RFI Kiswahili

Siha Njema

Makala inayojadili kwa kina masuala ya afya, tiba na kutambua magonjwa mbalimbali bila ya kusahau namna ya kukabiliana nayo. Watalaam walibobea kwenye sekta ya afya watakujuvya na kukuelimisha juu ya umuhimu wa kuwa na afya bora na si bora afya. Pia utawasikiliza kwa maneno yao watu ambao wameathirika na magonjwa mbalimbali na walikumbwa na nini hadi kufika hapo walipo.

Bezoek zeker de website van de podcast en steun de maker: www.rfi.fr

Auteur

RFI Kiswahili

Categorie

Health

Website van de podcast

www.rfi.fr

Nieuwste aflevering

20 nov. 2026

Waar luisteren?

Podcasts in de app Replaio Radio Binnenkort beschikbaar

Podcasts komen binnenkort naar de app. Installeer nu en zie als eerste een compleet nieuwe kijk op podcasts

Download het op Google Play Gratis installeren Android 10 mln+ downloads · beoordeling 4,7+ iOS binnenkort

Afleveringen

Wagonjwa wa Kisukari nchini DRC wanalazimika kustahimili ugumu mwingi 20.11.2026

Wagonjwa wa Kisukari nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wanapata ugumu wa kupata matibabu na lishe kutokana na usalama mdogo mashariki mwa DRC

Wanawake wanavyotumia idadi na ushikamano wao kustawisha afya jamii 11.11.2026

Wanawake kupitia mikutano ya kijamii,mikutano ya kirafiki nchini Kenya wanahamasisha kuhusu namna ya kuishi maisha yenye afya ,afya ya uzazi na namni wanaweza kuchangia huduma za afya . Nchini Kenya kundi la wanawake maarufu Iron Ladies  kila linapoandaa mikutano yao ya kila baada ya miezi miwili ni lazima kuwa somo kuhusu afya ya uzazi ,usafi kwa kila mwanamke na namna kwa njia moja wanaweza kuch...

Maji ya barafu na kutembea bila viatu inavyotibu mishipa na sonona 03.11.2026

Watu wengi wameanza kukumbatia matibabu yasiyo ya dawa kuyatibu baadhi ya matatizo ya kiafya. Miongoni mwa matatizo hayo ni matatizo ya mishipa,viungo na matatizo ya afya ya akili Dkt Hamisi Kote Ali ni mmoja wa madaktari ambao wanatoa matibabu hayo ambayo yanafahamika kama matibabu ya 'Chiropractic'. Katika makala haya Dkt Hamisi anaelezea faida za kutembea bila viatu ambapo anatumia mfano wake ,...

Unajiandaaje kwa ajili ya dharura za kiafya kutokana na El nino? 30.10.2026

Mamlaka za hewa za kimataifa na za kikanda zimezidi kubashiri El nino ya kuvunja rekodi muda wowote kuelekea mwisho wa mwaka huu hadi mwakani. Msimu huo unahofiwa kusababisha mafuriko,uhaba wa chakula na dharura za kiafya ,swali ni je wananchi wamejiandaje? Dkt Valerie Nyange anafafanua baadhi ya maandalizi yanayohitajika kabla msimu huo kuanza na hata wakati wa msimu huo. Baadhi ya maandalizi hay...

Jinsi matatizo ya uti wa mgongo yanavyotibiwa bila upasuaji au dawa 20.10.2026

Matatizo ya uti wa mgongo kwa muda yamekuwa yakitibiwa kwa upasuaji au dawa kali za maumivu pia wagonjwa kupewa vifaa vya kuwasaidia kutembea,kuketi na kusimama Daktari Hamisi Kote Ali  mwasisi wa Human Garage jijini Nairobi,hata hivyo anasema mwili wenyewe unaweza kujitibu . Katika Human Garage Dkt Hamisi anatumia mazoezi maalum ,lishe na vifaa maalum kuwasaidia wagonjwa wake kukwepa upasuaji ,ma...

