Goodluck Joseph
Wanangu podcast
This podcast is hosted by Goodluck Joseph, a curious guy who likes to share all the things he finds interesting in the form of a podcast episode. In other words, this podcast is an extension of his personality and more. Expect to hear topics that range from music, movies, and books to random ideas, all presented in a creative manner.
Určitě navštivte web podcastu a podpořte jeho tvůrce: rss.com
Kde poslouchat?
Podcasty v aplikaci Replaio Radio Už brzyPodcasty míří do aplikace už brzy. Nainstaluj si ji teď a jako první uvidíš úplně nový pohled na podcasty
Epizody
Episode 93 | Fukuto la Ubunifu Feat. Araskies 25.05.2026 19:00
Katika episode hii, Host anamkaribisha “mgeni mwenyeji” Araskies, kwa mazungumzo yenye msukumo kuhusu kile anachokiita “Fukuto la Ubunifu” hali ya kutotulia hadi pale unapotekeleza na kukamilisha wazo au ndoto uliyonayo. Ndani ya dakika chache tu, wanagusia mambo mengi yenye kuhamasisha, kukuamsha kutoka kitandani, na kukusukuma kuchukua hatua kuelekea ndoto zako.
Episode 92 | Falsafa za Niccolò Machiavelli (The Prince) 18.05.2026 18:03
Katika episode hii, kwa lugha rahisi tunagusia kitabu cha 'The Prince' kilichoandikwa na Niccolò Machiavelli mnamo karne ya 16, kikiwa ni moja ya vitabu vyenye ushawishi mkubwa katika siasa na uongozi duniani. Tunaangazia hoja zake maarufu kama vile 'ni bora kiongozi kuogopwa kuliko kupendwa' na jinsi kilivyoshauri viongozi kulinda tawala zao.
Episode 91 | Gharama ya Kuwa na Fahamu. 04.05.2026 18:22
Katika episode hii, host ana-share wazo lililomjia hivi karibuni kuhusu fahamu (consciousness), lililomchochea kuanza kuchunguza kwa kina maana halisi na uhalisia wa dhana hiyo.
Episode 90 | Unabomber: Kwa Nini Alitaka Maisha Bila Teknolojia? 27.04.2026 17:13
Katika episode hii tunaingia ndani ya kisa cha Ted Kaczynski, maarufu kama "Unabomber", mwanazuoni aliyeacha taaluma yake na kuanza kushambulia wanasayansi kwa mabomu aliyoyatengeneza mwenyewe. Nini hasa kilimsukuma kufikia hatua hiyo? Pia, tunaangazia mawazo yake kuhusu teknolojia na jamii, hasa kupitia andiko lake la "Industrial Society and Its Future". Ni simulizi fupi lakini nzito na ya kukufa...
Episode 89 | "Chagua Sumu Yako" 20.04.2026 11:33
Episode hii inaelezea wazo la kwamba kila maamuzi maishani yana ugumu wake, hakuna njia iliyo rahisi. Kupitia mifano inaonyesha kuwa uamuzi wa kweli si kati ya rahisi na ngumu, bali ni kati ya aina tofauti za ugumu, na inakuhimiza uchague ule unaolingana na maisha unayotaka.
Episode 88 | Kweli ya Leo Sio ya Jana 13.04.2026 15:28
Katika episode hii, host anachambua dhana ya “kila zama na kitabu chake” na jinsi uhalisia unavyoundwa na nyakati tunazoishi. Aidha, anaeleza kuwa licha ya kila mtu kuwa na mtazamo wake binafsi, mitazamo ya pamoja huwa na nguvu kubwa katika namna tunavyoitazama na kuielewa dunia. Karibu!
