RFI Kiswahili

Siha Njema

Health SW ↓ 24 Folgen

Makala inayojadili kwa kina masuala ya afya, tiba na kutambua magonjwa mbalimbali bila ya kusahau namna ya kukabiliana nayo. Watalaam walibobea kwenye sekta ya afya watakujuvya na kukuelimisha juu ya umuhimu wa kuwa na afya bora na si bora afya. Pia utawasikiliza kwa maneno yao watu ambao wameathirika na magonjwa mbalimbali na walikumbwa na nini hadi kufika hapo walipo.

Autor

RFI Kiswahili

Kategorie

Health

Podcast-Website

www.rfi.fr

Neueste Folge

10. Jul 2026

Wo hören?

Podcasts in der App Replaio Radio Bald verfügbar

Podcasts kommen bald in die App. Installiere sie jetzt und erlebe als Erster einen ganz neuen Blick auf Podcasts

Bei Google Play herunterladen Kostenlos installieren Android 5 Mio.+ Downloads · Bewertung 4,8 iOS bald

Folgen

Mashirika ya kiraia Afrika yaanza kampeni dhidi ya madeni ya umma 10.07.2026

Mashirika ya kiraia yanasema nchi za Afrika zinalipa deni na kuachwa  na kiasi kidogo cha pesa kuendesha shughuli muhimu za serikali ,sekta ya afya ikiathirika zaidi Mashirika haya yanataka umoja wa Afrika kuja na jopo ambalo litakuwa linaangazia  maswala yote kuhusu mikopo ili kupunguza dhulma kwa nchi zinazoendelea

Kampeni kuhakikisha vyakula vilivyosindikwa vina maandishi ya kuonya 30.06.2026

Tafiti kadhaa za kiafya zimebainisha magonjwa mengi yasiyoambukizwa yana uhusiano mkubwa na vyakula vilivyosindikwa  na hali ya watu kukosa kuzingatia mazoezi  ya kila mara. Kenya ikiwa taifa la kwanza Afrika Mashariki kupitisha  mwongozo unaotoa maelekezo kuhusu viwango vya  madini ambavyo  vyakula au vinywaji  vinavyouzwa vinafaa kukidhii  au kwa lugha ya kiingereza Kenya Nutrient Profile Model,...

Kwa nini ni muhimu wanaume kuzingatia afya zao haswa afya ya akili 23.06.2026

Mwezi Juni ni mwezi wa kutoa uhamasisho kuhusu afya ya akili miongoni mwa wanaume ,swala la afya ambalo hupuuzwa mno Daktari Dominic Osiemo anasema wanaume wana haki wa kuonesha hisia ,kueleza maumivu  yao na kutaka kuskizwa. Na wanapofanya hivyo wanalinda afya zao za akili. Anaonya wanaume wengi wanakuwa hatarini kwa sababu wanajaribu kudhihirishia jamii kuwa wao ni imara siku zote. Baadhi ya vip...

Shule ya Mali jijini Nairobi inavyowasaidia watoto wenye Austism pamoja na wazazi 16.06.2026

Katika mkakati wa kupunguza unyanyapaa kwa wazazi wanaowalea watoto wenye Autism shule ya Mali inatoa tiba nasaha  na elimu kwa pamoja ikizingatia pia mahitaji ya wazazi wao ambao mara nyingi wanahitaji pia matunzo

Shinikizo kutaka mataifa kuja na sera endelevu na salama za uchukuzi 11.06.2026

Shinikizo zinazidi kutolewa kwa mataifa ya Afrika kukumbatia sera za uchukuzi zilizo salama na endelevu ili kupunguza idadi ya vifo vinavyotokana na barabara na madhara ya ajali za barabara kwa jamii. Katika  kongamano la kujadili mpango huo wa usalama ulio endelevu ,wadau wamesikitika vifo vya barabarani bado vinaripotiwa miongoni mwa watembea miguu na waendesha pikipiki. Katika makala ya Siha Nj...

Majanga yanaweza kusababisha matatizo ya afya ya akili miongoni mwa watoto 06.06.2026

Mataifa ya Afrika yameshuhudia mafuriko katika miaka ya hivi karibuni ,hali ambayo imesababisha wananchi wengi kulazimika kuhama makazi yao Nchini Kenya ,ukanda wa magharibi ,katika eneo la Busia,mafuriko hayo yamevuruga kalenda za wanafunzi wa shule ,watoto wengi wakishindwa kuendelea na shule au kukubaliana na msongamano kwenye shule chache ambazo ziko maeneo salama Hali hii imewasababisha chang...

