United Nations

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

News SW ↓ Epizody: 208

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Určitě navštivte web podcastu a podpořte jeho tvůrce: news.un.org

Autor

United Nations

Kategorie

News

Web podcastu

news.un.org

Nejnovější epizoda

9. říj 2026

Kde poslouchat?

Podcasty v aplikaci Replaio Radio Už brzy

Podcasty míří do aplikace už brzy. Nainstaluj si ji teď a jako první uvidíš úplně nový pohled na podcasty

Stáhnout z Google Play Nainstaluj zdarma Android téměř 10 mil. stažení · hodnocení 4,8 iOS už brzy

Epizody

AI iwe somo shuleni, asema mtoto Murad 09.10.2026

Hivi karibuni hoja ya watoto na AI ilimulikwa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa hususan jinsi ya kulinda haki za watoto. Je watoto wenyewe wananufaika vipi nayo? Wanataka nini kifanyike ili iwaletee maendeleo Chanya? Tuungane na Assumpta Massoi kutoka Nairobi Kenya akizungumza na mtoto anayeanza kwa kujitambulisha.

09 OKTOBA 2026 09.10.2026

Hii leo jaridani tunaangazia mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel mwaka 2026, maoni ya vijana kuhusu Akili Mnemba, na mchezaji wa soka au kandanda nchini Tanzania. • Kamati ya tuzo ya Nobel nchini Norway imemtangaza Navanethem “Navi” Pillay kuwa mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel mwaka 2026 kutokana na mchango wake katika kukuza amani na sheria za kimataifa. • Katika masuala ya Akili Mnemba au AI hivi...

Fatuma Issa Suleiman awataka wasichana kutokata tamaa kufuata ndoto zao katika soka 09.10.2026

Nchini Tanzania, mchezaji wa soka au kandanda, Fatuma Issah Suleiman amegeuza changamoto na kukatishwa tamaa kuwa chachu ya kufuatilia ndoto yake katika mchezo wa soka. Licha ya kukosa uungwaji mkono mwanzoni na baadaye kupata jeraha kubwa lililomweka nje ya uwanja kwa miezi kadhaa, Fatuma hakukata tamaa na hatimaye akafanikiwa kufikia kiwango cha kuchezea timu ya taifa. Kulikoni? tuungane na Cynt...

Navi Pillay, Kamishna Mkuu wa zamani wa Umoja wa mataifa kuhusu Haki za Binadamu ndiye mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel 2026 09.10.2026

Kamati ya tuzo ya Nobel nchini Norway imemtangaza Navanethem “Navi” Pillay kuwa mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel mwaka 2026 kutokana na mchango wake katika kukuza amani na sheria za kimataifa. Selina Jerobon na maelezo zaidi.

08 OKTOBER 2026 08.10.2026

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina. Umoja wa Mataifa unaonya kwamba pengo la kidijitali linaweza kubadilika kuwa pengo la Akili Mnemba (AI), na hatimaye kuwa pengo la maendeleo, usalama na mamlaka ya nchi. Shrika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo UNDP linatoa takwimu likisema barani Afrika kwa mfano, ni chini ya asilimia mbili ya uwezo wa vituo vya kuhifadhi na kuchakata data duni...

07 OKTOBA 2026 07.10.2026

Hii leo jaridani tunakuletea kipindi maalumu cha mahojiano yanayozingatia tangazo la jana kutoka serikali ya Kenya ya kwamba mtu mmoja amekufa kwa ugonjwa wa Ebola ya virusi vya Bundibugyo nchini humo. Kufuatia tangazo hilo Assumpta Massoi wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa jijini Nairobi, Kenya amezungumza na Mwakilishi wa shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani,(WHO) nchini humo Dkt....

Walinda amani wa Umoja wa Matifa nchini DRC wapatiwa Tuzo 06.10.2026

Walinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini DRC walipatiwa medali za Umoja wa Mataifa. Shuhuda wetu ni Kapteni Hamis Milyango, tuungane naye.

Walinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini DRC na harakati za kudhibiti Ebola 06.10.2026

Kufuatia mlipuko wa Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, (DRC) Walinda amani wa Umoja wa Mataifa nao wanachukua hatua kuhakikisha kuwa ugonjwa huo hauleti changamoto kwenye harakati za ulinzi wa raia. Je wanafanya nini? Tuungane na Private Lazaro Mlyuka kutoka Kikosi cha Tanzania cha walinda amani wa Umoja wa Mataifa kinachohudumu nchini humo.

