RFI Kiswahili
Siha Njema
Makala inayojadili kwa kina masuala ya afya, tiba na kutambua magonjwa mbalimbali bila ya kusahau namna ya kukabiliana nayo. Watalaam walibobea kwenye sekta ya afya watakujuvya na kukuelimisha juu ya umuhimu wa kuwa na afya bora na si bora afya. Pia utawasikiliza kwa maneno yao watu ambao wameathirika na magonjwa mbalimbali na walikumbwa na nini hadi kufika hapo walipo.
Husk at besøge podcastens hjemmeside og støtte skaberen: www.rfi.fr
Forfatter
RFI Kiswahili
Kategori
Podcastens hjemmeside
Seneste episode
7. okt. 2026
Hvor kan du lytte?
Podcasts i appen Replaio Radio Kommer snartPodcasts kommer snart til appen. Installer nu, og vær den første til at se en helt ny tilgang til podcasts
Episoder
Kifafa cha mimba bado kinasababisha vifo vingi vya akina mama na watoto Afrika 07.10.2026 9:59
Kifafa cha mimba hali inayohusishwa na shinikizo kubwa la damu mama anapokuwa mja mzito kuanzia wiki 20 za mimba na inaweza kujitokeza pia pindi mama anapojifungua ,ni hali ya dharura na tishio kubwa kwa akina mama waja wazito Watalaam wanahoji kuwa hatari yake hutokana na kwamba dalili zake wakati mwingi hufanana na dalili za kawaida za mama mja mzito Ni kutokana na hili mashirika ya kijamii kut...
Wagonjwa wa saratani wanavyochanganya matibabu ya hospitali na mazoezi 01.10.2026 9:57
Wagonjwa wengi wa saratani mara nyingi huhisi kulemewa na madhara yanayotokana na matibabu makali ambayo wanabidi kutumia kwa muda mrefu. Kurahisisha safari hiyo kituo cha Faraja Cancer Support Trust eneo la Parklands Nairobi kimewapa fursa ya kufanya mazoezi ; na kucheza muziki huku wakiendelea na matibabu hayo. Wengi ambao wamekuwa wakishiriki mazoezi hayo wanasema miili yao ina uimara zaidi...
Mchakato wa kupatikana chanjo mpya dhidi ya TB kufikia mwaka 2029 22.09.2026 10:15
Chanjo mpya za kupambana na ugonjwa wa kifua kikuu au TB zitakuwa tayari kufikia mwaka 2029 Hadi sasa chanjo 16 zimekuwa zikifanyiwa majaribio na ikiwa zitaidhinishwa zitaokoa maisha ya watu zaidi ya milioni saba kufikia 2050 haswa katika mataifa yanayoendelea. Kwa miongo kadhaa chanjo ya pekee ambayo imekuwa ikitumika kuzuia TB ni chanjo ya BCG ambayo mtoto anapewa pindi anapozaliwa. Wanaharakati...
Kwa nini kilimo sharti kuzingatiwa kumaliza njaa barani Afrika 19.09.2026 9:48
Ripoti ya mashirika kadhaa ya umoja wa mataifa yameonesha Afrika bado ina watu wengi ambao wanakabiliwa na njaa. Hii ni licha ya Afrika kuwa sehemu inayofanya kilimo . Watalaam wanasema kilimo kimeathirika na athari za mabadiliko ya tabia nchi kama vile mafuriko,ukame na sasa hivi vijana wengi hawapendi kilimo Hivi basi nini kifanyike kuhakikisha kuwa kuna lishe bora barani Afrika? Dkt Calistus K...