Mwendelezo wa mlipuko wa Ebola DRC na namna wenyeji wanavyojikinga 30.05.2026

Watu 220 wamefariki kwenye mlipuko wa Ebola unaohusishwa na virusi adimu vya Bundibugyo huku wengine zaidi ya 1000 wakiwa wameambukizwa Mlipuko huu hatari umesababisha baadhi ya mataifa kufunga mipaka yake na kuweka masharti magumu ya tahadhari

Kwenye kapu la sekta ya afya kufuatia kongamano la Africa Forward 22.05.2026

Baadhi ya makubaliano yalitotangazwa na Ufaransa baada ya siku mbili ya kongamano la  Africa Forward ni ufadhili kwa uzalishaji wa dawa na chanjo hapa barani Afrika. Shirika la Unitaid  pia lenye ushirikiano na Ufaransa lilitangaza kuratibu mchakato wa kuzalishwa dawa mpya ya kuzuia virusi vya HIV ,Lenacapavir kuzalishwa Afrika Kusini. Na kwenye viungo vingine vilivyosheheni majadiliano ya kuimari...

Mashirika ya kiraia Afrika yanataka nchi za Afrika kuwa na taratibu za pamoja kudhibiti magonjwa 16.05.2026

Taratibu hizo za pamoja yatahakikisha kuwa nchi za Afrika zinaweka bajeti kwenye sera ya uchumi na kuipa kipau mbele ufadhili wa afya

Watalaam wasisitiza uwekezaji wa utafiti wa DNA barani Afrika 05.05.2026

Utafiti unaoangazia vinasaba katika ukanda wa Afrika unaweza kuwa jawabu kwa ubainishaji potovu,gharama ya juu ya matibabu na usugu wa vimelea .  Kwa kuanzia , Mashirika matatu ya Afrika ya kitafiti  yametangaza mkataba wa dola milioni 3 nukta 5 ambao utawekezwa  kwenye utafiti  huu wa DNA  barani . Mashirika haya yakiwa ni Biolinx Africa,  YTO Foundation  yenye makao Ivory Coast na  Nextgen Molec...

Mpango wa kuongeza ujuzi wa wahudumu wa afya kwa kutumia teknolojia 28.04.2026

Ufadhili wa afya ukanda wa Afrika umezidi kupungua tangu kusitishwa kwa ufadhili mkubwa wa kigeni Pengo hilo linamanisha serikali nyingi hazina uwezo wa kifedha wa kutosha kuendelea kutoa mafunzo endelevu ya wahudumu wa afya. Katika kujaribu kutatua changamoto hii ,mpango wa ECHO unaowasaidia wahudumu wa afya kujifunza wakati wanapoendelea kuwahudumia wagonjwa ,umekuja kuleta matumaini.

Mataifa ya Afrika mbioni kuboresha mkataba wa kupambana na majanga 23.04.2026

WHO ilitoa nafasi zaidi kwa mataifa ya ulimwengu kujadililiana zaidi kuhusu vipengee muhimu kwenye mkataba wa kukabiliana na majanga ya kidunia Vipengee hivyo ni pamoja namna mataifa yanaweza kunufaika kutokana na mchango wao kwenye tafiti za kisayansi ,vimelea vinavyotoka kwenye mataifa yao na usawa wakati wa usambazaji wa chanjo au dawa

Miaka mitatu tangu Sudan kuingia kwenye mzozo huduma za afya zimedorora 16.04.2026

Asilimia 37 ya vituo vya afya nchini Sudan vimeharibiwa wakati wa mapigano na haviwezi kutoa huduma za afya Shirika la madaktari wasio na mipaka,MSF limekuwa likiwahudumia wagonjwa wenye majeraha ,waathiriwa wa magonjwa ya milipuko na waathiriwa wa ubakaji. Hali ya usalama imeilazimu  MSF kusitisha huduma katika maeneo kadhaa baada ya kushuhudiwa mashambulizi ya moja kwa moja kwenye vituo vya afya...

Kliniki tembezi za figo zinavyowasaidia wagonjwa wa figo nchini Kenya 07.04.2026

Idadi ya wagonjwa wa figo imekuwa ikiongezeka kutokana na kuongezeka pia kwa magonjwa yasiyoambukiza kama vile Kisukari.

Magonjwa ya Autoimune yana uwezo kukusababishia magonjwa mengine zaidi 31.03.2026

Magonjwa yanayoshambulia kinga yanapompata mtu ,huendelea kusambaa ,kudhuru kingamwili na  kumweka hatarini mgonjwa kiasi cha kuwa mgonjwa anaweza kupatwa na magonjwa zaidi ya moja ya aina hiyo. Elwyn Chebet aligunduliwa na Lupus na baadaye akajikuta anapambana na magonjwa zaidi ya tano aina ya Autoimmune. Mwezi Machi ambapo ulimwengu huelekeza kurunzi kwenye magonjwa ya mfumo wa kinga au Autoimmu...

Visa vingi vya TB Afrika bado vinapatikana miongoni mwa vijana hasa wanaume 24.03.2026

Watalaam wanasema vijana wengi hufikia kwenye maduka ya kuuza dawa kupata huduma za afya baadala ya kufika hospitali kufanyiwa vipimo Unyanyapaa pia inachangia wanaume au vijana kuwa na ari ya kwenda kupata huduma za afya haswa za TB.

