Hub of Wisdom inc.

H.W PODCAST - Positive Vibes!

Ni muda wa kuchukua nafasi yako katika meza ya H.W nasi tutawasilisha kwako mawazo ya thamani kwa maneno ya dhahabu. Mahali pa kwanza na pekee unapohitaji kuwa kwa ajili ya ustawi wako. Karibu tujifunze vingi. Pata nafasi ya kusikiliza mambo ya msingi sana yatakayonoa stadi zako, kukuongezea maarifa na kuchochea maendeleo yako ya kiutu. #Karibu_nyumbani.

Auteur

Hub of Wisdom inc.

Catégorie

Education

Site du podcast

www.hubofwisdom.com

Dernier épisode

12 janv. 2025

Où écouter ?

Les podcasts dans l'appli Replaio Radio Bientôt disponible

Les podcasts arrivent très bientôt dans l'appli. Installe-la dès maintenant et découvre en avant-première une toute nouvelle façon de vivre les podcasts

Télécharger sur Google Play Installe-la gratuitement Android 5 M+ de téléchargements · note de 4,8 iOS bientôt

Épisodes

UHURU WA KIFEDHA KUPITIA UWEKEZAJI - Emilian Busara (MBA, CPA) 12.01.2025

Ikiwa unaanza au ni mzoefu tayari katika eneo la uwekezaji kupitia hisa, UTT, hati fungani (bonds) katika video hii mwanataaluma Mwl. Emilian Busara (MBA, CPA) katika uongozi katika biashara, miradi na fedha anakufundisha hatua kwa hatua mbinu rahisi na za kipekee za kuwekeza kwenye hisa na masoko ya fedha kwa mafanikio makubwa! Utajifunza: jinsi ya kuchagua hisa sahihi, kuanza uwekezaji hata kama...

Najma Paul - KUIJENGA NGUVU YAKO & KUKABILIANA NA CHANGAMOTO 13.11.2024

"Nianze kwa kuzungumzia hili eneo... Mitikasi ya maisha yako, kutafuta kwako, kupambana kwako. Lifestyle yako, maizingira unayoishi, vinaamua, vinahitaji na vinajenga NGUVU YAKO." Anasema Najma Paul "Fanya vitu vinavyokukwaza, vitu vinavyokukera, katikati ya hivyo vitu kuna miujiza. Niamini mimi." Angalia toleo hili na mengine mengi kwa njia ya Youtube (H.W TV) www.youtube.com/hubofwisdom-inc Tuma...

KUFIKIA KIWANGO CHA JUU ZAIDI KATIKA KILE UTAKACHOKIFANYA - Sebastian Kolowa 26.01.2024

"Sisi sote tuna nafasi ya kustawi zaidi katika chochote tunachokifanya. Changamoto inayotukumba vijana wengi ni kwamba hatutambui na kuzifuata zile hatua muhimu zenye kutufikisha hapo. Muda ni mchache na sio sawa kwenda bila dira. Ndio maana leo nimeona niyazungumze haya yafuatayo..." Anasema Sebastian Kolowa katika mkutano wa nne wa Hub of Wisdom Community Jijini Dar Es Salaam. Fuatilia...

MAKOSA MAKUBWA YANAYOFANYIKA KATIKA MAHUSIANO NA NAMNA YA KUYAEPUKA - Sadaka Gandi #Mapenzi 26.01.2024

"Wewe unaamini kwamba huyo mwenzako unampenda kumbe kuna makosa makubwa sana. Twende pamoja tuangalie vijana wanakosea wapi na namna gani ufanye ili kuepuka au kurekebisha makosa." Anasema Bi Sadaka Gandi, mtaalamu wa saikolojia ya familia na mshauri mbobevu katika maswala ya mahusiano. Fuatilia matoleo haya katika H.W TV kwa njia ya YouTube na kwa mfumo sauti kupitia H.W PODCAST. Pia us...

