podcast publisher; show names, artwork and audio belong to their authors and are distributed through public RSS feeds.