Episode 87 | Jinsi ya Kuwa Mbunifu 06.04.2026 17:46
Katika episode hii, host anazungumzia jinsi ya kuondoa vikwazo vinavyokuzuia kuwa mbunifu, kuanzia kuacha kufikiria sana, kuchukua hatua hata kama hauko tayari, jinsi ya kushughulika na maoni ya watu, hadi kujenga utambulisho wako binafsi. Kama umewahi kuhisi una mawazo mengi lakini huchukui hatua au unaanza kitu halafu unakata tamaa njiani, basi hii episode ni kwa ajili yako. Karibu!
Episode 86 | Hatua ya Mwisho: Mwamwindi Vs. Dr. Kleruu 30.03.2026 16:22
Katika episode hii, tunachambua tukio la kihistoria la mwaka 1971 ambapo mkulima Saidi Abdallah Mwamwindi alimpiga risasi na kumuua Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dkt. Wilbert Kleruu, katika kijiji cha Ismani. Tukio hilo lilihusishwa na mvutano uliotokana na sera za ujamaa na utaifishaji wa mashamba, na baadaye ikawa kesi kubwa ya kisheria na kisiasa nchini Tanzania. Tunaangazia kwa undani kilichotokea s...
Episode 85 | Marekani Dhidi ya Iran (Simulizi ya filamu) 23.03.2026 19:08
Episode hii inasimulia filamu ya kusisimua iitwayo Argo (2012) iliyoongozwa na pia kuigizwa na Ben Affleck, ikihusu hadithi ya kweli ya operesheni ya CIA ya mwaka 1979 ambapo afisa wa ujasusi Tony Mendez aliwaokoa wanadiplomasia sita wa Marekani waliokuwa wamejificha mjini Tehran wakati wa mgogoro wa mateka wa Iran.
Episode 84 | Kwa Nini Mataifa Yanakimbilia Tena Mwezini? 16.03.2026 13:01
Kwa nini mataifa yanarudi tena kushindania kwenda Mwezini baada ya zaidi ya miaka 50? Episode hii inaangazia kurudi kwa mbio za anga (Space race) kwa kuanzia na historia ya ushindani wa Vita Baridi kati ya Marekani na Urusi uliyosababisha mafanikio makubwa kama uzinduzi wa setelaiti ya kwanza mwaka 1957 na kutua kwa binadamu Mwezini mwaka 1969 hadi mbio hizi mpya ambapo mataifa kama China, India,...
Episode 83 | Watoto wa Mtaani by Moni Centrozone (Album review) 09.03.2026 25:57
Episode hii inaangazia uchambuzi wa wimbo kwa wimbo wa albamu ya kwanza ya Moni Centrozone, “Watoto wa Mtaani.” Albamu hii inazungumzia nini hasa? Na imefanikiwa vipi kuwasilisha ujumbe na dhamira iliyokusudiwa? Karibu tuichambue pamoja!
Episode 82 | AI Imeathiri Vipi Upigaji wa Muziki Redioni? Feat. Araskies 02.03.2026 20:40
Episode hii inaangazia jinsi ujio wa akili bandia (AI) ulivyoathiri upigaji wa muziki katika redio. Je, wasikilizaji wanajua kwamba baadhi ya nyimbo wanazopigiwa redioni ni za AI?
Episode 81 | The Young Skywalker (Album review) 23.02.2026 31:45
Episode hii inaangazia uchambuzi wa wimbo kwa wimbo wa album ya “The Young Skywalker” kutoka kwake mkongwe wa masuala ya utangazaji Fredrick Bundala a.k.a Skywalker. Je, ujio wake rasmi katika muziki unahimili Mizania na mategemeo yanayokuja na uzito wa jina lake? Karibu.
Episode 80 | Stori ya Nike Cortez: Kuanzia riadha hadi kwa wahuni 16.02.2026 22:36
Episode hii inaangazia safari ya Nike Cortez kutoka kuwa kiatu cha riadha kilichotengenezwa na Nike hadi kuwa alama yenye uzito wa kitamaduni huko Los Angeles huku kikihusishwa na magenge ya wahuni.
