fr

Standard Media

Siasa na Gumzo

Mijadala, uchambuzi na gumzo la kusisimua kuhusu masuala ya kisiasa, kiuchumi na kijamii.

Auteur

Standard Media

Catégorie

History

Site du podcast

www.standardmedia.co.ke

Dernier épisode

25 juil. 2024

Où écouter ?

Les podcasts dans l'appli Replaio Radio Bientôt disponible

Les podcasts arrivent très bientôt dans l'appli. Installe-la dès maintenant et découvre en avant-première une toute nouvelle façon de vivre les podcasts

Télécharger sur Google Play Installe-la gratuitement Android près de 10 M de téléchargements · note de 4,8 iOS bientôt

Épisodes

Kujiunga kwa ODM Na Serikali Kutakomesha Maandamano ya Gen Zs? 25.07.2024

Baada ya Rais William Ruto kuwateua wanasiasa wanne kutoka ODM kujiunga na Baraza la Mawaziri, swali sasa ni hatima ya ODM ni gani? Je, Rais ametatua tatizo lililokuwepo?

Hasla Akosa Usingizi Kufuatia Gharama ya Maisha | Siasa na Gumzo Podcast 17.12.2022

Suala la gharama ya maisha limeendelea kumkosesha Hasla usingizi! Ameamua kutumia mbinu tatu; mbolea ya bei nafuu, serikali na sekta binafsi kuagiza tani elfu miatatu za mbolea na kuagiza mahindi ili kukabili uhaba wa chakula. Atafaulu? Aidha, kuna more goodies kwa mahasla, Rais akipata fedha kutoka Marekani kupiga jeki Hazina ya Hustler Fund. Umesaidika na fedha hizo? Kiwango ulichoomba kimeongez...

Uteuzi wa Makatibu Wazua Tumbojoto, Raila akitaka Waluke Kuachiliwa | Siasa na Gumzo Podcast 05.11.2022

Uteuzi wa makatibu umezua mjadala, wana-Azimio wakilalamika kwamba Rift Valley na Mt. Kenya zimependelewa. Unadhani suala la kimaeneo lilizingatiwa? Aidha, Baba anadai Kinoti anaandamwa na anataka majasusi wa kimataifa kualikwa kushughulikia suala la mauaji ya kiholela. Riggy G naye hataki harufu ya Tinga Kenya Kwanza, Tinga naye anasema wewe kijana wacha kuniota kila saa mimi si rika lako. Unamsh...

Gumzo la GMO; Azimio yamkosoa Hasla | Gumzo la Wiki Podcast 14.10.2022

GMO imezua gumzo, Azimio wakipinga. Kalonzo naye anasema Rais Ruto analenga kuangamiza kilimo cha mimea ya kiasili. Mbali na hayo, unadhani kwamba Kalonzo anatoshea viatu vya Odinga katika upinzani? Baba naye angali anamlaumu Chebukati na mataifa ya kigeni, kwamba yaliingilia uchaguzi wa Kenya! Unasemaje? Si hayo tu, Azimio inasema Ruto amekuwa kiguu na njia, bila kwanza kutimiza ahadi kwa Wakenya...

Gumzo na Siasa Podcast; Manifesto za Ruto na Wajackoyah 02.07.2022

Mgombea urais wa UDA, William Ruto amezindua manifesto yake akiangazia nguzo sita; kupunguza gharama ya maisha, kumaliza uhaba wa walimu, matibabu bila malipo, kujenga nyumba elfu 250 kila mwaka, kukuza biashara na kuimarisha kilimo. Ahadi hizi zinatekeleka? Upande mwingine Wajackoyah ameweka wazi manifesto yake akijumuisha mambo ya kiajabu. Mara atahamisha jiji la Nairobi hadi Isiolo, sijui kufug...

Siasa na Gumzo; Kabogo/Kuria walia, Sakaja atetea digrii 18.06.2022

Nyumba ya Kenya Kwanza imeanza kuwaka moto. Kuria na Kabogo wataka mkutano wa dharura wakimshtumu Gachagua kufuatia madai ya udikteta. Aidha, wanadai wana-UDA wanapendelewa katika kampeni za Kenya Kwanza. Kunani? Gachagua amekuwa mzigo Kenya Kwanza? Anavutia kura au anafukuza? Sakata ya Sakaja kuhusu digrii nayo yamfikia Tinga na Hustler. Kelele zimechacha kuhusu kisomo cha Tinga na PHD ya Hustler...