Kwa nini afya ya akili ni swala muhimu kwa wagonjwa wanaougua magonjwa sugu 13.10.2026

Shirika la afya duniani ,WHO limesema watu zaidi ya milioni 150 barani Afrika wana hitaji huduma za afya ya akili. Kutokana na idadi hii inayopanda kila wakati ,watalaam wa afya wanasisitiza wagonjwa walio kwenye matibabu ya magonjwa yasiyoambukizwa sharti kufuatiliwa pia kwa matatizo ya afya ya akili ,chini ya mpango wa huduma za afya jumuishi. Wataalam wanasema matibabu ,gharama kubwa na mabadil...

Kifafa cha mimba bado kinasababisha vifo vingi vya akina mama na watoto Afrika 07.10.2026

Kifafa cha mimba hali inayohusishwa na shinikizo kubwa la damu mama anapokuwa mja mzito kuanzia wiki 20 za mimba na inaweza kujitokeza pia pindi mama anapojifungua ,ni hali ya dharura na tishio kubwa kwa akina mama waja wazito Watalaam wanahoji kuwa hatari yake hutokana na kwamba dalili zake wakati mwingi hufanana na dalili za kawaida za mama mja mzito  Ni kutokana na hili mashirika ya kijamii kut...

Wagonjwa wa saratani wanavyochanganya matibabu ya hospitali na mazoezi 01.10.2026

Wagonjwa wengi wa saratani mara nyingi huhisi kulemewa na madhara yanayotokana na matibabu makali ambayo wanabidi kutumia kwa muda mrefu. Kurahisisha  safari hiyo kituo cha  Faraja Cancer Support Trust eneo la Parklands Nairobi kimewapa fursa ya kufanya mazoezi ; na kucheza muziki huku wakiendelea na matibabu hayo.   Wengi ambao wamekuwa wakishiriki mazoezi hayo wanasema miili yao ina uimara zaidi...

Mchakato wa kupatikana chanjo mpya dhidi ya TB kufikia mwaka 2029 22.09.2026

Chanjo mpya za kupambana na ugonjwa wa kifua kikuu au TB zitakuwa tayari kufikia mwaka 2029 Hadi sasa chanjo 16 zimekuwa zikifanyiwa majaribio na ikiwa zitaidhinishwa zitaokoa maisha ya watu zaidi ya milioni saba kufikia 2050 haswa katika mataifa yanayoendelea. Kwa miongo kadhaa chanjo ya pekee ambayo imekuwa ikitumika kuzuia TB ni chanjo ya BCG ambayo mtoto anapewa pindi anapozaliwa. Wanaharakati...

Kwa nini kilimo sharti kuzingatiwa kumaliza njaa barani Afrika 19.09.2026

Ripoti ya mashirika kadhaa ya umoja wa mataifa yameonesha Afrika bado ina watu wengi ambao wanakabiliwa na njaa. Hii ni licha ya Afrika kuwa sehemu inayofanya kilimo . Watalaam wanasema kilimo kimeathirika na athari za mabadiliko ya tabia nchi  kama vile mafuriko,ukame na sasa hivi vijana wengi hawapendi kilimo Hivi basi nini kifanyike kuhakikisha kuwa kuna lishe bora barani Afrika? Dkt Calistus K...

Kisukari inaendelea kuongeza idadi ya wagonjwa wa macho nchini Kenya 09.09.2026

Magonjwa yanoyohitaji matibabu ya muda mrefu ukiwemo kisukari unaendelea kusababisha watu wengi kupata matatizo ya macho au kupoteza uwezo wa kuona

Afrika kukabiliana na usugu wa vimelea vifo vikitarajiwa kuvuka milioni 4 02.09.2026

Kituo cha kuzuia na kudhibiti magonjwa barani Afrika ,Africa CDC kimeonya vifo vinavyohusishwa na usugu wa vimelea vinatarajiwa kuvuka milioni 4 mwaka wa 2050 Mashirika ya kikanda yanasisitiza utekelezwaji wa pamoja wa mikakati ya kukabiliana na usugu wa vimelea ikiwemo afya ya mifugo ,matumizi mazuri ya dawa za antibiotics na dawa za kunyunyuzia mimea kwenye sekta ya kilimo.   Watalaam wa afya wa...