Kisukari inaendelea kuongeza idadi ya wagonjwa wa macho nchini Kenya 09.09.2026 10:10
Magonjwa yanoyohitaji matibabu ya muda mrefu ukiwemo kisukari unaendelea kusababisha watu wengi kupata matatizo ya macho au kupoteza uwezo wa kuona
Afrika kukabiliana na usugu wa vimelea vifo vikitarajiwa kuvuka milioni 4 02.09.2026 10:07
Kituo cha kuzuia na kudhibiti magonjwa barani Afrika ,Africa CDC kimeonya vifo vinavyohusishwa na usugu wa vimelea vinatarajiwa kuvuka milioni 4 mwaka wa 2050 Mashirika ya kikanda yanasisitiza utekelezwaji wa pamoja wa mikakati ya kukabiliana na usugu wa vimelea ikiwemo afya ya mifugo ,matumizi mazuri ya dawa za antibiotics na dawa za kunyunyuzia mimea kwenye sekta ya kilimo. Watalaam wa afya wa...
Mapambano dhidi ya Ebola Bundibugyo nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo 28.08.2026 9:41
Ebola imekamilisha siku 100 tangu ilipotangazwa na bado bado haijadhibitiwa Shirika la kimataifa la VillageReach miongoni mwa mashirika yaliyoalikwa na utawala wa Kinshasa kusaidia juhudi za kudhibiti mwambao hatari wa Ebola Bundibugyo linazungumzia kuhusu mapambano hayo. Baadhi ya changamoto zinazofanya ugumu mapambano hayo ni ukosefu wa uaminifu kati ya wananchi na serikali ,tamaduni na pia taar...
Kwa nini bima ya afya ya msafiri ni sharti muhimu kwa mataifa ya Afrika 18.08.2026 10:01
Umuhimu wa bima ya afya kwa wasafiri ni pamoja na kupunguza gharama kwa taifa mwenyeji haswa wakati huu nchi nyingi hususan za Afrika zinashuhudia ongezeko la milipuko wa magonjwa ya milipuko Sharti hilo pia linatoa fursa kwa nchi kuboresha mifumo ya afya ili kukidhi mahitaji ya wasafiri wanaohitaji huduma za afya kwa nchi wanazozitembelea.
Unaweza kuendelea kunyonyesha hata baada ya kutenganishwa kwa muda na mwanao 11.08.2026 9:44
Imani kuwa mama na mtoto wanapotenganishwa inaweza kuathiri ubora wa maziwa ya mama inapotosha. Watalaam wanasisitiza maziwa ya mama hayawezi kuharibika kwenye titi. Aidha kunyonyesha kwa uaminifu kunaweza kukuepusha na saratani na mbinu pia ya kupanga uzazi.
Kwa nini watalaam wanahoji maumivu makali wakati wa hedhi si kawaida 31.07.2026 9:52
Maumivu wakati msichana au mwanamke anapokuwa kwenye siku zake za hedhi, yanaweza kuwa ya kawaida ila maumivu haya yanapomfanya kushindwa na shughuli za kawaida si kawaida Dkt Dominic Osiemo anasema maumivu haya makali yanaweza kuwa dalili za baadhi ya changamoto za kiafya kama vile Uvimbe au ugonjwa wa Endometriosis.
Changamoto ya wanaume na wanawake kukosa hamu ya tendo la ndoa 21.07.2026 10:09
Raia mmoja wa Kenya amefika kwenye bunge la kitaifa nchini Kenya akitaka swala la wanaume na wanawake kutokuwa na hamu ya tendo la ndoa kuorodheshwa kuwa ulemavu Kwa mujibu wa daktari Dominic Osiemo ,tatizo hilo linachangiwa na maswala kadhaa yakiwemo matumizi ya dawa za kisukari ,shinikizo la damu na msongo wa mawazo.
Visa vya kung'atwa na Nyoka vyaongezeka kaunti ya Turkana Nchini Kenya 21.07.2026 9:29
Kaunti ya Turkana inaongoza nchini Kenya kwa visa vya watu kung'atwa na nyoka. Wataalamu wa afya wanasema mabadiliko ya tabianchi, joto kali na changamoto za upatikanaji wa huduma za afya vinaongeza hatari kwa wakazi wa maeneo mengi ya kaunti hiyo,huku shirika la afya duniani WHO likisema visa vya kuumwa na nyoka vinapuuzwa wakati huu karibia watu 32000 wakifariki kila mwaka kutokana na sumu ya n...