Episode 79 | Grammy 2026: "ICE OUT" ni nini? 09.02.2026 12:53
Episode hii inaangazia ujumbe wa “ICE OUT” uliovaliwa na kutamkwa na watu mashuhuli wengi katika sherehe na utoaji wa tuzo kubwa za muziki duniani za Grammy mwaka 2026. Ni nini hasa maana yake na kwanini watu wengi waliona ni wazo zuri kusambaza ujumbe huo? Karibu.
Episode 78 | Falsafa za Yuri Boyka 02.02.2026 11:01
Host anatukumbusha umuhimu wa kugeuza hasi kuwa chanya katika kila gumu tunalopitia huku akitoa mfano kutoka katika moja ya filamu maarufu za sanaa za mapigano (Martial arts) inayoitwa Undisputed III: Redemption. Song of the week: Dilly Darling by Nikita Kering.
Episode 77 | Mwanajua by Dizasta Vina (Uchambuzi) 26.01.2026 23:03
Baada ya episode ya 75 kuchambua wimbo wa “Mbuzi” wa Dizasta Vina, watazamaji wa Wanangu podcast Youtube wameomba uchambuzi wa wimbo wake wa “Mwanajua” kutoka katika album yake ya The Verteller (2020). Episode hii imekuja kutuliza kiu yao.
Episode 76 | Malezi bora ni yapi? 19.01.2026 13:42
Katika episode hii, host ana-share mawazo yake juu ya malezi, ikichangiwa na mazungumzo aliyowahikufanya na watu mbali mbali katika maisha yake ya kila siku pamoja na uzoefu wake binafsi.
Episode 75 | Mbuzi by Dizasta Vina (Uchambuzi) 12.01.2026 18:17
Episode hii inahusu uchambuzi wa wimbo wa “Mbuzi” wa Dizasta Vina kutoka katika album yake ya A Father Figure (2024). Host anachambua Muundo, uandishi, dhamira kuu, mistari pendwa na mchango wa wimbo huu katika maisha yetu ya kila siku. Karibu!
Episode 74 | Kuzima kwa MTV 05.01.2026 8:24
Kufuatia Paramount kuzifunga chaneli za MTV zilizokuwa zikipiga muziki pekee sehemu mbali mbali duniani, episode hii inakuletea makala fupi iliyolenga kukujuza kuhusu kuchipua, kukua, kubadilika na hatimaye kuporomoka kwa brand hii iliyoweka alama mioyoni mwa watu wengi.
Episode 73 | Consistency 29.12.2025 13:22
Katika episode hii ya mwisho kwa mwaka 2025, host anapata nafasi ya kuzungumza na rafiki yake kuhusu alichojifunza ndani ya mwaka huo, kazi za sanaa alizozifurahia zaidi, matumizi ya AI na mengineyo.
Episode 72 | Little rooms 22.12.2025 12:19
Kupitia hotuba ya Andre 3000 kwenye Rock n' roll hall of fame 2025, tunakumbushwa kwamba mafanikio mengi makubwa duniani huanzia kwenye vyumba vidogo sana (Little rooms).
Episode 71 | Netflix yazidi kutanua mbawa 15.12.2025 10:53
Netflix yainunua Warner Bros. kwa bilioni za kimarekani 82.7. Hii inamaanisha nini kwenye kiwanda cha filamu duniani?
Episode 70| Makala ya Diddy 08.12.2025 14:13
Episode hii inaangazia makala (Documentary) mpya iliyotolewa na 50 Cent kumuhusu hasimu wake Diddy.
Episode 69 | Hiphop vs Singeli 01.12.2025 10:33
"Hiphop na Singeli ni aina mbili za muziki tofauti kabisa!" Sikiliza episode hii uone jinsi gani kauli hii inavyopoteza mashiko.
Podobné podcasty
Replaio není vydavatelem podcastů; názvy pořadů, obálky a audio patří jejich autorům a šíří se přes veřejné RSS kanály