Mapambano dhidi ya Ebola Bundibugyo nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo 28.08.2026

Ebola imekamilisha siku 100 tangu ilipotangazwa na bado bado haijadhibitiwa Shirika la kimataifa la VillageReach miongoni mwa mashirika yaliyoalikwa na utawala wa Kinshasa kusaidia juhudi za kudhibiti mwambao hatari wa Ebola Bundibugyo linazungumzia kuhusu mapambano hayo. Baadhi ya changamoto zinazofanya ugumu mapambano hayo ni ukosefu wa uaminifu kati ya wananchi na serikali ,tamaduni na pia taar...

Kwa nini bima ya afya ya msafiri ni sharti muhimu kwa mataifa ya Afrika 18.08.2026

Umuhimu wa bima ya afya kwa wasafiri ni pamoja na kupunguza gharama kwa taifa mwenyeji haswa wakati huu nchi nyingi hususan za Afrika zinashuhudia ongezeko la milipuko wa magonjwa ya milipuko Sharti hilo pia linatoa fursa kwa nchi kuboresha mifumo ya afya ili kukidhi mahitaji ya wasafiri wanaohitaji huduma za afya kwa nchi wanazozitembelea.

Unaweza kuendelea kunyonyesha hata baada ya kutenganishwa kwa muda na mwanao 11.08.2026

Imani kuwa mama na mtoto wanapotenganishwa inaweza kuathiri ubora wa maziwa ya mama inapotosha. Watalaam wanasisitiza maziwa ya mama hayawezi kuharibika kwenye titi. Aidha kunyonyesha kwa uaminifu kunaweza kukuepusha na saratani na mbinu pia ya kupanga uzazi.

Kwa nini watalaam wanahoji maumivu makali wakati wa hedhi si kawaida 31.07.2026

Maumivu wakati msichana au mwanamke anapokuwa kwenye siku zake za hedhi, yanaweza kuwa ya kawaida ila maumivu haya yanapomfanya kushindwa na shughuli za kawaida si kawaida Dkt Dominic Osiemo anasema maumivu haya makali yanaweza kuwa dalili za baadhi ya changamoto za kiafya kama vile Uvimbe au ugonjwa wa Endometriosis.

Changamoto ya wanaume na wanawake kukosa hamu ya tendo la ndoa 21.07.2026

Raia mmoja wa Kenya amefika kwenye bunge la kitaifa nchini Kenya akitaka swala la wanaume na wanawake kutokuwa na hamu ya tendo la ndoa kuorodheshwa kuwa ulemavu Kwa mujibu wa daktari Dominic Osiemo ,tatizo hilo linachangiwa na maswala kadhaa yakiwemo matumizi ya dawa za kisukari ,shinikizo la damu na msongo wa mawazo.

Visa vya kung'atwa na Nyoka vyaongezeka kaunti ya Turkana Nchini Kenya 21.07.2026

Kaunti ya Turkana inaongoza nchini Kenya kwa visa vya watu kung'atwa na nyoka. Wataalamu wa afya wanasema mabadiliko ya tabianchi, joto kali na changamoto za upatikanaji wa huduma za afya vinaongeza hatari kwa wakazi wa maeneo mengi ya kaunti hiyo,huku shirika la afya duniani WHO likisema visa vya kuumwa na nyoka vinapuuzwa wakati huu karibia watu 32000 wakifariki kila mwaka  kutokana na sumu ya n...