Mashirika ya kiraia Afrika yaanza kampeni dhidi ya madeni ya umma 10.07.2026 10:09
Mashirika ya kiraia yanasema nchi za Afrika zinalipa deni na kuachwa na kiasi kidogo cha pesa kuendesha shughuli muhimu za serikali ,sekta ya afya ikiathirika zaidi Mashirika haya yanataka umoja wa Afrika kuja na jopo ambalo litakuwa linaangazia maswala yote kuhusu mikopo ili kupunguza dhulma kwa nchi zinazoendelea
Kampeni kuhakikisha vyakula vilivyosindikwa vina maandishi ya kuonya 30.06.2026 10:00
Tafiti kadhaa za kiafya zimebainisha magonjwa mengi yasiyoambukizwa yana uhusiano mkubwa na vyakula vilivyosindikwa na hali ya watu kukosa kuzingatia mazoezi ya kila mara. Kenya ikiwa taifa la kwanza Afrika Mashariki kupitisha mwongozo unaotoa maelekezo kuhusu viwango vya madini ambavyo vyakula au vinywaji vinavyouzwa vinafaa kukidhii au kwa lugha ya kiingereza Kenya Nutrient Profile Model,...
Kwa nini ni muhimu wanaume kuzingatia afya zao haswa afya ya akili 23.06.2026 9:56
Mwezi Juni ni mwezi wa kutoa uhamasisho kuhusu afya ya akili miongoni mwa wanaume ,swala la afya ambalo hupuuzwa mno Daktari Dominic Osiemo anasema wanaume wana haki wa kuonesha hisia ,kueleza maumivu yao na kutaka kuskizwa. Na wanapofanya hivyo wanalinda afya zao za akili. Anaonya wanaume wengi wanakuwa hatarini kwa sababu wanajaribu kudhihirishia jamii kuwa wao ni imara siku zote. Baadhi ya vip...
Shule ya Mali jijini Nairobi inavyowasaidia watoto wenye Austism pamoja na wazazi 16.06.2026 10:17
Katika mkakati wa kupunguza unyanyapaa kwa wazazi wanaowalea watoto wenye Autism shule ya Mali inatoa tiba nasaha na elimu kwa pamoja ikizingatia pia mahitaji ya wazazi wao ambao mara nyingi wanahitaji pia matunzo
Shinikizo kutaka mataifa kuja na sera endelevu na salama za uchukuzi 11.06.2026 9:46
Shinikizo zinazidi kutolewa kwa mataifa ya Afrika kukumbatia sera za uchukuzi zilizo salama na endelevu ili kupunguza idadi ya vifo vinavyotokana na barabara na madhara ya ajali za barabara kwa jamii. Katika kongamano la kujadili mpango huo wa usalama ulio endelevu ,wadau wamesikitika vifo vya barabarani bado vinaripotiwa miongoni mwa watembea miguu na waendesha pikipiki. Katika makala ya Siha Nj...
Majanga yanaweza kusababisha matatizo ya afya ya akili miongoni mwa watoto 06.06.2026 9:43
Mataifa ya Afrika yameshuhudia mafuriko katika miaka ya hivi karibuni ,hali ambayo imesababisha wananchi wengi kulazimika kuhama makazi yao Nchini Kenya ,ukanda wa magharibi ,katika eneo la Busia,mafuriko hayo yamevuruga kalenda za wanafunzi wa shule ,watoto wengi wakishindwa kuendelea na shule au kukubaliana na msongamano kwenye shule chache ambazo ziko maeneo salama Hali hii imewasababisha chang...