KUONGEZA THAMANI 11.12.2023

Hauwi wa thamani kwasababu ya kile unachokipata bali kile unachokitoa. "Kwakuwa kile apandacho mtu ndicho atakachovuna, apandaye haba atavuna haba. Apandaye kwa ukarimu atavuna kwa ukarimu." Kitakachofanya bidhaa zako au huduma zako ziwe za thamani sio gharama yake bali ni manufaa yanayotokana na hiyo huduma. Ili upate faida kubwa kutokana na kile unachokifanya unatakiwa upande mbegu ya...

NAMNA SAHIHI YA KUJENGA 15.11.2023

"Start Small think Big". Zingatia mambo madogo. "Start Small, Think Big". Ukifanya vizuri katika uwanda mdogo hata siku ukiwa katika uwanda mkubwa, uwezekano ni kwamba utafanya vizuri. Wakati unapofikiria kujenga mambo makubwa anza kidogokidogo. ....................................................................... Maoni yako ni muhimu na atunayathamini sana, hivyo tuma ujumbe...

KWANINI MAHUSIANO MENGI YA KIMAPENZI HAYADUMU? - Sarah Ngonyani 03.11.2023

Kwa uwazi na utaalamu Mis Sarah anaelezea namna ya kudumisha mahusiano ya kimapenzi. Sikiliza

WATU 30.10.2023

"The more hands you shake, the more opportunities you create." Katika hatua za awali za kujenga biashara au asasi uwezekano mkubwa ni kwamba watakaojihusisha na wewe ni watu wanaokufahamu. Vivyo hivyo ili watu wakufungulie milango ya fursa kigezo kimoja wapo kikubwa ni namna gani wanakufahamu. Fuatilia mtiririko wa episode hizi katika YouTube: H.W TV na Podcast: H.W PODCAST kila wiki. Ma...

MIPANGO 25.10.2023

Watu wengi hudhani kuwa wakipata fedha nyingi ndio watafanya mambo fulani makubwa. Lakini ukweli ni kwamba wengi hawana umadhubuti wa matarajio yao, yapo hewani tu. Fuatilia mtiririko wa episode hizi kwa katika YouTube: H.W TV na Podcast: H.W PODCAST kila wiki. Maoni yako ni muhimu na atunayathamini sana, hivyo tuma ujumbe wako wa sauti kwa njia ya WhatsApp nasi tutaumbatanisha katika toleo lijalo...

SIRI ZA USHINIDI - Halima Kopwe (MISS WORD TZ 2023) 25.10.2023

'From a Rough to a Diamond' Mis. Halima Kopwe anaelezea safari yake ya ushindi na kile anachowashauri vijana wengine wenye kiu ya kustawi katika nyanja walizopo. EDITION 4 - THE WISE MEGA MEET-UP (Episode) Tembelea www.hubofwisdom/media kuangalia na kusikiliza zaidi. Toa maoni yako ili jukwaa hili lizidi kuwa bora kwa ajili yako, tumia 0753825794 au tuandikie katika barua pepe hubofwisdom@...

DONDOO ZA MPENYO WA KIUCHUMI - James Mwang'amba. 03.05.2023

"Tunaposema mpenyo wa kifedha maana yake ni kwamba mtu anatoka sehemu moja ya chini na kwenda katika sehemu nyingine ya juu. Ushindani ni mkubwa na hakuna mtu anayejali kwamba unalia au unalalamika. Watu wanataka kuona kwamba unaleta nini mezani." Anasema James Mwang'amba. Fuatilia muhtasari huu wa mazungumzo ili kufahamu dondoo za kukuweka sehemu ya juu kifedha katika eneo lako la kazi au biashar...

MALENGO (Goal Setting) - Anthony Luvanda 28.02.2023

Unachotakiwa kufahamu kuhusu malengo. Anthony Luvanda anazungumzia manufaa ya kuweka malengo, sababu zinazowafanya watu wengi wasizingatie kuweka malengo na Kwanini watu wengi wenye malengo wanashindwa kutekeleza. Ufanye mini kuliepuka hilo? Tia maono yako kuhusu toleo hili. Tuma ujumbe wa sauti na kuelezea ulichojifunza nasi tutaambatanisha katika toleo lijalo.

