RFI Kiswahili

Wimbi la Siasa

News SW ↓ Επεισόδια: 35

Makala ya Wimbi la Siasa inakupa fursa ya kufahamu masuala ya kisiasa yanayoendelea ndani na nje ya Bara la Afrika. Kwenye Makala haya utapata habari ambazo zinakugusa moja kwa moja wewe msikilizaji. Kila wakati usikose kusikiliza Makala ya Wimbi la Siasa

Μην παραλείψεις να επισκεφτείς τη σελίδα του podcast και να στηρίξεις τον δημιουργό: www.rfi.fr

Δημιουργός

RFI Kiswahili

Κατηγορία

News

Ιστοσελίδα του podcast

www.rfi.fr

Τελευταίο επεισόδιο

30 Σεπ 2026

Πού να ακούσεις;

Podcast στην εφαρμογή Replaio Radio Έρχεται σύντομα

Τα podcast έρχονται σύντομα στην εφαρμογή. Εγκατάστησέ την τώρα και δες πρώτος μια εντελώς νέα προσέγγιση στα podcast

Κατέβασέ το από το Google Play Δωρεάν εγκατάσταση Android σχεδόν 10 εκατ. λήψεις · βαθμολογία 4,8 iOS σύντομα

Επεισόδια

Viongozi wa ODM wanaweza kuungana tena baada ya mpasuko wa chama ? 01.04.2026

Chama siasa cha Orange Democratic Movement-ODM kinaendelea kugawanyika, kuelekea uchaguzi mkuu mwaka 2027 nchini Kenya. Tangu kufariki dunia kwa Raila Odinga, mwasisi wa chama hicho kikubwa cha upinzani, viongozi waandamizi wa ODM wameshindwa kuelewana kuhusu kuendelea kumuunga mkono rais William Ruto, anayetarajiwa kuwania tena urais kwa muhula wa pili. Nini hatima ya chama hiki ?

DR Congo: Ni wakati mwafaka wa kuibadilisha katiba ya DRC ? 25.03.2026

Mjadala wa kuibadilisha katiba nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, umepamba moto. Wanasiasa wanaoegemea upande wa rais Felix Tshisekedi na chama chake cha UDPS wanaunga mkono mchakato wa katiba kubadilishwa. Upinzani wakiongozwa na naibu Spika wa Bunge la Seneti aliyejiuzulu Modeste Bahati Lukwebo, unapinga. Ni wakati mwafaka wa kuibadilisha katiba ya DRC ? 

Nini hatima ya vita vya Marekani na Israeli nchini Iran ? 18.03.2026

Ni wiki ya tatu sasa, baada ya Marekani na Israeli zilipoanza kutekeleza mashambulizi ya kijeshi nchini Iran. Mataifa hayo mawili yanasema lengo la mashambulizi hayo ni kuhakikisha kuwa inaharibu kabisa miundo mbinu ya Iran kutengeneza silaha za nyuklia. Rais wa Marekani Donald Trump, anasema vita hivi vitamalizika hivi karibuni, lakini haifahamiki ni lini. Tunachambua.

Kenya: Je, ushirikiano wa serikali kati ya vyama vya ODM na UDA unafanikiwa ? 11.03.2026

Umepita mwaka mmoja tangu chama tawala nchini Kenya UDA na kile cha upinzani ODM, vilipoingia kwenye makubaliano ya kisiasa na kutaja mambo 10 kama vita dhidi ya ufisadi, kupunguza deni la taifa, ujumuishwaji ulio sawa serikalini kama baadhi ya mambo ya kushughulikia baada ya maandamano ya vijana ya mwaka 2024. Je, mwaka mmoja baadaye mambo hayo yametekelezwa kwa kiasi gani ?  Tunachambua.

Nini hatima ya vita vya Israel na Marekani nchini Iran ? 04.03.2026

Dunia inashuhudia vita katika ukanda wa Mashariki ya Kati, baada ya Marekani na Israeli kuishambulia Iran, tangu Februari 28. Rais wa Marekani Donald Trump na Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu wanataka Iran iache kutengeneza silaha za maangamizi, kuyaunga mkono makundi yenye silaha nje ya Iran na kubadilisha utawala. Kongozi wa kiroho Ayatolla Ali Khamenei, ameuawa katika vita hivyo. Nini...

Vita vya miaka minne nchini Ukraine, nini suluhu ? 25.02.2026

Imetia miaka minne, tangu Urusi ilipoivamia Ukraine, katika vita vikubwa tangu vile vya pili vya dunia barani Ulaya. Maelfu ya watu wameuawa, miji na miundo mbinu muhimu imeharibiwa nchini Ukraine. Rais Volodymyr Zelenskyy anasema mwenzake wa Urusi hajatimiza malengo yake ya vita. Kwanini suluhu haijapatikana miaka minne baadaye ?

Kenya: Kwanini chama cha ODM kimegawanyika kuelekea uchaguzi mkuu 2027 ? 18.02.2026

Joto la kisiasa limeendelea kupanda kwenye chama cha siasa cha ODM nchini Kenya kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2027. Chama hicho kilichoanzishwa zaidi ya miaka 20 iliyopita na aliyekuwa Waziri Mkuu Marehemu Raila Odinga, kimegawanyika kwa makundi mawili. Kundi moja linaongozwa na Oburu Oginga, kaka yake Raila, linamuunga mkono rais William Ruto. Kundi lingine, linangozwa na Edwin Sifuna, Katibu M...

Nini kikwazo cha utekelezwaji wa mkataba wa kusitisha vita nchini DRC ? 11.02.2026

Wawezeshaji na wasuluhishi wa mzozo wa Mashariki mwa DRC kutoka Umoja wa Afrika, wanataka usitishwaji wa vita na utekelezwaji wa mkataba wa amani wa Washington na kuheshimu mchakato wa Doha. Ni kwanini inakuwa vigumu kutekeleza mkataba huo  kuheshimu maelewano ya Doha ? Tunachambua.

Mazungumzo ndio suluhu ya changamoto zinazoikabili DRC ? 04.02.2026

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Felix Tshisekedi amesema serikali yake ipo tayari kuongoza mazungumzo kati ya Wakongomani, ili kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili nchi hiyo, hasa utovu wa usalama, mashariki mwa nchi hiyo. Hata hivyo, Chama cha "Ensemble pour la République, kinachoongozwa na mwanasiasa mashuhuri wa upinzani Moise Katumbi, kinasema mazungumzo hayo yanaweza kufanyik...

Kenya: Nini suluhu ya mzozo wa chama cha ODM ? 28.01.2026

Chama cha ODM kilichoanzishwa na aliyekuwa Waziri Mkuu  nchini Kenya Hayati Raila Odinga, kinapitia mgawanyiko wa kisiasa kuhusu kumuunga mkono rais William Ruto kuwania urais kwa muhula wa pili. Viongozi  wa chama hicho wamegawanyika kuhusu mpango huo kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2027. Mvutano  huu unamaanisha nini ?

Άκου το podcast Wimbi la Siasa στο Replaio

Ραδιόφωνο και podcast σε μία εφαρμογή - δωρεάν, χωρίς εγγραφή. Εγκατάστησέ την σήμερα και μη χάσεις την πρεμιέρα

Κατέβασέ το από το Google Play

Το Replaio δεν είναι εκδότης podcast - τα ονόματα των εκπομπών, τα εξώφυλλα και ο ήχος ανήκουν στους δημιουργούς τους και διανέμονται μέσω δημόσιων ροών RSS