Mwendelezo wa mlipuko wa Ebola DRC na namna wenyeji wanavyojikinga 30.05.2026 9:37
Watu 220 wamefariki kwenye mlipuko wa Ebola unaohusishwa na virusi adimu vya Bundibugyo huku wengine zaidi ya 1000 wakiwa wameambukizwa Mlipuko huu hatari umesababisha baadhi ya mataifa kufunga mipaka yake na kuweka masharti magumu ya tahadhari
Kwenye kapu la sekta ya afya kufuatia kongamano la Africa Forward 22.05.2026 10:08
Baadhi ya makubaliano yalitotangazwa na Ufaransa baada ya siku mbili ya kongamano la Africa Forward ni ufadhili kwa uzalishaji wa dawa na chanjo hapa barani Afrika. Shirika la Unitaid pia lenye ushirikiano na Ufaransa lilitangaza kuratibu mchakato wa kuzalishwa dawa mpya ya kuzuia virusi vya HIV ,Lenacapavir kuzalishwa Afrika Kusini. Na kwenye viungo vingine vilivyosheheni majadiliano ya kuimari...
Mashirika ya kiraia Afrika yanataka nchi za Afrika kuwa na taratibu za pamoja kudhibiti magonjwa 16.05.2026 9:37
Taratibu hizo za pamoja yatahakikisha kuwa nchi za Afrika zinaweka bajeti kwenye sera ya uchumi na kuipa kipau mbele ufadhili wa afya
Watalaam wasisitiza uwekezaji wa utafiti wa DNA barani Afrika 05.05.2026 9:58
Utafiti unaoangazia vinasaba katika ukanda wa Afrika unaweza kuwa jawabu kwa ubainishaji potovu,gharama ya juu ya matibabu na usugu wa vimelea . Kwa kuanzia , Mashirika matatu ya Afrika ya kitafiti yametangaza mkataba wa dola milioni 3 nukta 5 ambao utawekezwa kwenye utafiti huu wa DNA barani . Mashirika haya yakiwa ni Biolinx Africa, YTO Foundation yenye makao Ivory Coast na Nextgen Molec...
Mpango wa kuongeza ujuzi wa wahudumu wa afya kwa kutumia teknolojia 28.04.2026 10:12
Ufadhili wa afya ukanda wa Afrika umezidi kupungua tangu kusitishwa kwa ufadhili mkubwa wa kigeni Pengo hilo linamanisha serikali nyingi hazina uwezo wa kifedha wa kutosha kuendelea kutoa mafunzo endelevu ya wahudumu wa afya. Katika kujaribu kutatua changamoto hii ,mpango wa ECHO unaowasaidia wahudumu wa afya kujifunza wakati wanapoendelea kuwahudumia wagonjwa ,umekuja kuleta matumaini.
Mataifa ya Afrika mbioni kuboresha mkataba wa kupambana na majanga 23.04.2026 10:07
WHO ilitoa nafasi zaidi kwa mataifa ya ulimwengu kujadililiana zaidi kuhusu vipengee muhimu kwenye mkataba wa kukabiliana na majanga ya kidunia Vipengee hivyo ni pamoja namna mataifa yanaweza kunufaika kutokana na mchango wao kwenye tafiti za kisayansi ,vimelea vinavyotoka kwenye mataifa yao na usawa wakati wa usambazaji wa chanjo au dawa
Miaka mitatu tangu Sudan kuingia kwenye mzozo huduma za afya zimedorora 16.04.2026 9:19
Asilimia 37 ya vituo vya afya nchini Sudan vimeharibiwa wakati wa mapigano na haviwezi kutoa huduma za afya Shirika la madaktari wasio na mipaka,MSF limekuwa likiwahudumia wagonjwa wenye majeraha ,waathiriwa wa magonjwa ya milipuko na waathiriwa wa ubakaji. Hali ya usalama imeilazimu MSF kusitisha huduma katika maeneo kadhaa baada ya kushuhudiwa mashambulizi ya moja kwa moja kwenye vituo vya afya...
Replaio er ikke podcastudgiver; programmernes navne, coverbilleder og lyd tilhører deres ophavsmænd og distribueres via offentlige RSS-feeds.