Mlipuko wa Ebola ukiendelea Ituri na Kivu Kaskazini nchini DRC, maisha ya watoto yaparaganyika 06.10.2026

Watoto wachanga wawili, mmoja mwenye umri wa miezi 7 na mwingine miezi minane,ni miongoni mwa watoto ambao maisha yao yamebadili baada ya wazazi wao kufariki kwa ugonjwa wa Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, na sasa Umoja wa Mataifa unataka hatua zichukuliwe kuwalinda wao na wengine wengi. Flora Nducha na maelezo zaidi.

06 SEPTEMBA 2026 06.10.2026

Hii leo jaridani tunaangazia Ebola nchini DR Congo na kazi ya walinda amani nchini humo. • Watoto wachanga wawili, mmoja mwenye umri wa miezi 7 na mwingine miezi minane,ni miongoni mwa watoto ambao maisha yao yamebadili baada ya wazazi wao kufariki kwa ugonjwa wa Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, na sasa Umoja wa Mataifa unataka hatua zichukuliwe kuwalinda wao na wengine wengi. •...

Jifunze Kiswahili: Maana ya neno, MAFAMBA 05.10.2026

Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, leo Mchambuzi wetu Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili huko Zanzibar, BAKIZA anafafanua maana ya neno, MAFAMBA.

05 OKTOBA 2026 05.10.2026

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina. Wiki iliyopita katika Ofisi ya Kenya ya Utafiti wa Kilimo na Mifugo, KALRO iliyoko jijini Nairobi nchini Kenya, FAO nchini Kenya kwa kushirikiana na serikali walizindua mradi wa SoilFer. Mradi huu unahusisha kuwa na ramani ya aina za udongo za taifa hilo la Afrika Mashariki ili kusaidia wakulima kuongeza tija kwenye kilimo. Je ina maana gani? Na kwa nini...

“Maisha yanaweza kuwa mabaya kwa sababu ya vita, lakini tunaimba tu… na ninapoimba inanifanya kusahau matatizo yote na kuwa katika wakati huo." - Toussaint Chiza 02.10.2026

Mwaka huu ni miaka 75 tangu ulipopitishwa mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Wakimbizi mwaka 1951 na tangu wakati huo mamilioni ya wakimbizi wamepatiwa hifahi, usalama na maisha yao kuokolewa na kubadilishwa kupitia mpango wa mkataba huo wa kuwapeleka wakimbizi katika nchi ya tatu kuanza upya maisha yao. Miongoni mwa wafaidika wa mpango huo ni mgeni wetu kwenye mada ya leo aliyekimbia vita Jamhuri ya...

02 OKTOBA 2026 02.10.2026

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina. Mwaka huu ni miaka 75 tangu ulipopitishwa mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Wakimbizi mwaka 1951 na tangu wakati huo mamilioni ya wakimbizi wamepatiwa hifahi, usalama na maisha yao kuokolewa na kubadilishwa kupitia mpango wa mkataba huo wa kuwapeleka wakimbizi katika nchi ya tatu kuanza upya maisha yao. Miongoni mwa wafaidika wa mpango huo ni mgeni wetu kwe...

01 OKTOBA 2026 01.10.2026

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina. Miongoni mwa mikutano iliyochukua nafasi kubwa wakati wa Mjadala Mkuu wa ngazi ya juu wa Kikao cha 81 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa , UNGA81 ni kuhusu Akili Mnembaa u AI. Pamoja na changamoto zake lakini AI inauweza mkubwa wa kusaidia jamii kutatua changamoto na hata kuondoa taarifa potofu. Waandishi wa habari hawakuachwa nyuma nao walikuwa na mikut...

30 SEPTEMBA 2026 30.09.2026

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina, tukimsikiliza mmoja wa washiriki wa UNGA81ulioanza tarehe 22 Septemba na kufunga pazia Jumatatu, tarehe 28 Septemba mwaka huu wa 2026 Paul Siniga, ambaye pamoja na wadhifa mwingine alionao ni mchechemuzi wa Tanzania katika utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu SDGs na mleta mabadiliko wa watoto kupitia shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wato...

29 SEPTEMBA 2026 29.09.2026

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina. Dunia hivi sasa imegubikwa na mazingira ya uhalifu yanayozidi kuwa magum ukila uchao. Umoja wa Mataifa unasema kutokana na mazingira hayo huduma, miundombinu na teknolojia vinaweza kutumiwa vibaya na wahalifu. Hii ni pamoja na mienendo mipya inayojulikana kama “uhalifu kama huduma” na “vurugu kama huduma. Ni kwa kuzingatia hilo, Ofisi ya Umoja wa Mataifa...