Dina Marios anatoa funzo kubwa kutoka katika historia ya kusisimua ya maisha yake. Hamasika! 12.08.2022

Mwanadada Dina ni mmoja wa watu wanaoshangiliwa sana hapa Tanzania. Ameotesha mizizi ya ushawishi kwa hadhira yake kupitia umaridadi alionao katika media na harakati za kuwaleta wanawake wa kitanzania pamoja. Lakini nani ajuaye kuhusu mapito yake na kilichomfanya asimame na kuwa mfano bora hata leo. Hapa anatoa hamasa ya maisha. Mawazo yake juu ya kinachopaswa kufanywa na kila mwanajamii mwenye ki...

MAPENZI YA BLUETOOTH - Irene Kamugisha. 30.07.2022

"Connection kwenye mapenzi ni suala la muhimu sana. Inawezekana kufanya mapenzi yakashamiri na yakawa na tija kwa wewe na mwenzako kama kuzingatia mambo haya niyakayoyazungumza hapa." Anasema madam Irene Kamugisha. Mmoja wa washauri bora sana wa masuala ya mahusiano hapa Tanzania.

Mafanikio ya Kifedha | Victor Mwambene - (Kanuni kumi za kutengeneza fedha) 21.07.2022

"Mafanikio ya kifedha sio bahati, mafanikio yanakuja kwa kuwa na maarifa sahihi juu ya fedha, kwa juhudi, nidhamu binafsi na kwa kupambana. Mungu ametupa wote neema ila ni tabia zetu, imani na fikra zetu ndio zinazoamua ustawi wetu. Hizi ni kanuni kumi zitakazokujengea uwezo wa kustawi kiuchumi." Anaeleza Mwalimu Victor Mwambene, muelimishaji wa maswala ya fedha na biadhara. Sikiliza kanuni kumi m...

Mkakati wa maendeleo Binafsi - Mosses Raymond (Samora) 06.07.2022

Ili mwanadamu aweze kutimiza kusudi la uwepo wake maishani ni lazima atumie na kuboresha uwezo wake binafsi. Kwa kufanya hivyo ndio atakuwa mwenye tija. Mosses Raymond anaeleza ukweli wa maisha, kwanini tujinoe, kwa namna ipi, na namna gani tujiendeleze kibinafsi. Kuwa sehemu ya mijadala hii kwa kutuma neno WISDOM kwenda namba 0753825794.

Kujiandaa kwa ajili ya ndoa - Chris Mauki 01.07.2022

"Ndoa ni kama nyumba, msingi usipokuwa mzuri, nyumba haiwi imara."

KUFUNGUA MILANGO YA FURSA ZA KIFEDHA - James Mwang'amba. 28.04.2022

Kustawi kifedha na mafanikio ya uchumi kwa ujumla ni matokeo ya maarifa na juhudi zinazoelekezwa katika kutengeneza fursa na kuzitumia. James Mwang'amba ni mtaalamu wa masuala ya biashara na mhamasishaji. Ni mjasiriamali na mbobevu katika masuala ya fedha. Katika episode hii anazungumzia mbinu muhimu za kukua kifedha.

KUOA NA KUOLEWA. Upi ni muda sahihi? Fahamu sababu na namna ya kushulika nazo - Sadaka Gandi. 11.04.2022

"Tunaongea habari ya kuoa na kuolewa. Pamoja na kwamba wanasema ndoa haina fomula lakini kuna _best practices_ ambazo ukizifuata utaona matunda." Anasema Aunt Sadaka. Pata kufahamu kuhusu madhara ya kuoa au kuolewa mapema, kuchelewa, sababu zipi hupelekea na namna gani ya kushughulika nazo. Kuwa sehemu ya mijadala hii kwa njia ya whatsApp. Tuma neno WISDOM kwenda namba 0753825794.