Mashirika ya kiraia Afrika yaanza kampeni dhidi ya madeni ya umma 10.07.2026

Mashirika ya kiraia yanasema nchi za Afrika zinalipa deni na kuachwa  na kiasi kidogo cha pesa kuendesha shughuli muhimu za serikali ,sekta ya afya ikiathirika zaidi Mashirika haya yanataka umoja wa Afrika kuja na jopo ambalo litakuwa linaangazia  maswala yote kuhusu mikopo ili kupunguza dhulma kwa nchi zinazoendelea

Kampeni kuhakikisha vyakula vilivyosindikwa vina maandishi ya kuonya 30.06.2026

Tafiti kadhaa za kiafya zimebainisha magonjwa mengi yasiyoambukizwa yana uhusiano mkubwa na vyakula vilivyosindikwa  na hali ya watu kukosa kuzingatia mazoezi  ya kila mara. Kenya ikiwa taifa la kwanza Afrika Mashariki kupitisha  mwongozo unaotoa maelekezo kuhusu viwango vya  madini ambavyo  vyakula au vinywaji  vinavyouzwa vinafaa kukidhii  au kwa lugha ya kiingereza Kenya Nutrient Profile Model,...

Kwa nini ni muhimu wanaume kuzingatia afya zao haswa afya ya akili 23.06.2026

Mwezi Juni ni mwezi wa kutoa uhamasisho kuhusu afya ya akili miongoni mwa wanaume ,swala la afya ambalo hupuuzwa mno Daktari Dominic Osiemo anasema wanaume wana haki wa kuonesha hisia ,kueleza maumivu  yao na kutaka kuskizwa. Na wanapofanya hivyo wanalinda afya zao za akili. Anaonya wanaume wengi wanakuwa hatarini kwa sababu wanajaribu kudhihirishia jamii kuwa wao ni imara siku zote. Baadhi ya vip...

Shule ya Mali jijini Nairobi inavyowasaidia watoto wenye Austism pamoja na wazazi 16.06.2026

Katika mkakati wa kupunguza unyanyapaa kwa wazazi wanaowalea watoto wenye Autism shule ya Mali inatoa tiba nasaha  na elimu kwa pamoja ikizingatia pia mahitaji ya wazazi wao ambao mara nyingi wanahitaji pia matunzo

Shinikizo kutaka mataifa kuja na sera endelevu na salama za uchukuzi 11.06.2026

Shinikizo zinazidi kutolewa kwa mataifa ya Afrika kukumbatia sera za uchukuzi zilizo salama na endelevu ili kupunguza idadi ya vifo vinavyotokana na barabara na madhara ya ajali za barabara kwa jamii. Katika  kongamano la kujadili mpango huo wa usalama ulio endelevu ,wadau wamesikitika vifo vya barabarani bado vinaripotiwa miongoni mwa watembea miguu na waendesha pikipiki. Katika makala ya Siha Nj...

Majanga yanaweza kusababisha matatizo ya afya ya akili miongoni mwa watoto 06.06.2026

Mataifa ya Afrika yameshuhudia mafuriko katika miaka ya hivi karibuni ,hali ambayo imesababisha wananchi wengi kulazimika kuhama makazi yao Nchini Kenya ,ukanda wa magharibi ,katika eneo la Busia,mafuriko hayo yamevuruga kalenda za wanafunzi wa shule ,watoto wengi wakishindwa kuendelea na shule au kukubaliana na msongamano kwenye shule chache ambazo ziko maeneo salama Hali hii imewasababisha chang...

Mwendelezo wa mlipuko wa Ebola DRC na namna wenyeji wanavyojikinga 30.05.2026

Watu 220 wamefariki kwenye mlipuko wa Ebola unaohusishwa na virusi adimu vya Bundibugyo huku wengine zaidi ya 1000 wakiwa wameambukizwa Mlipuko huu hatari umesababisha baadhi ya mataifa kufunga mipaka yake na kuweka masharti magumu ya tahadhari

Luister naar de podcast Siha Njema in Replaio

Radio en podcasts in één app - gratis en zonder account. Installeer vandaag nog en mis de lancering niet

Download het op Google Play

Replaio is geen uitgever van podcasts; namen van shows, covers en audio zijn eigendom van hun makers en worden verspreid via openbare RSS-feeds