28 SEPTEMNA 2026 28.09.2026

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina. Hii leo tunaangazia sekta ya afya barani Afrika na kuzungumzia hilo mwenzangu Leah Mushi amezungumza na Mkurugenzi wa shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni Kanda ya Afrika Profesa Mohamed Janabi. Suala la kwanza kutaka kufangamu kutoka kwake ni je mkutano wa Ngazi ya Juu kuhusu maandalizi dhidi ya majanga ya milipuko ya magonjwa ulifanyika mwis...

25 SEPTEMBA 2026 25.09.2026

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina. Hapa katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa leo unafanyika mkutano wa Ngazi ya Juu kuhusu maandalizi dhidi ya majanga ya milipuko ya magonjwa na kama nilivyokudokeza kuwa tutakuwa na maoni na ushauri wa baadhi ya wananchi wa Afrika Mashariki kwa viongozi wanaoshiriki mkutano huo, tunaanzia nchini Uganda, kisha tuelekee nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya C...

24 SEPTEMBA 2026 24.09.2026

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina. “Kuwa mkimbizi si chaguo wala hiyari ni shuruti inayotokana na sababu mbalimbali ikiwemo kutokuwa amani sababu ya vita na kila mtu anaweza kuwa mkimbizi siku moja.” Hiyo ni kauli ya Marry Nyiriak Maker Balozi Mwema wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR ambaye amezungumza na Flora Nducha wa Idhaa hii kandoni mwa mjadala Mkuu wa Baraz...

23 SEPTEMBA 2026 23.09.2026

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina. Kesho Septemba 24 viongozi wa dunia wanaokutana hapa New York, Marekani kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa watakuwa na mkutano wa ngazi ya juu kuhusu ongezeko la kina cha maji ya bahari duniani. Hatimaye wanatarajiwa kupitisha azimio la kusaidia mataifa yanayokumbwa na madhara yatokanayo na ongezeko hilo. Kutoka Nairobi, Kenya, Assumpta Massoi kwa us...

22 SEPTEMBA 2026 22.09.2026

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina. Mabadiliko ya tabianchi hayawaathiri watu wote kwa kiwango sawa. Baadhi ya nchi zimejenga uchumi wao kwa miongo kadhaa kupitia matumizi makubwa ya nishati ya mafuta, huku nyingine zilizochangia kidogo katika uzalishaji wa gesi chafu zikikabiliwa na mafuriko, vimbunga, ukame, ongezeko la kina cha bahari na kupotea kwa njia za kujipatia riziki. Hili ndilo...

Balozi Thigo: Kuwalinda watoto zama za AI na teknolojia ni muhimu sana 21.09.2026

Kesho Jumanne tarehe 22 Septemba mbali ya kufunguliwa kwa mjadala Mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Matanfa wa UNGA81, kandoni mwa mjadala huo kutakuwa na Mkutano wa Ngazi ya Juu kuhusu Akili Mnemba, au Akili Unde AI, na Usalama wa watoto Mtandaoni. Balozi Philip Thigo anayehusika na masuala ya AI kutoka Kenya ni miongoni mwa watakaoshiriki mkutano huo amenieleza kwa nini suala hili ni muhimu katika...

Maandalizi ya Mjadala Mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa UNGA81 21.09.2026

Mjadala Mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataofa UNGA81 unafungua pazia kesho Jumanne ambapo mada mbalimbali zitajadiliwa kwa kina na nchi wanachama 193 wa Umoja wa Mataifa ikiwemo kuwasilisha tarifa zao wenzangu Leah Mushi na Anold Kayanda waafuatilia maandalizi ya mjadala huo.

21 SEPTEMBA 2026 21.09.2026

Hii leo jaridani tunaangazia ujumbe wa Katibu Mkuu na vijana kuhusu siku ya amani, ufunguzi wa UNGA81, Akili Mnemba, au Akili Unde AI, na Usalama wa watoto Mtandaoni. • Leo ni siku ya amani duniani ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, amepongeza watu wote mashinani wakiwemo watumishi wa kujitolea, wachechemuzi na viongozi wa mashirika ya kiraia wanaojitolea kwa hali na mali ku...

Poslouchej podcast Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu v Replaio

Rádio a podcasty v jedné aplikaci - zdarma a bez registrace. Nainstaluj si ji ještě dnes a nepropásni premiéru

Stáhnout z Google Play

Replaio není vydavatelem podcastů; názvy pořadů, obálky a audio patří jejich autorům a šíří se přes veřejné RSS kanály