Gumzo la Wiki; Wabunge wa tumbokrasia; si demokrasia wala uwajibikaji 10.06.2022

Bunge la 12 limevunjwa rasmi baada ya kuhudumu kwa kipindi cha miaka mitano. Je, limetimiza matarajio ya Wakenya ama limekuwa bunge la demokrasia ama utumbokrasia kwa kujali tu donge nono kupitia marupurupu? Kura za maoni nazo zinaendelea kutolewa kuelekea uchaguzi mkuu. Je, ni za kuaminika ama zinatoa taswira ya kila mwamba ngoma kuvutia kwake? Raila Odinga naye ametangaza manifesto ambayo imeibu...

Wasifu wa Hayati Mwai Kibaki 23.04.2022

Wasifu wa Hayati Stanly Emilio Mwai Kibaki aliyeongoza Kenya kati ya 2002 - 2012 na kuaga dunia tarehe 22/04/ 2022. Wasifu huu umeandaliwa na kusimuliwa na Victor Mulama.

Siasa Podcast; Ni kwanini viongozi wengi hasa wawakilishi wadi wametemwa katika michujo za vyama? 20.04.2022

Mchujo wa vyama vya kisiasa unapoendelea, lipo jambo moja bainifu kuhusu matokeo kuhusu ngome za Naibu wa Rais William Ruto kulinganishwa na ngome ya Raila Odinga. Kwenye eneo la Bonde la Ufa ambako Ruto ana ufuasi mkubwa, baadhi ya wanasiasa wenye tajriba wamelambishwa sakafu huku vijana wengi wakiingia ulingoni. Na huko Nyanza, wanasiasa wengi waliokuwapo uongozini wamedumishwa hasa katika nyadh...

Siasa na Gumzo: Vyama vya ODM na UDA vyazungumzia mikakati vinavyoweka kuelekea uchaguzi mkuu. 19.02.2022

Uchaguzi mkuu unapokaribia kila chama cha kisiasa kinaweka mikakati ya kuhakikisha mchujo utaofanyika katika chama unakuwa huru na wa haki. Mkurugenzi Mkuu katika Chama cha UDA, Odanga Pesa vilevile Cathrene Muma ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Uchaguzi ya ODM wanazungumzia mikakati mbalimbali inayofanywa na vyama vyao kuelekea uchaguzi mkuu ujao.

Siasa na Gumzo: Jubilee yafufuka? OKA nayo yapata marafiki wapya 05.02.2022

Baada ya kimya kingi na fukuzafukuza chamani, hatimaye Rais Uhuru Kenyatta amefanya mkutano na viongozi wa Jubilee katika Ikulu. Ikumbukwe chama hicho kimepanga Mkutano wa Kitaifa wa Wajumbe, NDC tarehe 25 Februari, 2022 katika Ukumbi wa KICC, mjadala ukiwa kuwafurusha rasmi Ruto na wandani wake kutoka chama hicho, mpango wa kushirikiana na miungano mingine na kumfanyia kampeni Raila Odinga. Vilev...

Ukweli wa Mambo: Mudavadi alisema ukweli Bomas ama la? Tunaweka paruwanja 31.01.2022

Katika Ukweli wa Mambo leo, tunaangazia hotuba ya Musalia Mudavadi wakati Kongamano la Kitaifa la ANC, Januari 23 mwaka wa 2022. Je, aliyoyasema yana ukweli ama la na kwa kiwango gani? Huu hapa ukweli wa mambo baada ya utafiti wa kina baina ya Shirika la Habari la Standard kwa ushirikiano na kampuni ya Africa Check. Katika hotuba yake ya kipekee ya kukubali uteuzi wa kupeperusha bendera ya urais k...

Gumzo la Wiki Podcast; Tutarajie miungano gani baada ya Mudavadi kuungana na Ruto? Wakenya wajadili. 29.01.2022

Mjadala mkali umetawala vinywa vya wengi wiki hii, kufuatia hatua ya Mudavadi na Wetangula kujiondoa katika OKA na kuungana na Ruto. Hatua hiyo imechochea gumzo huku wengi wakijiuliza je, Ruto atavuna kura nyingi za Magharibi dhidi ya Raila? Hatima ya Kalonzo katika OKA ni gani hasa? Atawania urais, ama ataungana na Raila katika Azimio la Umoja? Wanahabari wetu John Mbuthia wa Nyeri na Martin Ndie...