Masoud Kipanya - MBINU MBADALA ZA MAENDELEO 28.03.2022

Maendeleo ni kitu muhimu na tunahitaji uthubutu na uimara wa kifikra ili tufaulu. "Na ukitaka kufaulu kuliko kwingi, jifunze sana kutokulaumu watu, jifunze kutokutegemea watu. Jifunze kutengeneza njia." Anasema Ally Masoud. "Mambo yote haya yanaanza na fikra ndugu zangu." @masoudkipanya .................................................... Kuwa sehemu ya mijadala hii kwa kutuma neno WISDOM kwenda n...

KANUNI ZA MAFANIKIO - Anthony Luvanda. 15.03.2022

"Ninaamini haya mambo saba ukiyafanya basi kuna uwezekano mkubwa sana yakwamba ukafanikiwa katika jambo lolote unalotaka kulifanya." Anasema Anthony Luvanda. Mr. Anthony Luvanda anaelezea mambo yanayochochea mafanikio. #kanuni #mafanikio #luvanda #karibu_nyumbani ................. Kuwa sehemu ya Mijadala hii kwa njia ya WhatsApp kwa kutuma neno WISDOM kwenda namba 0753825794

Joel Lwaga - KWENDA KWA VIJANA WENYE SHAUKU YA KUSTAWI KATIKA MAISHA YAO. (An inspiring interview) 07.03.2022

"Wewe ambaye unahisi unakipaji fulani, kifanyie kazi. Natamani kila mmoja ajue ya kwamba Mungu amempa kila mtu uwezo, na hicho kipawa ndio sahani yako." Anasema Joel. "Kuna wakati nilihisi kukata tamaa, kipindi ambacho hakuna tumaini, katika hali kama hiyo Mungu analeta ujumbe, 'Mimi ni mtetezi wako, hautobaki kama ulivyo''' Joel Lwaga ni mwimbaji wa nyimbo za injili nchini Tanzania. Ni mmoja wa v...

SIRI 5 ZA KUDUMISHA MAPENZI - Dr. Chris Mauki. 24.02.2022

Dr. Chris Mauki mtaalamu na mbobevu katika maswala ya mahusiano. Hapa anaelezea siri tano zitakazokusaidia kufanya mahusiano yako yastawi, kukuweka tayari kwa ajili ya kuingia kwenye mahusiano, kukusaidia kutatua migogoro na mambo mengine mengi unayopaswa kuyajua ili kukufanya imara na kukupa ujuzi katika eneo mapenzi. Kushiriki mijadala hii kwa njia ya whatsApp tuma neno WISDOM kwenda namba 07538...

TATHMINI YA MAISHA YA YAKO - Amos Makala 24.02.2022

Kuna haja ya kufanya tathmini ya maisha yako. Maana cha muhimu kwetu sio miaka tunayoishi kwenye maisha yetu bali maisha tunayoishi kwenye miaka yetu. Amos anaelezea kwa upana.

NAMNA NZURI YA KUPENDA | Amri Amri 19.02.2022

Je, unafahamu namna nzuri ya kupenda? Amri Amri anazungumza juu ya 'namna ya kupenda kweli.' Namna gani mwenza anatakiwa afanye kwa ajili ya kulinda na kuendeleza mapenzi ya kweli. Mambo ambayo hutakiwi kufanya kwenye mapenzi. Kuwa sehemu ya mojadala hii kwa njia ya WhatsApp kwa kutuma neno WISDOM kwenda namba 0753825794. #Karibu_nyumbani

Écoute le podcast H.W PODCAST - Positive Vibes! sur Replaio

La radio et les podcasts dans une seule appli - gratuite, sans inscription. Installe-la dès aujourd'hui et ne rate pas le lancement

Télécharger sur Google Play

Replaio n'est pas éditeur de podcasts ; les noms des émissions, les visuels et l'audio appartiennent à leurs auteurs et sont diffusés via des flux RSS publics