Koleman Thompson

MAISHA na Koleman Thompson

Karibu kwenye podcast yangu, MAISHA: Swahili Edition! Dhumuni la podcast hii ni kuzungumzia safari zetu za maisha na mambo ambayo tumepitia na kujifunza. Kwa majina naitwa Koleman Thompson. Nililelewa katika jingo la Utah, Marekani. Nilijifunza Kiswahili nilipotumikia kama Mmisionari kwa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho. Pia, nina podcast nyingine inayoitwa “MAISHA: English Edition”. Ukitaka kusikiliza kuhusu maisha ya watu waongeao Kiingereza, utafute hiyo podcast. Asante sana kwa kusikiliza!

Určitě navštivte web podcastu a podpořte jeho tvůrce: podcasters.spotify.com

Autor

Koleman Thompson

Kategorie

Education

Web podcastu

podcasters.spotify.com

Nejnovější epizoda

7. čvn 2025

Kde poslouchat?

Podcasty v aplikaci Replaio Radio Už brzy

Podcasty míří do aplikace už brzy. Nainstaluj si ji teď a jako první uvidíš úplně nový pohled na podcasty

Stáhnout z Google Play Nainstaluj zdarma Android 10 mil.+ stažení · hodnocení 4,7+ iOS už brzy

Epizody

7. Sean Olson na Mzungu Mswahili | Two Americans do a Podcast in Swahili 07.06.2025

Jiunge nasi tunavyozungumzia kwa nini tunapenda Kiswahili na utamaduni wa Afrika. Mfuatilie Sean kwenye TikTok @seanolson0237 na unifuatilie mimi kwenye TikTok @mzungu_mswahili

6. Lizbeth Leonard | Maisha ya Vijana wa Tanzania 25.08.2024

Lizbeth Leonard ni mtu mzuri sana ambaye anampenda Mungu na familia yake sana. Nilibarikiwa sana kuishi na yeye na familia yake wakati ambao nilikuwa Tanzania. Aliboresha maisha yangu sana kwa mfano na maneno yake. Kwenye kipindi hiki, tulizungumza sana kuhusu maisha ya vijana wa Tanzania (ikijumuisha umuhimu wao, changamoto zao, na utatuzi kwa changamoto zao). Natumaini kwamba wengine watafaidika...

5. Mwalimu Vinold John | Utamaduni na Lugha ya Waswahili 15.08.2024

Vinold John ni mwalimu bora kabisa na nimefurahi kujifunza kutoka kwake mara kwa mara kwenye progamu hii hapa Tanzania. Anapenda sana kufundisha kuhusu utamaduni na lugha ya Waswahili. Katika kipindi hiki, tulizungumza mawili matatu kuhusu mada hizo, pamoja na umuhimu wa subira katika maisha yetu. Furahie! Ukitamani kujifunza kutoka kwa mwalimu Vinold, unaweza kumkuta kwa njia zifuatazo: Email - v...

4. Erick Mwasha | Kuishi Maisha ya Furaha 08.08.2024

Jiunge na mimi na Rafiki yangu Erick tukizungumzia masuala makubwa ya maisha kama vile umuhimu wa kuwasaidia watu wengine, changamoto za maisha katika Tanzania, na kuishi vizuri na wengine!

3. Fredrick Charles | Maana ya Maisha na Umuhimu wa Amri za Mungu na Mpango Wake 19.07.2024

Katika kipindi hiki, Fredi na mimi tulizungumzia maana ya maisha kidini na kijamii. Fredi ni rafiki yangu mpya hapa Tanzania. Yeye ni mtu mwema sana na ana mawazo mazuri mengi kushiriki. Anapenda Mungu sana na pia anafuatilia mambo ya siasa na mpira. Tuliongea kuhusu mpango wa Mungu na umuhimu wa kupenda wengine katika maisha yetu. Alisimulia matokeo machache ya maisha yake pia. Mfurahie!

2. Grace Neema Lubango | Majaribu Magumu ya Maisha na Tofauti Kati ya Maisha ya Tanzania na Marekani 12.06.2024

Grace Neema Lubango ni rafiki yangu mwema. Alilelewa Tanzania na akahamia Marekani miaka kadhaa iliyopita. Katika kipindi hiki tulizungumzia sana tofauti kati ya maisha yake Tanzania na maisha yake Marekani. Aliweza kutoa ushauri mzuri sana. Pia, aligusia sana majaribu magumu ambayo amepitia maishani mwake na jinsi alivyoweza kumkaribia Mungu katika majaribu hayo. Nafiriki mtafaidika sana kwa kusi...

1. Kujitambulisha Kwangu, Dhumuni la Podkasti hii, na Historia Kidogo ya Maisha Yangu 08.06.2024

Katika episode hii, najitambulisha na kueleza dhumuni la podcast hii. Naeleza jinsi nilivyopata kujifunza Kiswahili na pia miujiza michache ambayo Mungu amenitendea katika maisha yangu. Asante kwa kusikiliza.

Poslouchej podcast MAISHA na Koleman Thompson v Replaio

Rádio a podcasty v jedné aplikaci - zdarma a bez registrace. Nainstaluj si ji ještě dnes a nepropásni premiéru

Stáhnout z Google Play

Replaio není vydavatelem podcastů; názvy pořadů, obálky a audio patří jejich autorům a šíří se přes veřejné RSS kanály