Gumzo la Wiki Podcast; Mudavadi awazuia Odinga na Ruto kuhudhuria NDC 22.01.2022

Earthquake aliyoahidi Musalia Mudavadi inasubiriwa kwa hamu kuu Jumapili. Amewaalika wana'OKA na kuwafungia nje Ruto na Raila. Wakenya wana maoni gani? Aidha, cheche baina ya Raila na Ruto zimezidi, kuhusu urushaji mawe na kuitana majina. Haya yanahatarisha utangamano nchini? UDA tayari imeandikia ICC ikidai serikali inafadhili vurugu kwa manufaa ya Raila. Vilevile tunaangazia kesi ya BBI katika M...

Mwanajeshi mstaafu Marekani, anawania ubunge Marakwet Magharibi-Benson Cheserek 18.01.2022

Benson Cheserek ni miongoni mwa Wakenya ambao wanaishi ughaibuni (Kenyans in diaspora) na sasa analenga kuwania kiti cha ubunge kwenye eneo la Marakwet Magharibi katika Kaunti ya Elgeyo Marakwet. Cheserek amekuwa akiishi Marekani kwa miaka 17 ambapo amefanya kazi katika jeshi la Marekani kwa miaka 8 kabla ya kuanza biashara yake binafsi. Kwenye mahojiano na mwanahabari Faith Kutere, Cheserek anase...

Gumzo la Wiki Podcast: UDA yadai kwamba kamatakama ya wanaohusishwa na chuki inawalenga wanachama wake, kunani? OKA nayo yaonekana kuchanganyikiwa kuhusu siku ya kumtangaza mgombea wa urais, 15.01.2022

Wanasiasa kadhaa wamekamatwa kwa kuhusishwa na matamshi ya uchochezi. Swali ni je, kuna mapendeleo jinsi UDA inavyodai? Je, ni kamatakamata kwa kigezo cha mirengo ili kuleta usawa wa kisiasa? Aidha, Rais Kenyatta alifanya mkutano katika Ikulu na viongozi wanaounga mkono Azimio la Umoja akiwamo Raila ambapo wote walipigia debe Mswada wa Marekebisho ya Sheria za Vyama vya Kisiasa. Vigogo wa OKA wali...

Kitendawili cha idadi kubwa ya wabunge kati ya mirengo ya Raila na Ruto bungeni? 09.01.2022

Mswada wa Marekebisho ya Sheria za Vyama vya Kisiasa umekuwa kichocheo cha mjadala wiki hii, ambapo wengi wanajiuliza iwapo kufaulu kwake kutakuwa mwanzo wa wanasiasa kuaminiana. Je, iwapo mswada huo utafanywa sheria, tutarajie miungano gani, hasa kati ya nani na nani? Na je, mswada huu umeashiria upande gani kuwa na ubabe bungeni? Aidha, tunaangazia mwaliko wa Ruto kwa kina Mudavadi na Wetangula...

Gumzo la Wiki Podcast: Mudavadi ajiunge na Raila ama Ruto? 20.12.2021

Mjadala mkali unaendelea kufuatia hatua ya Raila Odinga kuwatafuta marafiki wapya wa kisiasa, hasa kwenye eneo la Magharibi baada ya Mudavadi kusisitiza kwamba hatamuunga mkono tena. Aidha, Ruto anawataka Mudavadi na Wetangula wajiunge naye katika UDA. Si hayo tu, ipo hofu kutokana na kupanda kwa maambukizi ya korona hasa baada ya kugunduliwa kwa Omicron hapa Kenya. Wanahabari wetu John Mbuthia wa...

Gumzo la Wiki Podcast: Raila debeni 2022; Wana'OKA watamuunga nani? 12.12.2021

Tangazo la Odinga kuwania urais kwa mara ya tano, ni ithibati kamili kwamba kinyang'anyiro kitakuwa kati yake na William Ruto. Je, hatima ya Kalonzo, Mudavadi na Wetangula ambao walikosa kufika Kasarani ni ipi? Aidha, Wakfu wa Mlima Kenya Foundation, MKFumesema Raila tosha. Je, unadhani wafanyabiashara hao wataamua mwelekeo wa siasa za Mlima Kenya ama ni wananchi ndio watakaoamua jinsi anavyosisit...