Nini magonjwa yanayoathiri kinga mwili au Autoimmune 24.03.2026

Unapopata magonjwa ambayo yanaathiri kinga ya mwili wako,ina maana kuwa kinga yako inaweka mifumo yote ya mwili kwenye hatari. Unaweza kujikuta unapata magonjwa kama Lupus,ugonjwa wa Tezi Koo au Mifupo yako kuwa nyepesi kiasi cha kuvunjika kwa urahisi. Ubainishaji wa magonjwa haya unahitaji subira na ufuatialiaji wa karibu ili kuelewa kila dalili anayoonesha mgonjwa .Gharama yake basi inamanisha n...

Kampeni ya kumaliza unyanyapaa wa siku za hedhi kwa kushirikisha wanaume 20.03.2026

Siku za hedhi huchukuliwa kuwa swala la wanawake na halifai kuzungumzwa hadharani kwa jamii nyingi .Hali hii imesababisha wanawake na wasichana kupitia unyanyapaa ijapokuwa hili ni swala la haki ya uzazi

Madhara ya afya ya akili yanayotokana na matumizi ya kupitiliza ya simu 03.03.2026

Ripoti ya afya akili  duniani ,inaonya kuhusu madhara yanayotokana na matumizi ya simu za mkononi miongoni mwa vijana wenye umri wa kati ya miaka 18 na 34 Katika mataifa ya Afrika ambapo matumizi ya simu hizi huanza kwa kuchelewa ,vijana walionekana kuwa afadhali ikilinganishwa na mataifa kama Finland ambapo watoto huanza kutumia simu katika umri mdogo mno.   Katika mataifa yaliyozingatia maswala...

Fahamu madhara ya mvua kubwa kwa afya yako na namna ya kujikinga 24.02.2026

Mvua kubwa inaendelea kunyesha katika mataifa mengi ya Afrika ikisababisha mafuriko makubwa ,maafa na uharibifu wa mali Mvua ingawaje ni baraka, kunaponyesha ghafla inaweza kuwa chanzo cha baadhi ya magonjwa kama vile Malaria, Kipindu Pindu na magonjwa ya kusambazwa na minyoo.

Kupambana na ugonjwa wa mbwa kichaa Nairobi kwa kuzingatia maslahi ya mbwa 10.02.2026

Mamlaka jijini Nairobi zimefanya operesheni kudhibiti ongezeko la mbwa mtaa katika mkakati wa kupambana na ugonjwa wa mbwa kichaa Mbwa japo anasemekana kuwa rafiki wa karibu na mwaminifu unapomfuga ,matunzo yasiyofaa au kuwatelekeza unaweza kukuweka karibu na ugonjwa wa mbwa kichaa Ukiwa utamfuga mbwa ,sharti kuzingatia usafi na chanjo ya kila mwaka dhidi ya ugonjwa wa mbwa kichaa

Kwa nini kuna umuhimu wa kutumia dawa za minyoo baada ya miezi sita 05.02.2026

 Shirika la afya duniani ,WHO hupendekeza matumizi ya dawa za minyoo kwa watoto kati ya mwaka moja hadi 12 ,vijana wenye umri kati ya 13- 19 ,wanawake walio kwenye umri wa kupata watoto na watu wanaoishi katika maeneo yenye minyoo. Hii ni njia mojawapo ya kupambana na utapiamlo, Anamia na matatizo yanayoletwa na minyoo.

Kufunga saum inafaidi afya yako vile vile nafsi yako ikiwa utafanya mara kwa mara 26.01.2026

Kuna ushahidi unaoonesha kwamba kufunga kunaweza kusaidia kurekebisha miili yetu ,wakati mwingine kuongeza maisha yetu, pia  njia bora ya kupunguza uzito,   Kitendo cha kukumbatia  Saum huchochea usafi wa moyo, nafsi na kusafisha mwili wako kwa kuondoa chakula ambacho mara nyingine hugeuka kuma sumu mwilini na chanzo cha magonjwa yasiyoambukiza.     Wataalam wa afya  pamoja na watetezi wa kufunga...

Mpango wa kliniki tembezi unavyowafaidi wakaaji kaskazini mwa Kenya 30.12.2025

Mpango wa kliniki tembezi yaani mobile clinics  ni pale ambapo wahudumu wa afya wanatembea nyumba kwa nyumba na kuwatibu wenyeji kama vile wazee,akina mama na watoto. Maeneo ya kaskazini mwa Kenya ambapo hospitali  huwa mbali na vijiji ,ndiyo yanayolengwa kwenye mpango huo.

Höre den Podcast Siha Njema in Replaio

Radio und Podcasts in einer App - kostenlos und ohne Anmeldung. Installiere sie noch heute und verpasse den Start nicht

Bei Google Play herunterladen

Replaio ist kein Herausgeber von Podcasts; die Namen der Sendungen, Cover und Audioinhalte gehören ihren Autoren und werden über öffentliche RSS-Feeds verbreitet