Gumzo la Wiki Podcast: Kenya si tajiri; Wakenya wamwambia Uhuru 05.12.2021

Kauli ya Rais Kenyatta kuwa Kenya ni namba sita barani Afrika kwa utajiri imewaghadhabisha Wakenya wanaosema umaskini umekithiri nchini. Kuhusu siasa, Rais Kenyatta anasema wanasiasa viana watashindwa na wazee licha ya mbio zao za kisiasa. Je, sasa ni wazi kuwa Uhur anamuunga mkono Odinga kuwania urais? Je, hatima ya OKA ni gani? Aidha, IEBC imejiondoa katika kamati ya pamoja ya maandalizi ya ucha...

Gumzo la Wiki Podcast: Mawe Kondele; Ruto alaumiwa 14.11.2021

Naibu wa Rais William Ruto abebeshwa lawama kuhusu vuruga za Kondele. Je, vuruguzu hizo zilichochewa kisiasa anavyodai? Na je, Ruto alifanya makosa kumshtumu Odinga katika ngome yake? Adha, Wakenya wanahisi kwamba Kalonzo Musyoka amekosa mwelekeo na wakati umefika kwake kutangaza wazi msimamo wake wa kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu ujao. Vilevile, Nick Mwendwa atakiwa kueleza jinsi amekuwa akiendes...

Gumzo la Wiki Podcast; OKA yafufuka, Jubilee ikiwaka moto 07.11.2021

Imekuwa wiki yenye matukio kadhaa ya kisiasa huku muungano wa OKA ulioonekana kufifia ukifufuka kwa mikutano ya kuwatia wasiwasi wapinzani japo swali ni lile lile la ni nani atakayepata tikiti? Kule Jubilee, mikakati ya kumtema Ruto rasmi inaendelea huku naye akiendeleza cheche kali, wakati huu akikosoa mikopo waliyoichukua kwa pamoja na Rais Kenyatta. Wanafunzi nao wamefanikiwa kuishinikiza serik...

Gumzo la Wiki Podcast: Waiguru ahamia UDA; OKA yapinga kugawika 31.10.2021

Gavana wa Kirinyaga, Ann Waiguru aigura Jubilee na kujiunga na UDA. Je, Ruto atamchagua kuwa mgombea mwenza? Je, ataweza kumenyana na Purity Ngurici na Martha Karua? Vilevile, Wakenya wamkumbusha Kenyatta ahadi ya kutoa mwanga zaidi kuhusu ufichuzi wa Pandora Papers. Aidha, Mudavadi na Kalonzo watakiwa kuweka wazi misimamo yao kuhusu kinyang'anyiro cha urais mwaka ujao. Watakwenda hadi debeni au l...

Gumzo la Wiki Podcast; Kafyu na vicheko vya UhuRuto; maoni ya Wakenya 24.10.2021

Kuondolewa kwa marufuku ya kuwa nje kwashabikiwa na Wakenya. Aidha, Mt. Kenya yasubiri ahadi ya Uhuru kuhusu kilichomkosanisha yeye na Ruto. Huko Kisii, hulka ya kuwateketeza wazee kwa madai ya kushukiwa kuwa wachawi yazua ghadhabu na kauli kinzani. Wanahabari wetu, John Mbuthia, William Omasire na Martin Ndiema wamewashirikisha wananchi kuhusu haya.

Gumzo la Wiki Podcast: Mt. Kenya Foundation ina ushawishi wa kisiasa? 10.10.2021

Vikao vya Wafanyabiashara wa Mount Kenya Foundation vimetikisa siasa za Kenya wiki hii, baada ya kusema wataamua kuhusu mgombea wa urais watakayemuunga mkono miongoni mwa vigogo wa OKA na Raila. Je, ajenda ya wafanyabiashara hao ni kumkabili Naibu wa Rais, William Ruto au ni kupigania maslahi ya wakazi wa Mlima Kenya? Aidha, ufichuzi wa Pandora Papers umeibua maswali mengi kuhusu uzalendo wa Kenya...

Écoute le podcast Siasa na Gumzo sur Replaio

La radio et les podcasts dans une seule appli - gratuite, sans inscription. Installe-la dès aujourd'hui et ne rate pas le lancement

Télécharger sur Google Play

Replaio n'est pas éditeur de podcasts ; les noms des émissions, les visuels et l'audio appartiennent à leurs auteurs et sont diffusés via des flux RSS publics